Wakati mwaka unaelekea mwisho hatuna budi kutoa Shukrani.

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,670
---Shukrani kwa wote wale waliochangamsha Forum yetu tulicheka na kufurahi..

---Shukran pia ziwaendee wale wote waliotoa zingatio ambalo liliwagusa wengine na wengine kubadilika,

---Shukrani kwa wale ambao forum yetu haikuwatendea haki kwa kukutana na kadhia ya baadhi ya nyuzi zao kufutwa kwa makosa lakini hawakujitoa wakaonyesha uvumilivu

---Shukrani pia ziwaendee wale walioombaa kwa niaba yetu maombi yenu yametufikisha hapa tulipo,

---Shukrani kwa wale waliotunza amani utulivu upendo na kutuliza jazba hasira kwenye forum yetu kwa busara zao,

---Shukrani Kwa wale waliotujuza kwa breaking news za ukweli na uongo habari za huzuni na za furaha,

---Shukrani zije kwako wewe usiyetaka kuchangia kitu hata kama kunakuwa na mjadala mzito,

---Shukrani kwa wale wanatupiaga vivideo na vipicha visivyotija hali wanajua bando la internet liko juu,

---Shukrani kwa wote wale wapitaji wao ni kuangalia tu hawachangii wala kushauri

---Shukrani kwa wale wanaotaka kila mtu akubaliane na wazo lake anaempinga yeye anamwona kama msaliti, mjinga na mpumbavu,


Mungu ni mwema, tumuombe atuvushe salama
 
Shukrani kwa mwaka 2018 ndani ya jf,.wow safari zilikuwa nyingi lakini hatimaye zinaenda ukomo,.lol😂😂😂😂

Bye bye 2018......🍃🍃🍃🌺🌺🌺
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom