Wakati muda unayoyoma je ni ahadi zipi kati ya hizi zimesha tekelezwa na raisi wetu mpendwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati muda unayoyoma je ni ahadi zipi kati ya hizi zimesha tekelezwa na raisi wetu mpendwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHASHA FARMING, May 18, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa yaKanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5.[NENO BAYA]liza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12.Mtukula kupa[NENO BAYA] umeme kutoka Uganda - Kagera
  13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi yataifa ya umeme - Kagera
  14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosimaalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25.[NENO BAYA]liza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihuriona kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoaniKilimanjaro
  30.[NENO BAYA]liza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wawalimu - Kisesa Magu
  33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ilikuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia [NENO BAYA][NENO BAYA] za kidini, kikabilana kisiasa - Musoma
  36.Kulinda haki za walemavu - Makete
  37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita109 - Iringa mjini
  38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wamaji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arushamjini
  46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti– Ngorongoro
  49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuwezakupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo chaumwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo zakilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayondiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii -Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa -Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

  Quote

   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Si dhana, make hizi ahadi nilisikia zina thamani ya Triliion 300, na kuzitekeleza inahitajika Bajeti ya Serikali ya Marekani kwa
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu KOMANDOO naomba ufute kauli ya kusema rais wetu mpendwa si wote wanaompenda hasa mimi ni kutoka na utendaji kazi wake mbovu.mwite mhe,rais wa tz kwa tiketi ya CCM
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya,wakuu wapya wa wilaya,wakuu wapya wa mikoamwilaya mpya,mikoa mipya(ameamua kutekeleza vile asivoahidi,jamaa namkubali sana,then kuvunja baraza la mawazir,kuongeza wabunge kwa mamlaka alopewa,kumualika beckham kuja bongo kutalii,kuhutubia g8-ni heshima kubwa sana hii,,,,,kuhutubia wazee wa jiji la dar es salaam,kusafiri mara kwa mara,HAYA YOOOTE HAJAYAAHIDI ILA AMEYATEKELEZA
   
Loading...