Wakati dunia inafungwa, wewe fungua vitabu (vitabu 12 vya kusoma wakati unajikinga na virusi vya Corona)

Sawa, kisome na usipanik kama wengi wanavyofanya sasa.
Napenda sana kusoma vitabu, lakini muda unanibana sana, ni vigumu kupata ratiba ya kunipa muda mrefu wa kusoma, Nikipata muda nalala kwa sababu ya kasi ya maisha na kuchoka, nilikuwa kijana mdogo nilisoma vitabu vingi sana na vimenisaidia mpaka leo. Natamani kuwa kama zamani lakini nashindwa.
 
Hakuna kinachoshindikana mkuu,
Kama uliweza kusoma ukiwa kijana, hata sasa ukiamua utaweza.
Nina hakika kuna mambo mengi unayafanya hayana tija, ukiyapunguza hayo utapata muda wa kusoma.
Lakini pia kuna mifumo mbalimbali ya kusoma, mfano kuna AUDIO BOOKS, hizi unaweza kusikiliza ukiwa unaenda au unarudi kazini, badala ya kupoteza muda ambao labda unakaa kwenye foleni au usafiri unakuwa unasikiliza vitabu.
Kama unahitaji hizo AUDIO BOOKS tuwasiliane.
Kila la kheri.
 
Aisee nazihitaji sana hizo Audio books, je vitabu ulivyorodhesha hapo juu vina audio zake?
Nazipataje?
 
Ahsante kwa uchambuzi
Kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa mafua makali unaoendelea kwa sasa duniani, dunia imefungwa.

Karibu kila nchi duniani imesitisha safari kati ya nchi moja na nyingine, hivyo watu wanaofanya kazi kwenye sekta za usafirishaji, malazi na utalii kwa sehemu kubwa hawana kazi.

Karibu kila nchi duniani imesitisha shughuli zote zinazokusanya watu pamoja, hivyo watu wanaofanya kazi zinazohusu michezo, mikutano, makongamano na kampeni mbalimbali hawana kazi.

Karibu kila nchi duniani imesitisha shughuli za kimasomo, hivyo wanaofanya kazi kwenye mifumo ya elimu kama walimu na wengineo hawana kazi kwa sasa.

Karibu kila nchi duniani inasisitiza watu wake kukaa majumbani na kutokutoka nje na kujumuika na wengine kama hakuna ulazima. Hivyo watu wengi wanalazimika kukaa nyumbani na kutokuwa na vingi vya kufanya.

Sekta nyingi za kazi watu hawana kazi kwa sasa, ukiondoa sekta ya afya. Hivyo kama unafanya kazi kwenye sekta isiyo ya afya, kwa wastani wa siku 30 zijazo, huenda hutafanya kazi kabisa au hata kama utaenda kazini, basi hakutakuwa na majukumu mengi ya kikazi.

usitaharuki, soma vitabu.jpg

Ni katika hali hii, nimeona baadhi ya watu wakiulizana ni ‘movie’ gani za kuangalia katika kipindi hiki cha mapumziko ya lazima.

Mimi rafiki yako nakuambia usipoteze muda wako kuangalia ‘movie’, kwa sababu zitakuwa na mchango mdogo sana kwako.

Nikinukuu maneno ya aliyekuwa mchekeshaji Groucho Marx, aliwahi kusema; “I find television very educational. Every time someone switches it on I go into another room and read a good book.” Akimaanisha; nimegundua tv ni kitu kinachofundisha sana, kila mara mtu anapoiwasha, naenda kwenye chumba kingine na kusoma kitabu kizuri.

Rafiki yangu mpendwa, wakati wengine wanawasha tv kuangalia ‘movie’ au kufuatilia habari zinazoendelea, wakati wengine wanashinda kwenye mitandao kuhakikisha hawapitwi na chochote, mimi nakushauri ufuate alichosema Groucho Marx, nenda eneo tulivu na soma kitabu kizuri.

Swali ni je ni vitabu gani vizuri kwako kusoma?

Hapo chini nimekushirikisha vitabu 12 vizuri vya kusoma katika kipindi tunachopitia sasa. Vitabu hivyo vitakupa maana, utulivu, hekima na uelewa mpana wa jinsi dunia na mambo yanavyokwenda. Ukivisoma na kuvielewa vitabu hivi 12, utakuwa imara na hakuna hofu yoyote itakayoweza kukusumbua.

Karibu sana ujue vitabu hivi na kuvisoma, uzuri ni kwamba vitabu vyote hivi nimevichambua kwa kina, hivyo unaweza kusoma chambuzi zake na ukaelewa dhana kuu ya vitabu hivi.

Kupata vitabu hivyo pamoja na chambuzi zake, karibu ujiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA, fungua; www.t.me/somavitabutanzania kisha bonyeza JOIN CHANNEL na utaweza kupakua vitabu hivi pamoja na chambuzi zake.

Vifuatavyo ni vitabu 12 vizuri kwako kusoma katika wakati tunaopitia sasa.

1. HOW TO BE A STOIC: Using Ancient Philosophy to Live a Modern Life kilichoandikwa na Massimo Pigliucci.
Wakati dunia inataharuki na kukutaka na wewe utaharuki pia, kuna Falsafa moja ambayo inakupa utulivu mkubwa mno. Falsafa hiyo ni Ustoa (Stoicism). Falsafa hii inakutaka uishi kwa msingi wa kujua kilicho ndani ya uwezo wako na kukifanyia kazi na kilicho nje ya uwezo wako na kuachana nacho.

Pia falsafa hii inakupa msingi wa kuishi maisha yako yote ndani ya siku moja, kama vile ndiyo siku yako ya mwisho, usiahirishe chochote wala kutegemea chochote kwa siku zijazo. Ukiishi vizuri leo, kesho ikija ni zawadi kwako, na isipokuja basi hakuna ulichoacha.

Soma kitabu hiki, utajifunza mazoezi ya kistoa ya kufanya ambayo yatakupa utulivu mkubwa katika kipindi hiki cha taharuki.

2. Man's Search for Meaning kilichoandikwa na Viktor Frankl.
Viktor Frankl alikuwa mmoja wa Wayahudi waliowekwa kwenye makambi ya mateso wakati wa vita ya pili ya dunia. Kupitia kitabu chake cha Man’s search for meaning, Viktor ameeleza magumu ambayo alipitia katika makambi hayo, namna maisha yalivyokuwa ya mateso na ya kinyama.

Lakini pamoja na yote hayo, aligundua kitu kimoja, maisha hayakukosa maana. Baada ya kupitia mateso hayo, Viktor aligundua kwamba mtu anaweza kujua maana ya maisha yake kuputia njia tatu, kazi anayoipenda, watu anaowapenda au anapopitia mateso au magumu.

Katika wakati huu ambao unalazimika kuishi maisha ambayo hukuzoea huko nyuma, ni sehemu nzuri ya kujua maana na kusudi la maisha yako kama bado hujajua. Na kama umeshajua, basi kuhakikisha unaishi maana na kusudi la maisha yako. soma kitabu hiki na kitakupa mwongozo zaidi.

3. STILLNESS IS THE KEY ambacho kimeandikwa na Ryan Holiday.
Kitabu hiki tunajifunza nguvu kubwa iliyopo kwenye utulivu, ambayo tukiijua na kuweza kuitumia basi itakuwa ufunguo wa mambo mengi kwenye maisha yetu. Tangu enzi na enzi, ukiangalia kila aina ya falsafa au dini, utulivu umekuwa unasisitizwa sana. Ni kupitia utulivu ndiyo tunaweza kufikiri sawasawa, kuiona picha kubwa na kujua hatua sahihi za kuchukua.

Hakuna wakati ambao utulivu unahitajika kama sasa, kila mtu anataharuki na katika taharuki hii, wengi wanachukua hatua ambazo hazina msaada kwao. Soma kitabu hiki upate utulivu wa ndani, ufikiri kwa usahihi, ufanye maamuzi mazuri na maisha yako yaende vizuri.

4. Factfulness: Ten Reasons We're Wrong About the World--and Why Things Are Better Than You Think kilichoandikwa na Book by Anna Rosling Rönnlund, Hans Rosling, and Ola Rosling
Mambo mengi tunayoyajua kuhusu dunia siyo sahihi, vyombo vya habari vimekuwa vinakuza mabaya machache kuhusu dunia, lakini ukweli ni kwamba dunia inapiga hatua na kuwa bora zaidi kila siku. Ukiangalia takwimu sahihi za dunia, utaona wazi kwamba dunia inapiga hatua na maisha yanakuwa bora kwa wengi. Vita vimepungua, watu wanaishi miaka mingi, afya imeboreshwa na hata umasikini unapungua.

Katika hali tunayopitia sasa, taarifa nyingi zisizo sahihi zinasambazwa kwa kasi, watu wanaona kama vile ndiyo mwisho wa dunia. Soma kitabu hiki na utaona kwamba dunia iko imara sana na hili tunalopitia ni la muda tu.

5. SAPIENS: A Brief History of Humankind kilichoandikwa na mwanahistoria Yuval Noah Harari.
Yuval amefanya kazi kubwa ya kuchimba historia kamili ya binadamu tangu miaka 70,000 iliyopita ambapo ndipo historia ya binadamu imeanza kuhesabiwa wakati mapinduzi ya kifikra yalipotokea. Miaka 12,000 iliyopita ndipo mapinduzi ya kilimo yalipotokea na miaka 500 iliyopita, mapinduzi ya sayansi yalianza, ambayo ndiyo tunayaishi mpaka sasa.

kama hujui ni kwamba sisi binadamu wa sasa (homo sapiens) siyo jamii pekee ya binadamu (homo) ambayo imewahi kuwepo duniani. Zilikuwepo jamii nyingi za binadamu, ila hii ya kwetu ndiyo imekuwa yenye nguvu na hivyo kushinda na kuteketeza hizo jamii nyingine. Tumepitia mengi magumu kama binadamu na tukavuka, hili tunalopitia ni dogo sana. Soma kitabu hiki, utaielewa vyema historia yetu binadamu na utaona jinsi tulivyo na uwezo mkubwa wa kuvuka chochote.

6. SEEKING WISDOM; From Darwin to Munger kilichoandikwa na Peter Bevelin.
Mwandishi amefanya kazi kubwa ya kukusanya hekima za watu mbalimbali walioweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yao na kwenda kinyume na mazoea. Kuanzia mwanabaiolojia Charles Darwin ambaye alileta mapinduzi makubwa kwenye baiolojia kwa kufikiri tofauti, mpaka kwa mwanafalsafa mwekezaji Charles Munger ambaye pamoja na mshirika wake Warren Buffett wameweza kupata mafanikio makubwa sana kwenye uwekezaji, kuliko wawekezaji wengine wote.

Unachohitaji ili kuvuka kipindi hiki ni HEKIMA na kitabu hiki kitakusaidia sana kukupa namna ya kufikiri kwa usahihi na kufanya maamuzi sahihi. Moja ya misemo ya Charlie MUnger ni huu; “All I want to know is where I’m going to die, so I’ll never go there” akimaanisha; ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa hivyo nisiende hapo. Jua kwa hakika ni vitu gani vinaweza kukudhuru katika hali tunayopitia kisha viepuke.

7. THE LAWS OF HUMAN NATURE ambacho kimeandikwa na Robert Greene.
Kama kuna mambo watu wanayafanya na yanakuacha mdomo wazi kwamba imekuwaje wakayafanya, basi hujaijua asili ya binadamu. Kwenye kitabu hiki, Green ametupa sheria 18 za kuijua asili ya binadamu, akitupa mifano halisi iliyowahi kutokea kwa watu waliozingatia sheria hizi na wakafanikiwa au walizipuuza na kushindwa. Ametuonesha kwa nini watu huwa wanafanya mambo ya kikatili, hasa pale ambapo tunakuwa hatutegemei wafanye hivyo.

Katika hali tunayopitia sasa, itakusaidia sana kuijua asili yetu binadamu na moja ya vitu unapaswa kuelewa ni kwamba huwa tunafanya maamuzi kwa hisia na siyo kwa kufikiria na hilo ndiyo chanzo cha matatizo yote tunayopitia hapa duniani. Soma kitabu hiki uijue asili yako na jinsi ya kukabiliana nayo isiwe kikwazo kwako.

8. DIGITAL MINIMALISM: Choosing a Focused Life in a Noisy World ambacho kimeandikwa na Cal Newport.
Mwandishi Cal Newport baada ya kuona changamoto kubwa ya simu janja na mitandao ya kijamii kwa wengi, amekuja na falsafa bora ya matumizi mazuri ya mitandao hii, ambayo itakuwa na manufaa kwetu na kuondokana na madhara ya mitandao hii. Falsafa hii haibadili kitu kimoja kwenye matumizi yetu ya simu janja na mitandao ya kijamii, bali inabadili mfumo wetu mzima wa maisha na jinsi tunavyoichukulia na kuitumia mitandao hii. Falsafa hii anaiitwa DIGITAL MINIMALISM na ameieleza kwenye kitabu hiki.

Kama kuna kitu bora unaweza kufanya wakati huu wa taharuki, basi ni hiki; ACHA KABISA KUTUMIA NA KUFUATILIA MITANDAO YA KIJAMII. Sitaongeza chochote kwenye hilo, bali soma kitabu na utajifunza mwenyewe jinsi mitandao hii inasambaza taharuki haraka.

9. 21 LESSONS FOR THE 21ST CENTURY ambacho kimeandikwa na mwanahistoria Yuval Noah Harari.
Kwenye kitabu hiki, Yuval amezichambua changamoto kubwa 21 zinazotukabili kwenye karne hii ya 21 na kupendekeza hatua tunazopaswa kuchukua ili tusiachwe nyuma na mabadiliko yanayotokea kwa kasi kubwa.

Wakati kirusi hiki cha Corona kinakupa wasiwasi, jua kuna changamoto nyingine kubwa ambazo hazijapata nafasi ya kuvumishwa kama kirusi hiki, lakini zina madhara makubwa. Kupitia kitabu hiki, utazijua na hatua sahihi kwa mtu mmoja, nchi na dunia kwa ujumla kuchukua.

10. The Obstacle Is the Way kilichoandikwa na Ryan Holiday
Kitabu hiki kimeandikwa kwa msingi wa Falsafa ya Ustoa na kinaeleza kwa kina kile ambacho Mwanafalsafa Marcus Aurelius aliandika kwenye kitabu chake kinachoitwa Meditations. Marcus aliandika hivi; "The mind adapts and converts to its own purposes the obstacle to our acting. The impediment to action advances action. What stands in the way becomes the way." Akimaanisha; Akili zetu zina uwezo wa kupokea na kugeuza kikwazo chochote tunachopitia kuwa hatua ya kuchukua. Kizuizi kinachokukwamisha kuchukua hatua ndiyo kinachochochea hatua. Kinachosimama kwenye njia kinakuwa ndiyo njia yenyewe.

Hali tunayopitia sasa, unaweza kuiangalia kama kikwazo au kama njia, kwa kusoma kitabu hiki, utaweza kuigeuza kutoka kuwa kikwazo na kuwa njia. Mfano kama umeajiriwa na kwa muda mrefu umekuwa unajiambia unataka uanze biashara lakini hufanyi hivyo, hali hii itakulazimisha uwe na biashara ili usitegemee chanzo kimoja pekee. Soma kitabu hiki na kila kikwazo unachopitia utaweza kukigeuza kuwa njia.

11. Predictably Irrational kilichoandikwa na Dan Ariely.
Sisi binadamu huwa tunajiambia ni viumbe wa kufikiri, kwamba tunafikiri kwa kina kabla hatujafanya maamuzi yetu. Lakini Dan anatuonesha kwamba hisia zetu huwa zinaathiri maamuzi yetu, maamuzi mengi tunayoyafanya tunasukumwa na hisia na siyo kwa kufikiri. Hivyo kama unataka kufanya maamuzi sahihi, fanya wakati ukiwa huna hisia kali.

Hili liko wazi sana katika hali inayoendelea sasa, watu wanavaa vifaa vya kuzipa pua na mdomo wakati hawana maambukizi, haina msaada wowote na watu wanaambiwa lakini bado hawasikii. Vitu visivyo na umuhimu wowote vimepanda bei ghafla na vingine vimeisha kabisa. Yote haya ni kwa sababu mawazo yetu yanatawaliwa na hisia badala ya fikra. Soma kitabu hiki, uepuke kuendeshwa na hisia.

12. Blur: How to Know What's True in the Age of Information Overload kilichoandikwa na Bill Kovach and Tom Rosenstiel.
Tunaishi kwenye zama za mapinduzi ya taarifa, hakuna tena mwenye uwezo wa kumiliki taarifa au kuzuia watu wasipate taarifa fulani. Kwa sababu kila mtu anayo nguvu ya kusambaza na kupokea taarifa yoyote. Japo hili linakuwa faida kwa walaji wa taarifa, lakini pia linakuja na hatari moja, ni vigumu sana kujua usahihi wa taarifa unazopata hasa kwenye mtandao. Watu wengi wamefanya maamuzi kwa taarifa zisizo sahihi kitu ambacho kimewagharimu sana.

Kama ulikuwa hujaona madhara ya hili, unapaswa uwe umeliona katika hali inayoendelea sasa. Kila mtu sasa ni mhabarishaji, ni mshauri, ni mtaalamu na kila mtu anasambaza kila aina ya taarifa anayopokea. Ni vigumu sana kujua ipi taarifa ya kweli na ipi siyo ya kweli. Soma kitabu hiki na utaweza kujua jinsi ya kuchuja taarifa za kweli na zisizo za kweli.

Rafiki, katika likizo hii ya lazima ambayo unaipata, na kwa kuwa likizo hii haikupi wewe uhuru wa kusafiri au kutembelea maeneo mbalimbali, kaa chini na usome vitabu hivi 12. Hata kama ulishasoma baadhi, rudia tena kusoma, utajifunza mambo muhimu sana ya kukuvusha salama kwenye hili tunalopitia.

Kupata vitabu hivyo pamoja na chambuzi zake, fungua www.t.me/somavitabutanzania kisha bonyeza JOIN CHANNEL.

Nihitimishe kwa kukushirikisha mambo matano muhimu ya kufanya katika kipindi hiki tunachopitia sasa.

Moja; nawa mikono yako kwa maji na sabuni mara kwa mara.

Mbili; usishikane mwili au mikono na mtu ambaye huna uhakika kwamba hana maambukizi ya Corona.

Tatu; usishike uso wako, yaani macho, pua na mdogo kwa mikono ambayo hujaisafisha. Ukishika chochote, nawa kwanza kabla hujashika uso wako.

Nne; epuka mikusanyiko yote isiyo na umuhimu na ulazima, tulia nyumbani au kwenye kazi yako.

Tano; acha kufuatilia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Hali hii inakuzwa sana kuliko uhalisia wake, kama unataka kupata taarifa za maendeleo ya mlipuko huu tembelea sehemu zenye taarifa sahihi; shirika la afya na wizara ya afya.

Nikutakie kila la kheri rafiki yangu, utavuka hili salama, lakini vuka ukiwa bora kuliko ulivyo sasa kwa kusoma vitabu hivi 12 nilivyokushirikisha hapa.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania
Kilichinishangaza ni pale uliposema tusiifuatilie mitandao ya kijamii ilhali unatoa link ya kupata vitabu vyako !, lakini pia mimi binafsi hapa nimeipata habari yako hii kwenye mtandao wa kijamii, hebu fafanua ulimaanisha nini
 
Nafuatilia sana kazi zako mkuu, hongera kiukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tano; acha kufuatilia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Hali hii inakuzwa sana kuliko uhalisia wake, kama unataka kupata taarifa za maendeleo ya mlipuko huu tembelea sehemu zenye taarifa sahihi; shirika la afya na wizara ya afya.

Sehemu zinginezo niko pamoja nawe. Lakini kuhusu vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kwamba tusiifuatilie, mmmmm!
Sie wengine tunashinda humu JF kupata updates za covid 19, kwa hiyo tuache kuingia humu JF?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu zinginezo niko pamoja nawe. Lakini kuhusu vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kwamba tusiifuatilie, mmmmm!
Sie wengine tunashinda humu JF kupata updates za covid 19, kwa hiyo tuache kuingia humu JF?

Sent using Jamii Forums mobile app
Achana na habari zinazokufanya upaniki,
Wewe fanya kile kilicho sahihi kujikinga na maambukizi haya.
Kupaniki kutokana na habari hakutakusaidia lolote,
Ndiyo maana ni muhimu kuachana na habari.
 
ACHA KABISA KUTUMIA NA KUFUATILIA MITANDAO YA KIJAMII

Hapo nafikiri ingekua tutumie mitandao Kwa manufaa na uangalifu.

JF pia ni mtandao wa kijamii, ukisema acha kabisa kutumia na kufuatilia mitandao inamaana hata wewe haupaswi kuwa hapa, pia watu wasingevijua hivyo vitabu umependekeza.
 
Back
Top Bottom