Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,445
- 113,456
Wanabodi,
Kesho ndio tarehe ya mwisho kwa Barrick kuonyesha nia ya dhati ya kuinunua Acacia katika hostile take over kupitia utaratibu unaitwa put up or shut up' (PUSU) deadline kwa Barrick kutoa tangazo la kifo cha Acacia kwa kuinunua kwa fedha kiduchu kwa hoja kuwa Acacia ni kampuni ya hasara tupu na risk company, siku ya leo Acacia, ametoa taarifa ya kuonyesha anapata faida kubwa.
Kuna msemo wa kizungu unasema kwa kawaida farasi kabla hajafa, huwa anarusha teke la mwisho ndipo anakufa, ikitokea teke hilo likakupata, na wewe safari ni hapo hapo!, mnaondoka pamoja!.
Hivyo kwa vile kesho ndio tarehe ya mwisho kwa Barrick kutangaza offer ya mwisho kuinunua Acacia na kuiua rasmi, kabla ya kesho, leo Acacia amerusha teke la mwisho la a dying horse kuonyeshea anapata faida kubwa, ili kama Barrick asipoongeza dau, Acacia waendelee kukomaa tuu na serikali ya Tanzania, ambayo licha ya taarifa za serikali yetu kutoitambua Acacia, lakini serikali inaendelea kuvuta mpunga wa Acacia kwa upande wa kodi na mrahaba.
Hii ndio taarifa ya Acacia
Taarifa kuwa serikali yetu bado inavuta mpunga wa Acacia ni hii hapa
Pia ili Barrick kuhalalisha kuinunua Acacia kwa fedha kiduchu, kuna media za kimataifa zimepelekewa taarifa za uwongo na uzushi kuihusu Acacia ili ziichafue uizwe kama sadaka, Acacia imezikanusha taarifa hizo kuwa ni uwongo na uzushi.
Kanusho la Acacia ni hili
A Way Forward.
Wakati wowote kuanzia sasa, yaani kati ya leo na kesho ambayo ndio deadline, Barrick watatangaza firm final offer ya kuinunua Acacia, na Acacia watatakiwa kujibu kama wanakubali kununuliwa au laa.
Acacia wakikubali kununuliwa, huu ndio unakuwa mwisho wa Acacia, Barrick itaimiliki Acacia kwa asilimia 100%, sisi Tanzania tutalipwa kile kishika uchumba chetu cha dola milioni 300, ambazo sasa ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni hewa la dola bilioni 190 za Noah zetu. Acacia itavunjwa, na kuundwa kampuni mpya ya ubio kati ya Tanzania na Barrick ambapo serikali itakuwa na hisa asilimia 16%, Watanzania wataingia kwenye bodi na menejiment, na tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.
Acacia akikataa offer ya Barrick, kitakachofuata ni mtifuano...
Paskali

Barrick Gold Corporation - Home
www.acaciamining.com