WAKATI LA DOWANS HALIJAISHA…Wadau wa pamba Tanzania kizimbani Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WAKATI LA DOWANS HALIJAISHA…Wadau wa pamba Tanzania kizimbani Uingereza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 29, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  WADAU wa kilimo cha pamba nchini wakiwamo wamiliki wa vinu vya kuchambulia wameshitakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Pamba mjini Liverpool, Uingereza, baada ya kushindwa kutekeleza mikataba waliyofunga na wanunuzi wa nje kutokana na kukosa pamba na wako hatarini kufilisiwa.

  Kutokana na unyeti wa suala hilo, Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi)
  amewasilisha ombi rasmi kwa Katibu wa Bunge kuhusu kusudio lake la kutaka kuwasilisha hoja binafsi kuhusu pamba.

  Machali akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema amewasilisha ombi kwa hati ya dharura na uharaka, ili aweze kuwasilisha hoja yake baada ya kuibuka ghafla kwa hoja hiyo kutoka kwa wakulima wa pamba na wamiliki wa vinu vya pamba.

  “Kama mnavyofahamu, Bunge linakutana Dodoma, kwa hiyo kama suala hili halitashughulikiwa mkutano huo, kuna hatari wakulima wakasusia pamba msimu huu na wamiliki wa vinu wakafilisiwa baada ya kufunguliwa kesi za madai dhidi yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Liverpool,” alisema.

  Machali alisema alipata malalamiko kutoka kwa wakulima na wamiliki wa vinu kuwa zao hilo liko hatarini kuangamia na kwamba taarifa za kuaminika zinasema mwaka jana uzalishaji wa zao hilo ulianguka kwa zaidi ya asilimia 30, badala ya kuzalishwa tani 260,000 za mbegu ya pamba zilizalishwa 160,000, huku pamba ikiadimika kwa kiwango kikubwa na wakulima kupata hasara.

  Kwa mujibu wa Machali, taarifa zinaonesha zaidi ya vinu 38 vinadaiwa na wanunuzi wa pamba wa nje na vingi vimeshitakiwa vikidaiwa si chini ya Sh bilioni 10.

  Mbunge huyo alisema Serikali inawajibika kutoa maelezo ya kutosha kuhusu kiini cha kuanguka kwa pamba kwa kile alichoeleza kuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Bodi ya Pamba, hazijawajibika kuwasaidia wakulima na wamiliki wa vinu ambao ni wadau muhimu katika sekta hiyo ya pamba.

  Kwa mujibu wa Machali wanasheria wao wameanza kuchunguza kuhusu suala hilo ili kuona nani awajibishwe vipi kutokana na tatizo hilo linalokabili sekta hiyo muhimu.

  “Nataka nikaihoji Serikali kwa niaba ya wadau hawa wa pamba na kufahamu itawasaidiaje watu hao na kuwasaidia kuwaokoa kulipa deni hilo la mabilioni ya fedha … nafanya yote kwa maslahi ya Taifa ndio maana nataka kwenda kuhoji bungeni,” alisema.

  Machali alisema jambo la msingi ni kuona Serikali inatoa tamko gani kunusuru hali hiyo na kuhakikisha wakulima wa pamba na wamiliki wa vinu hivyo vya pamba wanatendewa haki na kubainisha kuwa baadhi ya wanunuzi wa nje, wamekuwa wakitoa hata vitisho kwa wamiliki wa vinu vilivyoshindwa kutekeleza mikataba waliyofunga nao.

  Katika hatua nyingine, NCCR-Mageuzi imesema inaendelea kusubiri Chadema kuwapa jibu iwapo imekubali ombi lao la kutaka kuunda kambi moja rasmi ya upinzani.

  Hata hivyo, Machali alisema wabunge wa NCCR-Mageuzi wataendelea kufanya kazi zao hata kama watakuwa nje ya kambi rasmi ya upinzani na kuongeza kuwa wanasubiri kujibiwa, kwani si suala la kulumbana ila kukubaliana.

  Machali alisema anaamini nguvu ya wabunge wa vyama vya upinzani kuungana na kuwa na kambi moja rasmi ni muhimu kwani kwa pamoja wanaweza kusimamia hoja na kuitetea kwa maslahi ya wananchi.

  Mbunge huyo pia alikanusha NCCR-Mageuzi kushinikizwa na Chama cha Wananchi (CUF) kutaka kujiunga na CHADEMA ili kuunda kambi moja na kubainisha kuwa wabunge wa chama chake kila mmoja anajitegemea kimawazo ila wanaamini wabunge wa upinzani wakiwa na kambi moja rasmi watakuwa na nguvu ya pamoja bungeni kutetea hoja kwa maslahi ya umma.

  Source: Habari Leo/Jumamosi January 29
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu watu tutachanganyikiwa kabisa, ndo yanayowapata wana wa Farao huko kunako mapiramid
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  give me a break waulize what happened to the "stimulus package"..
   
 4. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Yes huu ni wakati mzui sana kuitumia hija hii kukumbushia stimulus package ambayo JK aligawana na marafiki zake kwa ajili ya kampeni za 2010. Hoja hii ikienda bungeni itasaidia sana. Tukirudi ktk tatizo chanzo ni palepale kwenye uongozi mbovu wa JK kuacha nchi ijiendeshe yenyewe. Sekta ya Pamba ina mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi yetu gt JK ameiacha ijiendeshe yenyewe huku bodi ya Pamba ikipata bajeti kiduchu ambayo haitoshi hata kucover administations. Anasahau kuwa hata wakwere wenzie pale Miono bagamoyo wanalima Pamba na wamekata tamaa. JK alielezwa mwaka jana pale Bariadi kuwa Wasira amewanyima wakulima vocha za pembejeo za pamba wamegawana wakubwa ofisini lakini hakuchukua hatua zozote. Zao la pamba linazidi kudidimia huku wakulima wa Pamba kanda ya ziwa wakizidi kuchoka kiuchumi na wengi wamekimbilia kulima mpunga au dengu ambazo uzalishaji ukiwa mkubwa bei inashuka sana na mkulima hanufaiki kabisa. JK okoa Pamba, Okoa viwanda vya Pamba, waokoe wananchi wa kanda ya ziwa ambao kwa miaka mingi ccm imewatumia kama daraja la kupata kura na sasa wameishtukia ccm.
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kuna mwanaharakati mmoja alituhabarisha kuhusu ufisadi mkubwa uliofanywa na viongozi wetu kupitia hiyo 'stimulus package'. Hakutoa ufafanuzi sana. Alikuwa anachangia kwenye kipindi cha TV kilichokuwa kinarushwa moja kwa moja. Alipotaka kuingia ndani kuhusu suala hilo alizuiliwa na mtangazaji kwamba hiyo haikuwa hoja iliyowekwa mezani kwa siku hiyo. Nakumbuka alisema anayo hata orodha ya majina ya viongozi walioshiriki kwenye ufisadi huo na kiasi cha fedha iliyochukuliwa. Jamani wenye data wazimwage hapa jamvini.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  sasa ndio tunafika pazuri, wtu wananyangwa Ardhi, watu wanamwagiwa tindikali kutoka migodini, huduma za Afya kwa wazee, kina mama na watoto hovyo, EPA, Dowans
  Uzuri ni kuwa hata kama mtu anaitetea Dowans basi atakuwa na sababu nyingine ya kutaka kuikomboa nchi, na siku zote mapinduzi hayaji na sababu moja
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  No no no Big NO!

  JKT Hawezi kuokoa Pamba wala hawezi kujiokoa mwenyewe ndo anakwenda kuzimu yeye na mjambazi wenzie wa CCM.
   
 8. N

  Njaare JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mh! zis cantri bwana kuna vituko. Kwani stimulus package ilikuwa ni kwa ajili ya nini?
   
 9. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Stimulus package ilijaa usanii mkubwa wakalipwa wasio stahili provided uko karibu na system.
  Wasira akiwa kilimo alipora madaraka ya bodi ya pamba ambayo haina mkurugenzi kwa mwaka mmoja sasa. Kajiingiza kwenye biashara ya kuuza madawa toka china yasiyo na ubora.

  Wenye viwanda wengi walifanya forward sale lakini pamba ikawa kidogo.
  Mwezi wa 9/2010 word market prices zilipanda frm $0.75/lb to $1.50/lb ya sasa. Baadhi yao waliuza pamba kwingine ili kkupata faida. Wacha washitakiwe tu.

  Kuhusu wkulima wao walilipwa vizuri ingawa uzalishaji umeshuka cozz wengi wameacha kulima pamba badala yake wanalima tumbaku kwa maeneo ya kahama na bukombe
   
 10. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Jamani hili tulifuatilie kwa karibu then tulipe muda wa kulidadavua kwa urefu na mapana yake
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kweli sasa tupo kwenye Transition period....., Decision na hatua tutakazochukua sasa ndio zitakazodetermine future yetu.......
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
   
Loading...