Wakati Kenneth David Kaunda anatimiza miaka 97, tuangalie uhusiano wake na Ally Sykes 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,083
KENNETH DAVID KAUNDA NA ALLY KLEIST 1953

Leo Kenneth Kaunda katimiza miaka 97.

Nimeangalia picha ya Kenneth David Kaunda na picha hii ikanikumbusha uhusiano wa Kaunda na Ally Kleist Sykes wakati Afrika ilipokuwa katika harakati ya kupigania uhuru wake.

Usiku umekuwa mwingi In Shaa Allah kesho nitaeleza vipi Ally Sykes na Kenneth Kaunda walifahamiana miaka ya 1950 wakati Northern Rhodesia sasa Zambia na Tanganyika zilipokuwa zinapigania uhuru wake.

Ally Sykes mzee wangu nimemvulia kofia katika kutunza kumbukumbu.

Faili la safari yake yeye na Dennis Phombeah kwenda Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa Kusini ya Ikweta naamini ndilo faili mwenyewe akilipenda kuliko mafaili yake yote yote yenye taarifa za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ndani ya faili hili kuna ''cuttings'' ya magazeti zikieleza mkasa mzima wa safari yake kutokea Dar es Salaam hadi Salisbury ambako yeye na Phombeah walitiwa mbaroni na makachero wa Kikaburu kama ''Waafrika Wakorofi,'' na kufungiwa ndani ya banda nyuma ya nyumba ya Mzungu usiku kucha.

Asubuhi wakaachiwa na kuamriwa kurudi Tanganyika kama wahamiaji wasiotakiwa.

Hii ni movie ni ''block blaster,'' ambayo itahitaji waigizaji mahiri kucheza nafasi ya Ally Sykes, Denis Phombeah, Kenneth Kaunda, Harry Nkumbula, Charles Mzengele kachero, kibaraka wa Wazungu walowezi wa Southern Rhodesia, kachero kibaraka wa Waingereza Tanganyika, Alexander Thobias, Trevor Huddleston Mwingereza muungwana aliyekuwa rafiki wa Waafrika.

Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa ANC na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini.
Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC.

Hapa ndipo Kaunda akaanza kuwatafuta wanasiasa wenzake waliokuwa Tanganyika, Kenya na Afrika Kusini na kuwaalika kwenye mkutano Lusaka, Northern Rhodesia ambao ungewakutanisha wapigania uhuru kutoka nchi za Afrika chini ya Ikweta.

Hivi ndivyo Kenneth Kaunda na Ally Sykes walivyokuja kufahamiana kwa kuandikiana barua ambazo Ally Sykes alizihifadhi hadi mimi kuja kuzisoma miaka mingi baadae.

Katika kusoma nyaraka kama hizi ndipo nikamwelewa Ally Sykes pale alipokuwa akiniambia, ''Hawa walioandika historia ya TANU hawana moja wanalolijua.''

Mkasa wa safari hii ya Ally Sykes na Denis Phombeah kuhudhuria mkutano wa Lusaka ni kisa kirefu sana lakini chote nimekieleza katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Nimeweka picha ya Charles Mzengele kachero kibaraka wa walowezi ikifuatiwa na picha ya Kenneth Kaunda na Harry Nkumbula kama walivyokuwa katika miaka ya 1950.

Ally Sykes alikuwa akitamka jina hili kama ''Mzengele,'' lakini usahihi wa jina la huyu kachero ni Mzingeli.

20210429_084655.jpg
 
Viva KK, happy birthday to you, a father of African democracy
 
Mzee Mohamed Said... Kuendelea kulalamika kwenye mitandao kwamba historia ya TANU , haijaandikwa vizuri , haisaidii kujua historia hiyo.. Andikeni hiyo historia kila anayetaka kujua ajue.. Nimezunguka kwenye maduka ya vitabu , nikaulizia kama kuna vitabu vyovyote ulivyoandika sikufanikiwa ... Au unauzia hivyo vitabu wapi ???
 
Mawazo mazuri haya!
 
Newazz,
Kitabu kipo sasa miaka 23.
Kinauzwa Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani.

Vilevile Elite Bookshop Mbezi Samaki na Tusome Bookshop Mikocheni.

Ibn Hazm wanauza 10,000.00.

2810471_Screenshot_20210616-231825_Photos.jpg
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom