Wakati Kabudi na Hayati Magufuli wanadanganya Taifa kuhusu Acacia, Rais Samia alikuwa 2 i/c

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,793
71,206
Nchi yetu ina tabia ya kuhabarisha mambo makubwa nusunusu kama vile sisi tunaohabarishwa hatuna akili ya kuhoji na kudadisi.

Profesa Kabudi wakati anakiri kuwa alidanganya (kwa makubaliano na Magufuli) watu wamemshushia lawama nyingi yeye na bosi wake kuwa walileta taharuki kwa watu na wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na kimaadiĺi.

Jambo linalo shangaza ni ukimya wa watu wote juu ya kuhusika au kulijua hili aliyekuwa Makamu wa Rais wa wakati huo ambaye sasa ndiye Rais.

Jee hakulijua hili wakati alikuwa makamu? Ana kwepaje lawama hizi za udanganyifu na kuleta taharuki?

Kwa vile yeye alikuwa 2 i/c wa Magufuli na sasa ni Rais kamili ni wajibu wake kutoka hadharani na kuliweka vizuri jambo hili na kuliombea msamaha kuwa halita rudia ili kujenga imani ya watu kuwa hatuta pigwa fix tena.

20221004_070638.jpg

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mbowe na Lissu kuanzia mwaka 2008 hadi 2014 walituhadaa watanzania kuhusu Lowassa.

Na mwaka 2015 tulitambua hadaa zao, ila mpaka leo wamegoma kutuomba radhi wadanganyika.

Kwanza wangekuwa waungwana (kama mzee Mwinyi) wangejiuzulu hata katika nyadhifa zao, lkn kwa vile wanawaongoza watu wasiojitambua, ndio maana mpaka leo wameng'ang'ania katika nafasi zao ili waendelee kujaza matumbo yao.

Mleta mada ulitakiwa ubalance kote kote sio uchague wa kuwalaumu na wengine kuwaficha utafikiri ni miungu watu.

Uongo, fitna, majungu na uzushi ni hulka ya watanzania wengi hasa wanasiasa. Kwahiyo mleta mada ili uonekane uko vizuri katika kusimamia ukweli ilitakiwa uwaseme wote viongozi wa upinzani, viongozi wa ccm na wa serikali wanaohadaa watanzania ili wasirudi tena kutuhadaa kupitia vyama vyao au Serikali yao.
 
Attachments

  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    24.9 KB · Views: 6
  • download.jpeg
    download.jpeg
    8.7 KB · Views: 4
  • images (30).jpeg
    images (30).jpeg
    24.2 KB · Views: 5
Yaani uwongo wa Kabudi na Magufuli lawama umpe Samia?...chuki zingine hazina hata aibu
Kwa hiyo kama makamu wa Rais alikuwa hajui kitu?
Na jee kama style hiyo ya uongo, ambao ulileta taharuki alikubaliana nayo hawezi kuruhusu uongo mwingine kama huo kutokea?
Kuchukia uongo ni aibu?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mbowe na Lisu kuanzia mwaka 2008 hadi 2014 walituhadaa watanzania kuhusu Lowasa.

Na mwaka 2015 tulitambua hadaa zao, ila mpaka leo wamegoma kutuomba radhi wadanganyika.
Mleta mada ulitakiwa ubalance kote kote sio uchague wa kuwalaumu na wengine kuwaficha utafikiri ni miungu watu.
Uongo, fitna, majungu na uzushi ni hulka ya watanzania wengi hasa wanasiasa. Kwahiyo mleta mada ili uonekane uko vizuri katika kusimamia ukweli ilitakiwa uwaseme wote viongozi wa upinzani, viongozi wa ccm na wa serikali wanaohadaa watanzania ili wasirudi tena kutuhadaa kupitia vyama vyao au serikali yao.
Utadhani uliyoandika ni sawa na mwendawazimu! Kichwa I hamnaga kitu zaidi ya ULumumba uchwara!!
 
Jiwe alikuwa ni shetani halisi na Kabudi alikuwa malaika wake mkuu
Malaika Kabudi?Mzee kaungama jamani.Uovu huwa una tabia ya kuitesa nafsi.Kiswahili cha kitaa tunasema,Roho ya Kabudi inatukutia kwa maumivu.Pole Lissu kwa yaliyokukuta.Mungu ana mipango yake.😂😂😂😂
 
Nchi yetu ina tabia ya kuhabarisha mambo makubwa nusunusu kama vile sisi tunaohabarishwa hatuna akili ya kuhoji na kudadisi.
Profesa Kabudi wakati anakiri kuwa alidanganya (kwa makubaliano na Magufuli) watu wamemshushia lawama nyingi yeye na bosi wake kuwa walileta taharuki kwa watu na wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na kimaadiĺi.
Jambo linalo shangaza ni ukimya wa watu wote juu ya kuhusika au kulijua hili aliyekuwa Makamu wa Rais wa wakati huo ambaye sasa ndiye Rais.
Jee hakulijua hili wakati alikuwa makamu? Ana kwepaje lawama hizi za udanganyifu na kuleta taharuki?
Kwa vile yeye alikuwa 2 i/c wa Magufuli na sasa ni Rais kamili ni wajibu wake kutoka hadharani na kuliweka vizuri jambo hili na kuliombea msamaha kuwa halita rudia ili kujenga imani ya watu kuwa hatuta pigwa fix tena.
View attachment 2377356

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Jamaa wanajua wanaongoza watu wajinga hakuna namna
 
Back
Top Bottom