Wakati muafaka sasa kumwaga hadharani undani wa wizi wa EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati muafaka sasa kumwaga hadharani undani wa wizi wa EPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 13, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wapenzi na wanachama wa Chadema:

  Kutokana na vita hii kali ya maneno kati ya CDM na CCM, naona imefika wakati muafaka kwa CDM kuweka hadharani ufisadi wote wa EPA -- jinsi CCM ilivyonufaika na mapesa hayo ya wananchi yaliyochotwa kwa ruhusa ya serikali ya CCM.


  Hapa nina maana kwamba ule ushahidi wa Jeetu Patel uwekwe hadharani -- maana katika sdtatement yake kwa kamati ya rais kuhusu uchotaji wa EPA, Jeetu Patel (aliyehojiwa na kamati hiyo) alieleza mengi -- ni nani na nani waliohusika na kupokea mapesa hayo.

  Hii itasadia kutafuta haki ambayo inaonoekana kufichwa sana na usiri mkubwa wa serikali ya CCM -- kitu ambacho ni hatari kwa amani yetu.

  Nasema kila itu kiwe hadharani na isiogopwe ile dhana ya eti ni kuingilia mahakama. Hii dhana ndiyo inawasaidia sana serikali ya CCM na mafisadi kuwaficha wananchi kile kilichotokea -- kwani kesi zenyewe ni magumashi tu.

  Namuomba Marando amwage siri yote ili kina Nape wafunge midomo yao mipana!!!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu Marando ni wakili makini na analijua hilo dude la uhuru wa mahakama. Mahakama ina haki zake ambazo huwa wakati mwingine zinavisha haki za wananchi kupata habari kwa wakati sahihi. Kwa mfano hizo kesi za Ufisadi zinaweza zikachukua muda mreefu na huruhusiwi kuziongelea nje ya mahakama kwa maana hiyo wananchi wanakosa habari kama ulizopendekeza hapo kwa wakati muafaka.

  Suala hapa ni kwamba mahakama zetu zibanwe ili ziharakishe kesi hasa hizo zenye national interest. Hukumu zitolewe tujue mbivu na mbichi. Inashangaza kuona kwamba JK ameteua majaji weeeengi lakini kesi bado zinacheleweshwa.
   
Loading...