Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Baada ya jana Real Madrid kuwafurusha Man City kwenye michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya,maarufu kama UCL,Real Madrid wamepanga miadi na wanajiji wenzao wa Atletico Madrid kupambana kwenye mchezo wa fainali ya UCL.
Fainali itapigwa mwezi huu kwenye uwanja wa kipekee wa Giusseppe Meazza,Italia. Fainali hiyo itakuwa marudio ya fainali ya timu hizohizo na kwenye michuano hiyohiyo ya mwaka 2014. Mwaka huo,Real Madrid chini ya Ancelotti walitwaa ubingwa wa UCL.
Mwaka 2015, wana La Liga wengine Barcelona chini ya Luis Enrique walitwaa ubingwa wa UCL wakiwashinda Juventus wa Massimiliano Allegri. Hadi hapo na kwa matokeo ya jana,La Liga powerhouses wako njiani kutwaa UCL kwa mara tatu mfululizo.
Kimsingi,La Liga imetawala soka la Ulaya. Lakini,wanazi hawakosekani. Wataendelea kudai kuwa Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama EPL ndiyo ligi bora duniani. Yaani ligi ya rugby iwe bora kwenye soka?!? La Liga wanapiga kimyakimya.