Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,886
- Thread starter
- #21
Nimesoma haya mahojiano yote, yanafungua macho. Shukrani kwa kuyaweka hapa.Ule mgawanyo wa Umbritch haukuwa fair, ila nchi zililazamika kukubaliana ili mambo yaishe hasa kwa vile wakati huo Tanzania na Uganda zilikuwa zimetoka vitani; alifanya kazi ya usuluhishi kwa karibu miaka kumi akamaliza mwaka 1982 baada ya vita. Ukisoma mahojiano yake hapa kwenye ukurasa wa 10 utaona kuwa hakukuwa na consensus kabisa kuhusu mgawanyo huo ambapo Kenya ilipata zaidi ya Tanzania wakati Uganda ndiyo iliyoonewa zaidi. Anasema mgawanyo wake ulifuata indicators za IMF, ambazo wakati huo zilikuwa zinaipendelea sana Kenya politically wakati huo kwa kuwa na uchumi ambao ni "market oriented"..
Huyu doctor anasema hicho kigezo cha kutumia indicator za IMF nchi zilikipinga hivuo hawakukitumia. Bali walitumia sababu za kijiografia na kuangalia usawa. Pia waligawana madeni ya jumuiya ambapo anasema nchi zilikuwa zinalipa vizuri sana.
Anasema nchi zilizopata assets nyingi zilitakiwa kulipa zile zilizopata assets chache ili kufikia usawa. Naona kama jamaa alifanya kazi nzuri sana. Na ndiyo umefanya hata huu ushirikiano wa sasa uweze kuwepo. Sioni kama kuna mtu alionewa.
Hili jumuia ilikuwa kubwa sana. Wafanyakazi 100,000 siyo mchezo!