Wakati gani huwa unadhani nguo imekuwa chafu?

Author

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
1,709
8,007
Watu tunatofautina sana kwenye mawazo ya kuwa nguo imekuwa chafu na hatuwezi kuirudia....baadhi ya watu hutumia njia zifuatazo kujiridhisha kuwa nguo ni chafu na haifai kuvaliwa tena mpaka ifuliwe;

1.Baada ya kuivaa mara moja; hii mara nyingi ni kwa nguo za ndani (hasa wadada)

2.Kuinusa; kama haina harufu ya jasho inaweza kuvaliwa (hii wakaka tunaitumia sana)

3.Kuangalia kama ina rangi ya uchafu; kama bado inaridhisha....inavaliwa.

4.Kupoa; umepambana Buguruni huko joto kali nguo imkuwa yamotoooo, ukirudi unaiweka ipoe...kesho yake au baada ya siku mbili inavaliwa. Hapa ya jumatatu unaivaa tena jumatano, ya jumatano unaivaa ijumaa n.k.

5.Mazoea; wengine wakivaa nguo mara moja wanakuwa na mawazo kuwa imeshachafuka hivyo hawawezi irudia.

Mdau wewe huwa unatumia vigezo gani kudhani kuwa nguo imechafuka na hauwezi kurudia kuivaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakat wa masika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye ‘kunusa’ ndo penyewe hasa boksa ambayo ni siri yangu, kama haina uvundo itapigwa tena (kwa mikoa isiyo na joto kali).... mashati nitabadili kwa ajili tu ya kubadili mwonekano nisitoke kama jana ila suruali ‘haichafuki’ inaweza kutupiwa hata wiki.
 
Inategemea na mahali nilipo, kwenye joto t-shirt nabadili kila siku, kwenye baridi huwa nna tabia kila nnapotoka naangalia nguo iliyo karibu kama nimeenda umbali mfupi na sijakutana na shuruba zozote hiyo ijiandae kwa matumizi mengine vinginevyo siivai tena, boxer hata iweje lazima ibadilishwe.
 
,, Suruali huwa haichafuki
Hapo kwenye ‘kunusa’ ndo penyewe hasa boksa ambayo ni siri yangu, kama haina uvundo itapigwa tena (kwa mikoa isiyo na joto kali).... mashati nitabadili kwa ajili tu ya kubadili mwonekano nisitoke kama jana ila suruali ‘haichafuki’ inaweza kutupiwa hata wiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shati , t-shirt, singland, boxer,,,! Kila siku zinabadilishwa !

Jeans naweza vaaa ht siku 2, then naiweka nakuja navaa Tena swaaafi !

Suruari za kawaida (kadeti) siku mbili mpk tatu inategemea na mazingira !
 
Back
Top Bottom