OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,072
- 114,557
Wizara ya viwanda, biashara na Uwekezaji imetengewa kiasi cha Sh bilioni 81.8 kama Bajeti ya kujiendesha kwa mwaka wa Fedha 2016/17. Fedha kwa ajili ya maendeleo zikiwa ni Sh bilioni 39.1 na fedha za matumizi ya kawaida zikiwa ni Sh bilioni 42.7.
Katika kampeni zake za kuwania Urais, Mhe.Magufuli alisema "Tanzania ya Magufuli itakua ya viwanda"
Kenya ina viwanda vingi zaidi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki lakini imetenga karibu Trilioni 1 kwa ajili ya viwanda. Bajeti hii ni karibu mara 12 ya bajeti ya viwanda ya Tanzania na karibu mara 26 ya bajeti ya maendeleo kwny wizara ya Viwanda Tanzania.
Maana yake ni kwamba kwa mwaka ujao wa fedha 2016/17 Kenya itapiga hatua mara 26 zaidi katika sekta ya viwanda kuliko Tanzania.
Kwa lugha rahisi ni kwamba kama Bilioni 39 itatosha kujenga angalau kiwanda kimoja basi kwa mwaka mzima Tanzania tutajenga kiwanda kimoja tu, na Kenya watajenga viwanda 26 vya aina hiyo (under ceteris peribus).