Kanusho: Bodaboda na Bajaji hawajapigwa marufuku kuingia katikati ya Jiji kuanzia Alhamisi 21 Aprili, 2022

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania imewatangazia kuanzia kesho Alhamisi bodaboda na bajaji zote hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji hilo.

bodaaa.jpg

=================

TAARIFA HII IMEKANUSHWA


DAR: BODABODA WAPEWA VITUO 9 MJINI

Baada ya kudaiwa bodaboda na Bajaji za biashara zimezuiwa kuingia Mjini Jijini Dar es Salaam, mamlaka zimekanusha zuio hilo na kuelezea kuna vituo 9 vimetengwa maalum kwa vyombo hivyo, mchakato ukishirikisha viongozi wa Bodaboda, TARURA, Jiji, Polisi na LATRA.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija amesema kuwa utaratibu wa vituo hivyo utawapa urahisi wa kushusha na kupakia abiria na siyo vituo holela kama ilivyokuwa awali.

Aidha, Msemaji wa Shirikisho la Vyama vya Madereva Pikipiki Mkoa wa Dar, Tito Lazaro amesema: “Utaratibu huo utapunguza uhalifu kwa kuwa kuna wasimamizi, mavazi maalum ya madereva, madereva watawasilisha nyaraka za utambulisho.

“Vituo hivyo ni Nasra Tower (Kariakoo), Sabasaba (Msimbazi), JK Park (Mnazi Mmoja), Fire, Mindu & Maliki (Upanda), Suwata (Kariakoo), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mnazi Mmoja na Kongo (Kariakoo).”
 
Boda Boda binafsi au Bajaji za Walemavu ndo wanatakiwa kufanya kazi mjini, lakini zingine zifanye kazi nje ya mjini

Huu utengano utendelea kuwasumbua sana viongozi wenye mamlaka husika.
 
Watu wamejiajiri na wanalea familia makatazo mengine watu wana kurupuka tu
Wamejiajiri sawa ila miji council nayo ina mipango yake
Umesahau kuwa hii marufuku ilikuwepo tangu zamani na wahusika walitii . Ruhusa ya kuingia jijini ilikuja baada ya daladala kuzuia kusimamisha watu mwaka juzi
Kwahiyo kabla ya mwaka juzi watu walikuwa hawajajiajiri?
 
Tutaelewa tu.

Jiji la Dar es Salaam limepiga MARUFUKU pikipiki na bajaj kuingia maeneo ya Kariakoo na Postal.

Asante sana mama kwa hilo la kuzuiliwa vyombo hivyo vya moto kuingia mjini maana is isingekuwa juhudi zako hakika lisingefanikiwa.
 
Back
Top Bottom