Wakati muafaka Oryx Gas kupunguza bei za gesi zao, Mh. Waziri tetea Wananchi kwa maendeleo ya Tanzania

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Kuna siku niliweka mshangao wangu hapa bei ya mafuta ya Uganda ni ndogo kuliko Diesel ama petrol inayouzwa Tanzania. Nikawaza haya Malori yanayosomba mafuta wanasema wanapeleka Uganda wanabeba mafuta ama ulezi.

Leo naomba nieleze bei za gesi hapa nchini

Kumekuwa na mtafaruku sana hapa kati kwanini Oryx awataki kupunguza bei ya gesi yao wakati Mihan aka gesi ya taifa inauzwa kwa bei nzuri kabisa?

Mh Waziri wa Nishati kama unaweza kaa na Oryx wape mwelekeo na bei elekezi. Kwa wanaokumbuka mimi ni mmoja wa wadau wa gesi na nimekaa nao sana vikao niwape tu siri kuna kipindi ilibidi Mihan waungane kuwa na bei moja na Oryx ingawa walikuwa wako chini zaidi ya Oryx

Hapa kati ilipokuja gesi ya taifa walipokaa kushusha bei Oryx hawakukubali pamoja na Mihan kutoa vigezo vya kwanini wapunguze gesi bado wakashikilia bei zao.

Wananchi wengi walishanunua mitungi ya Oryx gas huko nyuma. Tunaomba taifa gas wakubali kupokea mitungi ya Oryx wakapige rangi wananchi wengi wanatamani kubadilisha lakni wamwamekuwa wakiwaza hili jambo

Wananchi watanzania tunaungana na wamiliki wa gesi ya taifa kwa kuona umuhimu wa wananchi kutumia gesi nzuri na inayokaa tofauti na misemo ya huko nyuma

Tunaomba Mh. waziri wakati muafaka Oryx wawe na bei sawa na taifa gas wananchi waweze kufurahia na kunufaika na kile watakachoweza kununua

Ahsanteni sana
 
Bora umeliona hili Mpwa,hivi gesi si ileile tu? Au Oryx ya kwao ni Bora zaidi? Au kwa vile wao ndio kampuni ya mwanzo kwahiyo wanajisahau?
 
kitaa kwetu watu waelewa gas yyt wanakubali kutumia imeisha oryx anapewa mihan or O gas, Taifa wanakubali, gas zote ni sawa tofaut ni rangi za mitungi tu, sasa ukikutana na ambao hawaelew ndo wanapigwa bei ya juu kwa kung'ang'ania oryx tu
 
Naona walimeshafanyia kazi nimekutana gari ya matangazo Sasa wanauza tsh 35000 badala ya tsh 48000 Bei ya mwanzo.
hilo gari haliwez pita sehemu zote na kukutana na mteja ambaye ndo mtumiajia wa nyumban, washushe bei kwa maagent ila wateja wapate unafuu, mbona mihan kashusha..
 
Back
Top Bottom