Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,393
- 31,344
Mkuu ni kwasababu zifuatazo..kwanini Waganda hawako bitter na jinsi jumuiya ilivyovunjika mwaka 1977 kulinganisha na sisi Watanzania?
..au kwanini Waganda hawana hofu na jumuiya mpya kulinganisha na Watanzania tunavyoiogopa jumuiya?
..kwanini Watanzania hatuko tayari ku-embrace / ku-dominate jumuiya mpya ya afrika mashariki wakati tulikuwa na miaka 43+ ya kujiandaa toka 1977 mpaka 2021?
1. hatukubali kuwa tuna matatizo ya kulitambua tatizo na kwamba tuna uwezo wa kuwa bora
Tumetawaliwa na inferiority complex hata pale tulipo na upper hand.
Mfano, sisi tulikubali soko huria , kwa muda mfupi tukawa mbali sana hasa kwa mawasiliano
Vyuo vyetu vinatoa watu bora (zama hizo nadhani) sisi hatuwezi kuwatumia wenzetu wanawatumia n.k.
2. Watanzania hatuna ujasiri wa kukabiliana katika ushindani. Hatukubali kuwa ushindani unatufanya tuwe bora na si uadui. Kwamba, tunahitaji changamoto ili kuongeza uwezo wetu wa kufikiri.
Mfano, badala ya kuifanya ATCL itoe huduma bora na ijiendeshe kibiashara, tumeua mashirika mengine ili kutoa monopoly. !!! Sasa hivi ATCL ni local haiwezi kushindana na KQ kwasababu rahisi , inaishi kwa monopoly na hakuna 'challenge' katika soko.
Ili uweze kutengeneza Tanbond bora lazima kuwe na Blue Band ya ushindani.
Tazama mfano wa kitaaluma. Ipo wapi UDSM iliyozalisha viongozi wa Afrika?
Iliyokuwa kitovu cha kweli cha wanasheria na Wachumi? Tumeua UDSM kwasababu hatutaki kusikia tofauti.
Nenda Makerere na Nairobi utaona tofauti kubwa , ule uhuru wa kitaaluma unawajenga na kutoa wasomi bora. Tukienda soko la ajira tunalalamika Wakenya wanachukua nafasi zetu.
Tunaweka sheria lukuki badala ya kuwaandaa vijana wetu kiushindani.
Tazana mijadala ya UDSM ya leo na udhaifu wake, unaweza kudhani ni uvccm vikaoni.
Kwa wale tuoijua UDSM ya zama hizo, ya leo inatushangaza.
Katika mazingira kama hayo, sera za nchi, mwelekeo na mtazamo hauchambuliwi kisomi.
UDSM inajifia taratibu, huko Makerere na Nairobi wanachanja mbuga.
Ironically, vijana wetu hawawezi kwenda kugombea soko la Uganda au Kenya. Sio kwamba hawawezi, la hasha, hawakujengwa katika ushindani. Wamelelewa katika monopoly na wanaishi na inferiority complex
Inasikikitisha nusu karne bado tunalalama na kuwaza kama zamani.
Tunalaumu EAC na Ukombozi tena wanaofanya hivyo ni watu tusiotarajia waseme hayo! hawana hoja hawatafuti majibu wanatafuta flimsy excuse