Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,901
- 95,401
Juzi nimetoka kidogo kwenda kupata mahitaji ya hapa na pale baada ya kujiweka Karantini kwa muda ila niliyokutana nayo yamenishangaza sana.Asilimia zaidi ya tisini ya Watanzania wanavaa barakoa za vitambaa vya vitenge na wengine wamejifunga leso kama barakoa halafu shaka hawana. Nikawa najiuliza kwa mfano huu ugonjwa ungekuwa umetupiga kama vile ulivyopiga China, Italy, USA, Spain kuna mtu angepona?
Kikubwa nikawa nafikiri labda watu hawana elimu juu ya uvaaji wa barakoa na ni aina zipi za barakoa zinaweza kuzuia Coronavirus. Sasa kilichonisikitisha zaidi na kunichekesha ni kwamba kuna eneo fulani nilienda kupata mahitaji yangu, sasa hilo eneo lina kijiwe cha wanywa kahawa na wapiga story. Hicho kijiwe kina watu zaidi ya kumi na tano kwa hesabu ya haraka na wote walikuwa wamevaa barakoa za vitenge na wengine wamejifunga leso.
Sasa kwenye hicho kijiwe walikuwa wanasikiliza idhaa ya kiswahili ya BBC na alisikika makamu wa waziri wa afya wa Tanzania akisisitiza kuwa barakoa za vitambaa zinazoshonwa mitaani huko hazina uwezo wa kuzuia maambukizi ya Covid-19 na wale jamaa kwa sababu kwa muda huo walikuwa wanasikiliza BBC kwa umakini ili wapate habari za Corona kwa kina basi waliisikia taarifa hiyo ila hakuna alietilia maanani kwa kuiongelea.Sasa jana nikatoka pia nikapita eneo lilelile nikawakuta bado wametulia na barakoa zao za vitenge licha ya habari walioisikia jana yake.
Nilichojifunza ni kuwa mwafrika ni nusu chizi na usipokuwa nae makini anakuumbua fasta sana.Siyo binadamu ambae anaweza kuwa serious kwenye mambo ya msingi.Mambo yanayoshangaza kipindi hiki ni mengi, juzi nimeshangaa kidogo baada ya Mh. Rais kusisitiza kuwa ni vyema watu wanaopona Corona kutangazwa ili kuondoa hofu na ghafla takwimu zilizofuata za Covid-19 idadi ya waliopona corona ikapaa, nikajua ni mtu mweusi tayari! Kwa upande wangu mimi naona inatakiwa watu wapatwe na hofu zaidi ili waweze kuwa serious zaidi tofauti na wanavyokosa hofu na kujikuta wanajiachia.