Wakati mafisadi wakiendelea kupeta, wanaodhaniwa kupiga mawe msafara wa JK wakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati mafisadi wakiendelea kupeta, wanaodhaniwa kupiga mawe msafara wa JK wakamatwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 18, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 18.10.2008 0010 EAT

  • 60 mbaroni kupiga msafara wa Kikwete

  *Kamanda wa Polisi azungumza
  *Msako zaidi waendelea kijijini

  Na Charles Mwakipesile, Mbeya

  SIKU mbili baada ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete kushambuliwa kwa mawe na watu wasiojulikana na wanausalama kumwagwa kwenye kijiji cha Kanga wilayani Chunya, watu zaidi ya 60 wamekamatwa na Polisi Mkoa wakihusishwa na tukio hilo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini.

  Habari za kiuchunguzi za Majira zilizopatikana jana na baadaye kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bw. Zelothe Stephen, zilisema msako mkali wa Polisi unaendelea, huku watu wengi wakiwa wamekamatwa, hakutaka kutaja idadi kamili.

  Kamanda Stephen alikiri kuwepo tukio la watu kukamatwa lakini alisema asingeweza kwa sasa kutaja idadi kamili ya waliokamatwa, kwani ni mapema mno.

  Jumatano iliyopita, watu wasiojulikana waliyatupia mawe magari ya viongozi waliofuatana na Rais katika ziara yake mkoani hapa, kutokana na hasira ya kutopata fursa ya kuzungumza na Rais na kumpa kero zao.

  Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kanga Mkwajuni, baada ya wananchi hao kusubiri kuanzia asubuhi kwa matarajio kuwa Rais angesimama na kuzungumza nao, lakini ilipofika saa 1.30 usiku msafara huo ulipita bila kusimama na ndipo watu hao wakachukua hatua hiyo.

  Katika toleo lake la jana gazeti hili liliripoti kuwa siri kuu iliyowafanya wanachi hao kufikia hatua hiyo ni kutokana na kukerwa baada ya kuona wameshindwa kutoa kero zao kwa Rais baada ya kumsubiri kwa muda mrefu.

  Baadaye, taarifa za Jeshi la Polisi zilithibitisha wanausalama kupelekwa kijijini hapo wakiwemo askari kanzu, ili kuchunguza na kujua kiini cha tatizo ikiwa ni pamoja na kukamata wahusika.

  Jana Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa Rais alisikitishwa na tukio hilo.
   
 2. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #2
  Oct 18, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiini cha tatizo ni UFISADI.......what else?
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  waachieni wananchi hawa, nendeni mkawakamate akina rostam ambao ni majambazi ya kutukuka, waliompiga mawe rais siyo wananchi, bali ni mafisadi walioifilisi nchi, na kufanya wananchi wawe na hasira kwa kiranja wao ambaye kazi yake ni kukenua meno hata kwa watu wanaoteseka
   
Loading...