Uchaguzi 2020 Wakati kampeni zikianza mwishoni mwa wiki hii, ni dhahiri kuwa mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa na mvuto zaidi ya mgombea wa CCM John Magufuli

Jamaa mmoja alimpamba demu wake...
Akanielezea alivyo na lijitako, shapu, pretty
Nilitamani nimuone...
Siku nilipomuona ni wa kawaida sana..
Ukipenda sifia sana
Uhalisia tutajua baada ya uchaguzi
Wakati kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu zinaanza mwishoni mwa wiki hii, ni dhahiri kuwa mapambano huo utakuwa mkali sana, baina ya mgombea wa Chadema, Tundu Lissu na mgombea wa CCM John Pombe Magufuli.

Kwanza niainishe ni kwanini naona Tundu Lissu atampiku Magufuli kwenye kampeni hizo

1. Utawala huu wa awamu ya tano kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa vya upinzani na wakati huo huo kuruhusu chama cha CCM kuwa ndiyo pekee kilichoruhusiwa kuzunguka nchi nzima, kujitangaza kwa kipindi chote cha miaka mitano mfululizo, ndiko kutakakomuongezea mgombea wa Chadema, Tundu Lissu, kwa kuwa Umma wa watanzania utakuwa na hamu kubwa kusikiliza sera za Chadema, ambazo muda mrefu sana walikuwa hawazipati.

2. Ktendo cha CCM kutegemea vyombo vyote vya dola na vyombo vyote vya habari vya Umma na vya binafsi, kuwa upande wa CCM, kutaongeza mvuto mkubwa kwa wananchi kwenda kuzisikiliza sera za Chadema.

3. Kitendo cha kuonewa kupita kiasi kwa viongozi wa Chadema, ambao wamekuwa katika mazingira magumu mno katika kipindi chote hiki cha utawala huu wa awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wao, John Magufuli, wamekuwa wakihangaika mno kukabiliana na kesi mbalimbali, ambazo ni za kubambika, zitawaongezea Sana umaarufu, mgombea wao wa Urais Tundu Lissu na chama chake cha Chadema.

4. Lakini kitendo kikubwa kabisa ambacho kitamuongezea umarufu mno Tundu Lissu, ni kitendo cha yeye kushambuliwa kwa kupigwa risasi 16 mfululizo, akiwa ndani ya gari yake, hapo Septemba 7, mwaka 2017, mchana kweupe, tena kwenye makazi ya viongozi wakuu wa serikali hii, ambapo ni kitu ambacho siyo cha kawaida, kusikia hivi sasa takribani miaka 3, eti watu hao bado hawajajulikana!

Kwa sababu hizo Kuu, naamini kabisa mgombea wa Chadema atakuwa kama lulu, ambapo kila mwananchi atakuwa na hamu sana ya kumuona na kusikia sera zake, huku tukitarajia, CCM kama kawaida yao kutumia vyombo vya usafiri yakiwemo malori, kuwasomba wananchi sehemu mbalimbali ya nchi ili kuja kwa "kulazimishwa" kuja kumsikia mgombea wa Urais wa CCM, wakati wale watakaokwenda kumsikiliza Lissu watajitolea hata kwa kutembea kwa miguu kwa masafa marefu!
 
Naunga mkono hoja ya mvuto na watu kuja kushangaa, kwasababu kiukweli kwa maswahibu Lissu aliyopitia, kupona kwake ni muujiza.

Ila ingekuwa issue ya kushinda urais ni mvuto tuu wa makundi makubwa ya watu, basi saa hizi Edward Lowassa ndio angekuwa ndani ya Ikulu yetu.

Kitu kimoja ambacho nakikubali, hakuna ubaya kujipa matumaini ya upinzani kushinda, kuwa na matumaini ni jambo moja, na the plain reality on the ground ni jambo jingine!.

P.
Rejea
Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM Inaweza Kushinda!

Elections 2015 - Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Kama kipimo cha ushindi ni idadi ya watu, Lowassa ndiye rais wetu
Watashinda tu kama wakifanikiwa kuiweke NEC injuction ya kuendelea kusimamia mchakot mzima wa uchaguzi maana tayari nec wameonesha hawana uwezo wa kusimamia kwa kutoa majibu randaranda kwa haya mapingamizi yanayo endela.. ni mahakama pekee inayoweza kuwapiga stop au kuwapa maelekezo yatako redness na kua-address all short falls ikiwewo upendelo wa watu fulani au wa vyama fulani au hiziu sababu za kijinga kwamba mtu hakuweka full stop kwenye form.. haki ya mtu (fundamental rights ) huwa haipotezwi kwa makosa ya kiuandishi...ni kusahihisha tui hzi dosari na wagombea wote kuendela na uchaguzi...
 
wakati wale watakaokwenda kumsikiliza Lissu watajitolea hata kwa kutembea kwa miguu kwa masafa marefu!
Mm nasafiri toka Katavi muda huu ili jmosi nihudhurie mkutano wa uzinduzi hapo Dar.
Go Tundu Lisu go!
 
Wakati kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu zinaanza mwishoni mwa wiki hii, ni dhahiri kuwa mapambano huo utakuwa mkali sana, baina ya mgombea wa Chadema, Tundu Lissu na mgombea wa CCM John Pombe Magufuli.

Kwanza niainishe ni kwanini naona Tundu Lissu atampiku Magufuli kwenye kampeni hizo

1. Utawala huu wa awamu ya tano kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa vya upinzani na wakati huo huo kuruhusu chama cha CCM kuwa ndiyo pekee kilichoruhusiwa kuzunguka nchi nzima, kujitangaza kwa kipindi chote cha miaka mitano mfululizo, ndiko kutakakomuongezea mgombea wa Chadema, Tundu Lissu, kwa kuwa Umma wa watanzania utakuwa na hamu kubwa kusikiliza sera za Chadema, ambazo muda mrefu sana walikuwa hawazipati.

2. Ktendo cha CCM kutegemea vyombo vyote vya dola na vyombo vyote vya habari vya Umma na vya binafsi, kuwa upande wa CCM, kutaongeza mvuto mkubwa kwa wananchi kwenda kuzisikiliza sera za Chadema.

3. Kitendo cha kuonewa kupita kiasi kwa viongozi wa Chadema, ambao wamekuwa katika mazingira magumu mno katika kipindi chote hiki cha utawala huu wa awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wao, John Magufuli, wamekuwa wakihangaika mno kukabiliana na kesi mbalimbali, ambazo ni za kubambika, zitawaongezea Sana umaarufu, mgombea wao wa Urais Tundu Lissu na chama chake cha Chadema.

4. Lakini kitendo kikubwa kabisa ambacho kitamuongezea umarufu mno Tundu Lissu, ni kitendo cha yeye kushambuliwa kwa kupigwa risasi 16 mfululizo, akiwa ndani ya gari yake, hapo Septemba 7, mwaka 2017, mchana kweupe, tena kwenye makazi ya viongozi wakuu wa serikali hii, ambapo ni kitu ambacho siyo cha kawaida, kusikia hivi sasa takribani miaka 3, eti watu hao bado hawajajulikana!

Kwa sababu hizo Kuu, naamini kabisa mgombea wa Chadema atakuwa kama lulu, ambapo kila mwananchi atakuwa na hamu sana ya kumuona na kusikia sera zake, huku tukitarajia, CCM kama kawaida yao kutumia vyombo vya usafiri yakiwemo malori, kuwasomba wananchi sehemu mbalimbali ya nchi ili kuja kwa "kulazimishwa" kuja kumsikia mgombea wa Urais wa CCM, wakati wale watakaokwenda kumsikiliza Lissu watajitolea hata kwa kutembea kwa miguu kwa masafa marefu!
Nan kasema
 
Hii ndio picha halisi ya fikra zako, ila haiko hivyo kwa kila mtu.
 
Nakubaliana na hoja kadhaa

1. Kukosa muda wa Upinzani kukutana na wananchi.
Hii ccm walibugi, wangewaachia saa wangekuwa very dilute lkn sasa ndio muda wao kusema sera zao mbele za wananchi hivyo watajaa kusikiliza.

2. Kupigwa risasi na kupona.
Muujiza unaotembea watakuja kuuangalia na kama hulka ya binadamu ku sympathize naye watajaa kusikiliza.

Mwisho sera.
Hizi hazitambeba Lisu kabisaaa
Kama COVID 19 hili JMP his the best sio tu Tz Worldwide na wajonge wengine wanajua, kwahiyo Lisu atatazamwa na kupishana na walalahoi wengi eg Chinga

Ulinzi wa Maliasili.
Ikumbukwe Lisu aliwahi kutuaminisha kuwa Accia na Barrick hawawezi kuachia migodi.
Hata kama JPM hajafanya 100% lkn amewaonyesha HATISHWI.

Mwisho kwa sasa sijui kama kura zitapigwa kwa kuhurumiwa mtu aidha kwa kuonewa kwa risasi au sera.

Tuijenge Tanzania Yetu tuwe Wamoja Tusigawanyike. Upinzani uwe wa Upendo na kukutumia kwa Furaha kama Utani wa Jadi
 
Pangekua na tume huru unafikiri CCM wengekua hivi???
Hata Katibu wa uenezi wa CCM, Polepole alitangaza hadharani nanukuu "Kama nchi hii ikiwepo Tume huru, CCM ijiandae kukabidhi Ikulu" Mwisho wa kunukuu
 
Hata Polepole alitangaza hadharani nanukuu "Kama nchi hii ikiwepo Tume huru, CCM ijiandae kukabidhi Ikulu" Mwisho wa kunukuu
Polepole na Bashiru facial expressions zao Sasa hivi Zina aibu aibu kwakua wanajua wanachokifanya sema njaa tuu na usalama wao
 
Watu wanapenda kusikiliza hotuba za Lissu kwakua zona mvuto, Lissu ana charisma, maneno yake yana fundisha, yana tia moyo, na yanaleta matumaini.
Naunga mkono hoja, Lissu ni kweli ni charismatic kuliko, na hili nililisema wazi hapa
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!
Ila kura sio charisma!, kura is something else!.
Ingekuwa kura ni charisma tuu au makundi makubwa ya watu, saa hizi rais wetu angekuwa Lowassa!.
P
 
Mbona Ccm mnajikita kwenye wizi? Mbona hamhamini tena katika sera na ushawishi? Nani aliishi kqakutegemea wizi milele? Hujawahi kuona mwizi anaamua kuacha kuiba anashika jembe na kulima?

Mimi naamini wizi una mwisho ata wahenga walisema '' Za mwizi ni arobaini ''.
 
Kampeni zikianza ndani ya wiki moja tu,
Mje muandike tena hivi hivi atutaki wapiga ramli chonganishi
Umekaa kishabiki, jipe sekunde ishirini kwa imani yako na Mungu wako, halafu jiulize je CCM wanatenda haki kuanzia katika kuengua wagombea wa upinzani?Na je kama imani yako inafundisha kutenda haki na umesimamia hilo?
Vinginevyo unanuka dhambi, na dhambi hunuka kuliko mavi thats why inamkwaza hata Mungu.
Tunataka haki itendeke ashinde Rungwe, Magufuli,Tundu just kwa haki tu.
 
Back
Top Bottom