Wakati Kikwete anawapigia kampeni Mramba, Rostam, EL, alikuwa amewadharau wapiga kura? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati Kikwete anawapigia kampeni Mramba, Rostam, EL, alikuwa amewadharau wapiga kura?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Apr 14, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kila mtu sasa anashangilia kuwa CCM inajisafisha kwa kuwatema watuhumiwa wote wa ufisadi, miezi michache iliyopita tuliambiwa kuwa CCM ni chama kinachofuata utawala wa sheria kwamba kisingewaacha makada wake waliokuwa na tuhuma za ufisadi kwa kuwa tuhuma hizo zilikuwa hazijathibitishwa na kila mtu alishangilia (akiwemo Chiligati, Makamba, na wengine wengi), leo hii hao hao ambao sisi tulikuwa tunawaona hawafai kupewa fursa ya kuendelea kuwa viongozi kwa sababu ya tuhuma hizo wanaanza kuenguliwa na tunaambiwa kuwa huu ni mkakati wa chama kujisafisha...

  Binafsi siamini kuwa kuna utashi wa kweli kuwawajibisha makada wote wa CCM wanaotuhumiwa na ufisadi bali ni janja ya nyani kuendelea kula mahindi yetu. CCM ndicho kilicho madarakani, kina dola, kina vyombo vya uchunguzi na hakikuonyesha dalili za kulishughulikia tatizo la ufisadi tangia 2006 pale tuhuma nyingi zilipoanza kuzagaa kuwa tunaliwa, uchunguzi wa Kagoda bado unaendelea na haieleweki utaisha lini.. kila mtu aliambiwa kuwa hawa walirejesha sehemu ya hela waliyokuwa wamechukua na wakasamehewa (bila hata kufikishwa mahakamani tukaujua ukweli) na bado serikali bado inafanya uchunguzi sijui ni nini ambacho wanachunguza....

  Natoa wito kwa watanzania wote wapenda haki wasidanganyike na uhuni huu wa CCM bali tukaze kamba kelele tunazopiga sasa zinaanza kuwatia hofu tusipumuzike mpaka pale tutakapo wafikisha mahakamani wale wote wanajulikana kama untouchables, tuwa Housin Mubaraka hawa wahuni
   
 2. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hawa wote wanataka kutuzuga ili kusudi wasishitakiwe kama yanayomtokea Hosim Mubarak.... hawa ni wahalifu na tusiwape fursa ya kukwepa mkono wa sheria
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  wenzetu ccm maji yamewafika shingoni.huu ni mwanzo tu.tutegemee mengi zaidi ya kijihuzulu.kifuatacho ni kusalitiana.
   
 4. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ya leo jamani sio ya miaka ile ya 47. Uwezi leo ulasema kuwa EL, ROSTAM, CHENGE, MRAMBA,MKAPA na wengine wengi kuwa ni mafisadi wakati mlikuwa mnawatetea mwakajana tu na tena mlikuwa mnasema CCM aiwezi kufanya kazi kwa kuisi sasa tunataka ukweli kwa kuwa mlisema kuwa amuisi basi sasa mnaikweli tunaomba tuujue
   
 5. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania amka sasa tunataka wanaotoleo ndani ya ccm kwa tuuma sa ufisadi wafikishwe mahakamani maana wamekula pesa za walipa kodi wa tanzania[
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nadhani pale alikua amesahau kidogo ufisadi wa hawa mpaka baada ya yeye Kikwete kuwarudisha bungeni watu hawa kupitia zile kura za ki-miujiza anazojua yeye peke yake tu!!!
   
 7. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jk siku zote ni bendera hufuata upepo, hufanya maamuzi bila kujua madhara yake baadae. Uswahili unamponza maana hatumii akili hata siku moja kuamua kitu. Chochote kinachoonekana at stake ndicho kinachotumika. He doesn't select a right solution for the right problem.
  Sasa amedanganywa kuwa anaweza ku regain his populaty kwa njia ya kijinga kama hii ya kujivua gamba.
  This is a new generation my friend people will critically verify whatever comes out of your mouh.
  bado wanadhani wanao mtaji wa wajinga huko vijijini lakini tunasema tumechoka na wazazi wetu hawatatumika tena kuliangamiza taifa hili kwa upuuzi huu.
  Chadema please help this country to get to realy freedom. People are tired, they need chnage.
  Watu wanataka nao waishi maisha kama watu wengine duniani.
  Tumechoka watu wachache kuendelea kula nguvu za watu 40milion.
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA, Mungu wabariki viongozi wa chadema, Mungu wabariki wapiganaji wote wa kweli wa nchi hii.
  Pamoja tutashinda!
   
 8. I

  Igembe Nsabo Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuendeleze SHIME na kushikamana katika VITA hii ya UFISADI mpaka kieleweke.
  Hatukubali kudanganywa na hawa WEZI wa mali yetu na wanaotutia au kutusababishia umaskini. Tuwaogope kama UKOMA
   
Loading...