Wakati kizazi kipya kikiwalamba CCM miguu kwenye kampeni, Rose Mhando atesa Kenya..

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Kizazi kipya wamekuwa wakijidhalilisha na kuthibitisha hawana mikakati ya kujitegema kiuchumi na ndiyo maana hujisalimisha kwa wanasiasa hususani wa CCM katika kipindi cha kampeni.

Huko huambulia makombo tu. Angalia mwanadada mmoja iliripotiwa ndani ya jamvi hili kuwa aliachwa kwenye msafara wa JK huko Singida na ikabidi ajikodishie pikipiki imrudishe kule alikofikia. Wanamuziki wa kizazi kipya wamejikuta katika hali mbaya kifedha kiasi kwamba wanasiasa huwatumia na baadaye kuwatelekeza.

Mfano katika mkutano mkuu wa CCM wa mwaka 2007 uliomtawaza JK kuwa Mwenyekiti wa CCM, JK aliwaumbua wanamuziki hao baada ya matumbuizo yao pale aliposema......" Hawa tulikuwa nao na tuliwatumia katika kampeni zetu za 2005.."

Ungelitegemea basi baada ya kauli ya bosi huyo wa CCM, kizazi kipya wangelijifunza na kuachana na tabia hiyo ya kujidhalilisha kwenye kampeni za CCM ambako uchunguzi wangu umebaini malipo wanayolipwa ni kiduchu sana.

Lakini mwanamuziki wa kwaya ya dini au "gospel" mwanamama Rose Mhando amewaonyesha njia kizazi kipya kwani huko Kenya ameingia mkataba mnono na Safaricom
na nyimbo zake sasa zinatumika katika mtandao huo naye hulipwa pesa kibao.

Mfano wimbo wake wa "Nibebe" sasa unamwingizia zaidi ya Tshs 16 Milioni kwa mwezi au Kshs 800, 000/= kwa Exchange rate of one Kshs for 20 Tshs.

Kwa kitega uchumi kama hicho Rose Mhando anapata zaidi ya Tshs 152 Milioni kwa mwaka kwa wimbo mmoja tu. Na anazo nyimbo nyingi kwenye mtandao wa Safaricom na hivi sasa ana matamasha mengi huko Kenya kutangaza nyimbo zake ili watumiaji wa mtandao wa safaricom waweze kuwa wanazitumia kwenye milio ya sauti ya simu zao.

Sidhani hata kampeni ikiendelea kwa miaka kumi ijayo kama kizazi kipya kilichojisalimisha kwa wanasiasa wetu wa CCM kitakaa kiweze kupambana na mapato ya gwiji huyu wa miziki ya kidini.

Ushauri wangu ni kuwa vijana hawa wa kizazi kipya ni vyema wakajiangalia tena na kujipima wako wapi, wanatoka wapi na wanakwenda wapi.


 
Yani mimi wameniboa kabisaa na wengine hata kusikiliza kazi zao siku hizi nimeamua kuacha kabisa, kichefuchefu tupu, na cd zao sinunui tena.
 
Ni kweli wanamshabikia mtu aliyewaahidi kuwapa na kufuatilia hakimiliki zao, lakini akawakataaa na kuwatosa. wanafanya kazi nzuri zinaliwa na Wahindi tu! Wanahitaji kupewa Elimu kubwa sana hawa vijana!
 
Hawa kizazi kipya njaa tu, hawana lolote kabisa. Cheki hata yule binti Nakaaya yaani hata nyimbo zake siku hizi sizitaki kabisa, upuuzi mtupu
Wataendelea kuula wa chuya
 
wamuige na Lady jaydee naye anakula shavu kwa heshima ya ajira yake kila siku anakuwa balozi wa mashirika makubwa! hamna international org inayoweza kumtumia Marlaw na upuuzi wake
 
Back
Top Bottom