Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 233
Katika kutafuta uhuru wa maisha yangu , kazi , mapenzi yangu na amani ya akili yangu
Niliacha kumbukumbu yako nyuma , moyoni kwangu ulikuwa umejaa sana kuliko pishi la wali , hukuwahi kuteleza wala kuterereka .
Nataka kuanza maisha mapya ya mapenzi lakini siwezi , kwasababu bado ulikuwa akilini mwangu moyoni mwangu nakatika shuguli zangu za kawaida , sikuwa na njia nyingine yoyote ile
Kwasababu najua ukweli kamba ntakufikiria wewe saa zote , muda wote na popote pale nilipo likija suala la kukupenda wewe milele na milele , kukusikiliza na kuwasiliana na wewe , kama muda na wakati napata .
Najaribu kutupa picha yako kutoka akilini mwangu , labda ntakusahau , au pengine upotee kabisa toka sehemu zote ntakazo kua Najaribu kuacha kukufikiria ,kama nilivyokuwa nakufikiria na kukujali enzi hizo lakini hata siwezi hata robo haifikii .
Kila nikipita njiani wale ndege wa mitini wanaimba nyimbo za jina lako , naona aibu hata kuangalia ardhi kwa siku ile ya mwisho tulivyofanyiana mambo ya ajabu ajabu , hata mawingu nahisi yanataka kunidondokea , magari nahisi kama yanataka kunigonga , watu pia nawaogopa labda wanaweza kunisulubu
Nikipita baharini , sauti za mawimbi zanabeba sauti kutoka kwako , Inanikumbusha enzi hizo nikienda kuogelea , sikuwa naona maji ya blue bali niliona sura yako majini , hiyo ilinifanya niogelee kwa ufanisi na furaha , haya maji ndio yanaunganisha sehemu ulipo nami .
Siku hizi naogopa hata kuangalia maji ya baharini kwasababu sioni kitu chochote kile sioni rangi naona mawimbi tu na sauti za ajabu ajabu , hawa ndege nao wanaimba nyimbo mbaya mbaya tu hazina radha .
Sijui unanifikiria kiasi gani hapo ulipo , au sijui unanifikiria kwa mabaya sio mazuri ? nahisi ni mazuri , kwasababu mambo yale yalishapita nami nimeshasahau kitambo , kama unanifikiria kama ninavyohisi na kufikiria je Unajua ukweli kwamba nakufikiria wewe pia ?
Ukirudi kwangu katika maisha yetu ya kawaida Siku moja sijui ni siku gani hiyo kwa sasa siwezi kufikiria zaidi mahala Fulani , wala sijui mahala gani , labda juu yam lima Kilimanjaro au bagamoyo katika hoteli fulani , au Zanzibar kuogelea na samaki wadogo
Ni mimi na wewe mpenzi
Tutajua hatima yetu , kuhusu mapenzi yetu na maisha yetu ya mbeleni , ukisharudi tukikutana siku hiyo , naogopa kufikiria sana au kuelezea sana kwasababu najua ni dhambi kuhisi vitu ambavyo havipo au pengine haviwezi kuwepo
Tutasheherekea mapenzi yetu mazuri na ya kweli kabisa Kwasababu hakuna mtu anayetumiliki , wala hakuna mtu anayeamua mambo yetu , hata huu uamuzi tulioufikia hakuna mtu aliyeamua , ila naona nahisi kuna wengi wanajifanya kwamba wameamua wao tuwe mbali kwa muda Fulani au pengine milele na milele .
Tutakutana , wewe uwe wangu nami niwe wako kuliko enzi hizo tulivyojuana kwa mara ya kwanza , kwasabu kila mtu atakuwa amerudi kwa ari mpya , kazi mpya na kila kitu kipya sasa kila mmoja wetu atajua anafanya nini kwa mwenzake .
Tutacheza na kufurahia pamoja
Huu upendo tulio nao pamoja
Lakini sasa uko dunia yako , sijui huko ulipo unajisikiaje na uko na nani na huyo nani anakushauri nini au anakusaidia nini kimawazo , najua hilo suala halinihusu , napenda kukusikia uko na amani na unaendelea vizuri na maisha yako mpaka siku hiyo tutakapo kutana tena sijui lini
Mimi pia niko katika dunia yangu , maisha yangu ni salama tu , hapa mjini mvua nyingi sana , natamani ungekuja kunipa angalau joto la mwili wako nami nikupe baridi la mwili wangu , nikukumbatie na kukubusu sehemu zote nzuri zinazokubalika , ila dunia yangu iko kimya sana kwasababu yako iko kimya kabisa .
Huo upendo ulioupanda katika moyo wangu na roho yangu ni upendo ambao hauwezi kuisha milele ,nawe unajua hilo .
Sijawahi kupata hisia hizi kabla na kitu katika moyo wangu unaniambia ni wewe pekee , je nawewe unajisikia sawa namimi ? nakutaka wewe wote , mwili wako na roho yako .
Ndoto zote nzuri ambazo hujawahi sema , kila kitu ambacho hujawahi kushirikiana kabla , kila baya na zuri lako
Jamani ninavyosubiria ,kusikia sauti yako
Na hayo maajabu ya penzi lako
Siku tukiwa wote katika giza
Nisikie mdundo wa moyo
Sina cha kuficha
Nakutaka wewe na kila kitu ambacho unataka katika penzi letu liwe bora na kudumu zaidi , utaelewa zaidi siku hiyo tukiwa tunasikiliza radio , nimekushika mkono kisha tuanze kucheza muziki taratibu .
Bado nakupenda na kukuhitaji sana , umeondoka wakati ambapo ndio nakuhitaji zaidi na sana .
Si utarudi tena ?
Hivi nilichelewa kukuambia haya ninayokuambia sasa ? kama nimechelewa naomba unisamehe sio makosa yangu ni makosa ya mawazo yangu nilihitaji kupumzika kwanza kuweka mambo sawa ili niandike vizuri sio uchochoro
Je nilichelewa kukuambia kwamba hakuna aliye juu yako ?
Unajaza moyo wangu na amani unaondoa mateso yote
Kutowa shida zangu , ndio unachofanya
Siku zangu huzijaza na upendo
Unajaza maisha yangu na tabasamu , ndivyo ulivyo
Kuna upendo unaolezeka , nao ni kati yangu na yako
Mwisho wa siku , inabidi tuombe na kumtukuza aliyetukutanisha