Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,178
- 876
Source:Majira
...Kada aliyepata ajali na Kapuya afariki-3rd
Na Waandishi wetu, Dar na Tabora
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bw Twaha Ngosso ambaye hivi karibuni alipata ajali akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Prof. Juma Kapuya, amefariki dunia jana baada ya kuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa majeraha aliyopata.
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM mkoa wa Tabora. Bw Daniel Fussi marehemu amefariki dunia saa mbili asubuhi na mwili wake unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda mkoani Tabora kwa mazishi.
Bw. Fusi alisema kuwa mwili huo unatarajiwa kuwasili kwa ndege majira saa tano asubuhi ambapo utasafirishwa hadi kijijini kwake Usindi na kwamba taratibu za mazishi zimekamilika.
Alisema kuwa mazishi hayo yanatarajiwa kufanyika majira ya saa tisa alasiri baada ya kuwasili kijijini kwake na taratibu zote zimekamilika.
" Hivi sasa uongozi wa mkoa tupo katika kikao cha maandalizi ya mazishi na tunatarajiwa kupokea mwili wa marehemu kesho saa tisa alasiri na utasafirishwa kwenda Urambo kwa mazishi," alifafanua.
Wakati huo huo, Waziri Kapuya ambaye alikuwa amepelekwa nchini India kwa matibabu zaidi mara baada ya ajali hiyo, amerejea nchini juzi mchana na hali yake inaendelea vizuri.
"Nimetoka kuzungumza naye hivi sasa, yupo Dar es Salaam na anaendelea vyema. Alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa sababu ajali ilipotokea alibanwa sana na mkanda na anaweza kujimudu kutembea mwenyewe," kilisema chanzo chetu kilicho karibu na Waziri huo.
Inasemekana kwamba laiti uhai wa kada huyu ungepewa uzito unaostahili basi yeye ndiye aliyepaswa kwenda nje kwa matibabu kwani hali yake ilikuwa mbaya zaidi ya ile ya Kapuya.Hatahivyo,kazi ya Mungu haina makosa japo kuna wakati uzembe na ubinafsi wa binadamu unachangia sana "kuharakisha maamuzi ya Mola eg kifo.