Wakati Kodi ikiongezeka kwenye huduma za kifedha, ni wakati sasa kufikiria kukata Bima ya Maisha

rasachri

Senior Member
Apr 8, 2011
145
35
Habari wandugu?

Kama tunavyofahamu kua katika Bunge la bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017 imepitishwa kulipisha kodi ya ongezeko la thamani yaani (VAT) kwa kila muamala wa kifedha kwenye huduma za mabenki, tigo pesa, m pesa, airtell money, ezzy pesa pamoja na miamala katika masoko ya hisa.

Kwa faida ya wasiofahamu ni kwamba, bima hua hailipiwi kodi pindi mteja wa bima anapopata malipo yake, hivyo kwa wale wenye malengo ya mda mrefu kama kusomesha watoto, kutaka kufanya uwekezaji kwa siku za mbeleni, na wenye malengo mbali mbali, huu ni wakati sahihi wa kuchagua kukata Bima ya Maisha kwa ajili yako na wale uwapendao.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kampuni bora ya kukata Bima hii ya maisha, na elim kuhusu Bima ya maisha (elim isiyo na malipo) usisite kuwasiliana nami kwa sim namba +255 652 876811 au +255 754 455865 au email: sam_mpema@yahoo.com

Ahsanteni wakuu.
 
Mkuu hiyo elimu si bora ungeimwaga tu hapa hadharani kuliko kila mhitaji mmoja mmoja kukupigia kwa wakati wake? Pia kwa kuiweka hapa itasaidia wadau kuchangia mawazo yao ambayo itakuwa ni kwa faida ya wote watakaopitia uzi huu. Otherwise expect poor response.
 
Kweli kabisa! Aweka elimu hapa tuelimike kisha tumtafute, itapendeza kulko mmojammoja kumtafuta.
 
Nashukuru kwa mawazo yenu ndugu zangu, niliamua kuachagua njia ya kutotoa elim ile moja kwa moja ili kutoleta mgongano kwenye maada kuu.

Kwa kampuni ninayofanyanayo kazi(Jubilee Insurance) tuna products tatu ambazo ni Career Life, Fanaka Plan pamoja na Family Shield.

Career Life ni bidhaa yenye dhumuni la kumuhakikishia mtoto wako au mtegemezi wako elimu bora kwa kipindi ambacho upo hai ama unapokua umefariki, na wakati wa uzima ama ulemavu. Maana yake ni kua, ukikata bidhaa hii leo kwa kulipia malipo yako ya kwanza ya kila mwezi, mtoto wako anakua analindwa kwa thamani ambayo wewe mzazi umeamua kumkatia. Kiasi cha chini kabisa kumkatia mtoto wako ni Tsh 5,000,000, kiasi cha juu hakuna mwisho. Hii milioni 5 hailipwi kwa mara moja, hesabu hupigwa kwa kuangalia umri wa mkataji wa bima, mda ambao unataka bima hii ikulinde, na hicho kiasi ambacho umeamua kikulinde yaani hiyo milioni 5, jibu tutakalopata hapo yaweza kua ni 50,000 au 60,000 kwa mwezi. Hivyo utakapolipia elfu 50 yako au 60 ya kwanza tayari unakua unalindwa kwa thamani ya milioni 5 ambapo kukitokea tatizo kama ulemavu wa kudumu, kuugua ugonjwa utakaodhoofisha ufanyaji wako wa kazi kama kansa au kupooza au kufariki mteja hufutiwa malipo hayo ya kila mwezi na kulipwa milioni 5 ambayo hugawanywa kwenye miezi 36. Pia miaka ambayo mteja amekata bima hii inapomalizika moja kwa moja hulipwa hiyo milioni tano ili akatimize lengo lake la kusomesha mtoto au mtegemezi wake.

Bidhaa nyingine ni Fanaka Plan, ambayo hii ni maalumu kwa ajili ya uwekezaji na malengo. Mkataji wa Bima hii huweza kumkatia mtu yoyote ambae ni ndugu kwenye familia au hata yeye mwenyewe. Mfano, kutokana na changamoto za ajira, mzazi unaweza kuamua kukata bima hii kwa ajili ya kumuwekea mtaji kijana wako pindi anapomaliza masomo yake, pia waweza kujikatia wewe mwenyewe kwa ajili ya biashara hapo baadae kwa kua pindi marejesho ya bidhaa hii yanapofanyika huangalia ongezeko la thamani ya pesa kwa uwekezaji na hivyo hulipa zaidi ya ile thamani unayokatia bima. Mkataji wa bima hii anapofariki, wanufaika wake hulipwa 175% pamoja na 10% ya kuchangia gharama za mazishi, tofauti na hiyo ya bidhaa ya kwanza hii hulipa mara moja wakati ile ya shule hulipa pindi mteja alipofariki na pia hulipa pindi miaka ya bima inapomalizika. Masharti mengine ya kiwango cha kukatia bima na mda, na namna malipo ya kila mwezi yanavyopatiakana hufanana na hayo ya bidhaa ya kwanza.

Aina ya tatu ni Family shield. Hii ni Bima ya maisha maalumu kwa ajili ya misiba. Mkataji huikata kwa kati ya miaka mitano na miaka kumi ambapo anaweza kukata kwa ajili yake na familia yake pamoja na ndugu wengine. Pindi mmoja wa waliokatiwa bima hii anapofariki,mkataji hupata pesa kwa ajili ya kusaidia gharama za mazishi. Malipo yake hufanyika kwa mwaka na sio kila mwezi kama kwenye aina zingine hii ni kwa sababu malipo ya kila mwezi ni madogo mno kiasi cha Tshs 1,500 mpaka 21,000. Kiwango cha juu kabisa kulipia kwa mwaka kwa bidhaa hii ni Tsh 240,000.

Ahsanteni na karibuni sana kwa ajili ya kueleweshana na kuelimishana zaidi.

Raphael Christopher
Sales Advisor-Jubilee Life Insurance
+255 652 876811/ +255 754 455865
sam_mpema@yahoo.com
 
Fanaka ina experience mbaya.. Kuna mtu namfahamu alikata fanaka product ya miaka kumi, ameenda kusurrender, mambo waliyomwambia ... Hawezi kupata hiyo hela yake aliyochangia kwa miezi 9
 
Hebu fafanua zaidi mkuu ili wengine wapate mwanga.
Hizi bima nyingi zimejiweka kwenye corner ambazo ni ngumu kwa mwekezaji kufaidi alichowekeza/wekezewa.
Mfano hiyo ya kusubiri mpaka ufe ndio pesa itoke kuja kukuzika.
 
Kwa mfano hii fanaka... Unaweza kukata kwa miaka kumi.... Lakini kama umepata tatizo, kwa mfano ndani ya miaka mitatu au chini ya hapo, hawawezi kukurudishia ile michango uliyochangia kwa miaka miaka mitatu... Au ukisema labda ulikuwa unachangia sh..300,000 sasa nataka kuchangia chini ya kiwango cha awali... Hapo utakuwa umepoteza michango yako ya awali na wataanza upya kwa huo uchangiaji mpya. Bima ni uwekezaji na hapo hapo ukingaji wa majanga.... Ukiangalia katika mazingira hayo, utagundua bima hapo wanataka kubakia na hela yako no matter what happens ...Sasa huu ni mfumo wa ovyo.... Kwani mteja anaweza kupata na majanga mengine, ambayo yanaweza kupelekea kutoendelea na hiyo bima..>Sasa kwa nini iwe kama umejiunga na chama cha wachawi hakuna kutoka ??
 
Back
Top Bottom