Uchaguzi 2020 Wakati kampeni zikianza mwishoni mwa wiki hii, ni dhahiri kuwa mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa na mvuto zaidi ya mgombea wa CCM John Magufuli

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Wakati kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu zinaanza mwishoni mwa wiki hii, ni dhahiri kuwa mapambano huo utakuwa mkali sana, baina ya mgombea wa Chadema, Tundu Lissu na mgombea wa CCM John Pombe Magufuli.

Kwanza niainishe ni kwanini naona Tundu Lissu atampiku Magufuli kwenye kampeni hizo

1. Utawala huu wa awamu ya tano kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa vya upinzani na wakati huo huo kuruhusu chama cha CCM kuwa ndiyo pekee kilichoruhusiwa kuzunguka nchi nzima, kujitangaza kwa kipindi chote cha miaka mitano mfululizo, ndiko kutakakomuongezea mgombea wa Chadema, Tundu Lissu, kwa kuwa Umma wa watanzania utakuwa na hamu kubwa kusikiliza sera za Chadema, ambazo muda mrefu sana walikuwa hawazipati.

2. Ktendo cha CCM kutegemea vyombo vyote vya dola na vyombo vyote vya habari vya Umma na vya binafsi, kuwa upande wa CCM, kutaongeza mvuto mkubwa kwa wananchi kwenda kuzisikiliza sera za Chadema.

3. Kitendo cha kuonewa kupita kiasi kwa viongozi wa Chadema, ambao wamekuwa katika mazingira magumu mno katika kipindi chote hiki cha utawala huu wa awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wao, John Magufuli, wamekuwa wakihangaika mno kukabiliana na kesi mbalimbali, ambazo ni za kubambika, zitawaongezea Sana umaarufu, mgombea wao wa Urais Tundu Lissu na chama chake cha Chadema.

4. Lakini kitendo kikubwa kabisa ambacho kitamuongezea umarufu mno Tundu Lissu, ni kitendo cha yeye kushambuliwa kwa kupigwa risasi 16 mfululizo, akiwa ndani ya gari yake, hapo Septemba 7, mwaka 2017, mchana kweupe, tena kwenye makazi ya viongozi wakuu wa serikali hii, ambapo ni kitu ambacho siyo cha kawaida, kusikia hivi sasa takribani miaka 3, eti watu hao bado hawajajulikana!

Kwa sababu hizo Kuu, naamini kabisa mgombea wa Chadema atakuwa kama lulu, ambapo kila mwananchi atakuwa na hamu sana ya kumuona na kusikia sera zake, huku tukitarajia, CCM kama kawaida yao kutumia vyombo vya usafiri yakiwemo malori, kuwasomba wananchi sehemu mbalimbali ya nchi ili kuja kwa "kulazimishwa" kuja kumsikia mgombea wa Urais wa CCM, wakati wale watakaokwenda kumsikiliza Lissu watajitolea hata kwa kutembea kwa miguu kwa masafa marefu!
 
Naunga mkono hoja ya mvuto na watu kuja kushangaa, kwasababu kiukweli kwa maswahibu Lissu aliyopitia, kupona kwake ni muujiza.

Ila ingekuwa issue ya kushinda urais ni mvuto tuu wa makundi makubwa ya watu, basi saa hizi Edward Lowassa ndio angekuwa ndani ya Ikulu yetu.

Kitu kimoja ambacho nakikubali, hakuna ubaya kujipa matumaini ya upinzani kushinda, kuwa na matumaini ni jambo moja, na the plain reality on the ground ni jambo jingine!.

P.
Rejea
Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM Inaweza Kushinda!

Elections 2015 - Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Kama kipimo cha ushindi ni idadi ya watu, Lowassa ndiye rais wetu
 
Naunga mkono hoja ya mvuto na watu kuja kushangaa, kwasababu kiukweli kwa maswahibu Lissu aliyopitia, kupona kwake ni muujiza.

Ila ingekuwa issue ya kushinda urais ni mvuto tuu wa makundi makubwa ya watu, basi saa hizi Edward Lowassa ndio angekuwa ndani ya Ikulu yetu.

Kitu kimoja ambacho nakikubali, hakuna ubaya kujipa matumaini ya upinzani kushinda, kuwa na matumaini ni jambo moja, na the plain reality on the ground ni jambo jingine!.

P.
Kama ww ulivyojipa matumaini kura za maoni ukaondoka na kura mbili
 
Naunga mkono hoja ya mvuto na watu kuja kushangaa, kwasababu kiukweli kwa maswahibu Lissu aliyopitia, kupona kwake ni muujiza.

Ila ingekuwa issue ya kushinda urais ni mvuto tuu wa makundi makubwa ya watu, basi saa hizi Edward Lowassa ndio angekuwa ndani ya Ikulu yetu.

Kitu kimoja ambacho nakikubali, hakuna ubaya kujipa matumaini ya upinzani kushinda, kuwa na matumaini ni jambo moja, na the plain reality on the ground ni jambo jingine!.

P.
Pascal Mayalla
Ngoja nikuulize swali jepesi tu hivi unadhani "popularity" ya mtu haiwezi kuwa kigezo mojawapo cha kumpa mgombea ushindi?
 
Ni kweli, tume ya uchaguzi ingekuwa ni chombo huru, kwa mvuto na umaarufu huo wa Tundu Lissu, uwezekano wa kushinda ungekuwa mkubwa sana.
 
Naunga mkono hoja ya mvuto na watu kuja kushangaa, kwasababu kiukweli kwa maswahibu Lissu aliyopitia, kupona kwake ni muujiza.

Ila ingekuwa issue ya kushinda urais ni mvuto tuu wa makundi makubwa ya watu, basi saa hizi Edward Lowassa ndio angekuwa ndani ya Ikulu yetu.

Kitu kimoja ambacho nakikubali, hakuna ubaya kujipa matumaini ya upinzani kushinda, kuwa na matumaini ni jambo moja, na the plain reality on the ground ni jambo jingine!.

P.
Rejea
Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM Inaweza Kushinda!

Elections 2015 - Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?
Kwa umaarufu huu wa Lissu, tungekuwa na tume huru ya uchaguzi,miezi miwili ijayo watumishi wa umma wangekuwa wanasheherekea kwa kuwa mkandamizaji wa haki zao angekuwa ameondoka madarakani,lakini kwa hali iliyopo sasa,upo sahihi kabisa kwamba ushindi kwa upinzani ni kujipa matumaini tu.
 
Kama ww ulivyojioa matumaini kura za main ukaondoka na kura mbili
Its very true, kiukweli kabla sijatupa karata yangu, nilijipima na Kumwaga sera zangu kwanini nataka kwenda Bungeni na kule nakwenda kufanya nini!

Je, wajua kuna watu wazuri, waadilifu wenye uwezo, wanaotaka kuingia Bungeni kulisaidia Taifa, Bunge na kumsaidia JPM kwa dhati, lakini kwa vile...

Lakini masikini wajumbe, kumbe wana jambo lao!
Na mara tuu baada ya kushindwa nilijitokeza kuyakubali matokeo
Uchaguzi 2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Maadam aliyeshinda na kuteuliwa ni mtu mwenye uwezo, na mtaji mkubwa wa ushindi, namuunga mkono, jimbo la Kawe tumelikomboa.
P
 
Wakati kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu zinaanza mwishoni mwa wiki hii, ni dhahiri kuwa mapambano huo utakuwa mkali sana, baina ya mgombea wa Chadema, Tundu Lissu na mgombea wa CCM John Pombe Magufuli.

Kwanza niainishe ni kwanini naona Tundu Lissu atampiku Magufuli kwenye kampeni hizo

1. Utawala huu wa awamu ya tano kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa vya upinzani na wakati huo huo kuruhusu chama cha CCM kuwa ndiyo pekee kilichoruhusiwa kuzunguka nchi nzima, kujitangaza kwa kipindi chote cha miaka mitano mfululizo, ndiko kutakakomuongezea mgombea wa Chadema, Tundu Lissu, kwa kuwa Umma wa watanzania utakuwa na hamu kubwa kusikiliza sera za Chadema, ambazo muda mrefu sana walikuwa hawazipati.

2. Ktendo cha CCM kutegemea vyombo vyote vya dola na vyombo vyote vya habari vya Umma na vya binafsi, kuwa upande wa CCM, kutaongeza mvuto mkubwa kwa wananchi kwenda kuzisikiliza sera za Chadema.

3. Kitendo cha kuonewa kupita kiasi kwa viongozi wa Chadema, ambao wamekuwa katika mazingira magumu mno katika kipindi chote hiki cha utawala huu wa awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wao, John Magufuli, wamekuwa wakihangaika mno kukabiliana na kesi mbalimbali, ambazo ni za kubambika, zitawaongezea Sana umaarufu, mgombea wao wa Urais Tundu Lissu na chama chake cha Chadema.

4. Lakini kitendo kikubwa ambacho kitamuongezea umarufu mno Tundu Lissu, ni kitendo cha yeye kushambuliwa kwa kupigwa risasi 16 mfululizo, akiwa ndani ya gari yake, hapo Septemba 7, mwaka 2017, mchana kweupe, tena kwenye makazi ya viongozi wakuu wa serikali hii, ambapo ni kitu ambacho siyo cha kawaida, kusikia hivi sasa takribani miaka 3, eti watu hao bado hawajajulikana!

Kwa sababu hizo Kuu, naamini kabisa mgombea wa Chadema atakuwa kama lulu, ambapo kila mwananchi atakuwa na hamu sana ya kumuona na kusikia sera zake, huku tukitarajia, CCM kama kawaida yao kutumia vyombo vya usafiri yakiwemo malori, kuwasomba wananchi sehemu mbalimbali ya nchi ili kuja kwa "kulazimishwa" kuja kumsikia mgombea wa Urais wa CCM, wakati wale watakaokwenda kumsikiliza Lissu watajitolea hata kwa kutembea kwa miguu, kwa masafa marefu!
time talks
 
Pascal Mayalla
Ngoja nikuulize swali jepesi tu hivi unadhani "popularity" ya mtu haiwezi kuwa kigezo mojawapo cha kumpa mgombea ushindi?
Mkuu Mystery, kiukweli popularity matters sana kwenye kukusanya tuu makundi ya watu, mfano Diamond akitangaza kupiga show ya bure pale Taifa, atajaza uwanja toka asubuhi mapema, tatizo hayo makundi ya watu sio ya wapiga kura.

Kwenye issue serious kama uchaguzi, ukishindanisha umaarufu na umashuhuri, umashuhuri ndio unashinda!.

Ni kweli kwa sasa Tundu Lissu ndie mgombea maarufu kuliko wote, na umaarufu wake haukuanza leo, hata mimi mwenyewe ni miongoni mwa tuliomchagiza Lissu kugombea
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Katika chagizo hilo, tulimchagiza Lissu sio ili amshinde Magufuli bali kuongeza tuu joto la uchaguzi kwa amsha amsha, lakini kwa upande wa Magufuli kiukweli kabisa ukweli ni huu, mkubali, mkatae
Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au ni Magufuli tu?!.
P
 
Sawa wengi watapenda kumuona na kusikia yaliyompata kila sehem atakapopitia kwa mara ya kwanza....pindi ikitokea akarudia sehem hiyo mara mbili ndo itakua kipimo sahihi kulinganisha matokeo
 
Back
Top Bottom