WAKATI DUNIA IKIBADILIKA SISI HATULALI TUKIWAZA KUMNYIMA LISU UBUNGE.

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Anaandika Thadei Ole Mushi.

Pichani yupo Rais wetu Magufuli, yupo Lee Kuan Yew waziri mkuu wa kwanza kabisa wa taifa la Singapore, Netanyahu waziri mkuu wa Israel na Shekh Mohamed Maktoum waziri mkuu wa DUBAI.

Katika viongozi hao wote hapo ni Rais wetu ambaye anaongoza taifa lenye Rasilimali kuliko yote katika mataifa niliyoyataja kwa maana ya Israel, Falme za kiarabu, na Singapore. Yaani mataifa yote hayo hayana rasilimali yoyote kama madini, mafuta, gesi, au hata maeneo ya kilimo ambacho Tanzania inayo.

Cha kushangaza Katika nchi zote hizo Tanzania ndio maskini kuliko zote. Twende sawa hawapa.

1. Israeli:- Juzi niliwaambia kuwa waziri wao mkuu akiwa Nairobi alisema hawana chochote zaidi ya akili zao. Hawa tumewaongelea sana tuachane nao.

2.Falme za Kiarabu uchumi wao mkubwa wa nchi zote katika ukanda huo ni Mafuta. Cha kushangaza kabisa ni Dubai ambayo ni mojawapo ya nchi kutoka ukanda huo kuwa na kiasi Kidogo sana cha mafuta lakini inaendelea kwa kasi kuliko zote zenye mafuta.

#Dubai ni kweli kabisa haina mafuta wanachokifanya hununua mafuta tu na kuyahifadhi. Watu wengi hufikiri Dubai inaendelea au imeendelea kwa ajili ya mafuta si kweli.

#Siri kubwa katika maendeleo yao ni uwezo wa kuwavutia wawekezaji. Wana kitu wanakiita "Free trade and investments" katika hilo wameondoa kodi kabisa kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza Dubai ila wanaipata kodi yao baada ya wawekezaji kuanza kuzalisha. Haya ni matumizi makubwa kabisa ya akili vinginevyo wangelikuwa maskini wa kutupwa.

3. Singapore yenyewe ilipata Uhuru nyuma yetu 1965 iliwa haina kitu chochote. Hawa hawana rasilimali yoyote, hawana madini, hawana Gesi wala nini walichokifanya waliamua kutulià chini ya Lee Kuan Yew na kufanya mambo ambayo ukitaka kutulinganisha sisi na wao ni mbingu na Ardhi. Singapore inazipita nchi nyingi za ulaya kwa kutoa huduma za kijamii kama vile Elimu na Afya. Uwanja wao was ndege wa Changi unapambana vilivyo na Amsterdam airport. Kwa mwaka hawa wanapokea wasafiri Milioni 58.7 airport hii ipo busy hasa na hawana maneno mengi unapoingia Singapore wao wanakupa kadi unapoingia wanakuambia ukikamatwa na madawa ya kulevya adhabu ni moja tu Kifo hili si la kupelekana mahakamani.

Wana tumia neno moja maarufu KIASU lenye maana ya target yao ya kuongoza kwa kila kitu duniani. Kiasu ni kuogopa kushindwa au kupitwa. Watu wanapambana haswa Singapore na ni mojawapo ya nchi inayokua kwa kasi kuliko zote Duniani kwa sasa. Hiki ndio kisiwa cha Singapore ambacho kilikuwa in makazi ya wavuvi wasiokuwa na mbele wala nyuma mpaka 1965 lakini sasa hivi wanakimbizana na marekani na nchi nyingi za ulaya.

DUNIA INAHAMA.

Si vibaya kuwa na Rasilimali kama Gesi, Madini na Malighafi nyinginezo. Watu wanawekeza sana kwenye matumizi makubwa ya akili kuliko malighafi. Mataifa mengi ya Afrika hujisifu usiku na machana kuanzia January hadi December kuwa tuna Rasilimali nyingi kuliko ulaya, kwa hapa Tanzania ndio usiseme tunaringia position tulizopo kwenye wingi wa dhahabu utasikia sijui Tanzania ni ya pili, Tanzanaite ni ya kwanza, almasi sijui ni ya Tatu, Tuna mlima mrefu kuliko yote na kadhalika lakini je zinatufaishaje? Je tumeweza kutoa elimu bure hadi chuo kikuu? Hapana, tumeweza kutoa Afya bure kabisa? Hapana he tumepunguzaje tatizo la ajira? Ndio linazidi kuongezeka nk.

Dunia inawaza tofauti wanataka kuachana na Malighafi za Afrika kama vile pamba na madini. Wanawekeza zaidi kwenye technolojia. Iangalieni China inakimbizana na technology sio migodi na nchi nyingi zipo kwenye mwelekeo huo miaka mia ijayo utabaki na dhahabu yako, almasi yako nk watu wanakimbizana na dhahabu mpya inayoitwa Technolojia. Kampuni na Apple likiweka simu mpya Sokoni kila mtu duniani anajigusa nk.

Uhusiano tulionao kati yetu na mataifa ya magharibi unaenda kubadilika kutoka kutegemeana kwenye misaada vs Malighafi zilizopo Africa. Kwa sasa tuna uhusiano wa unequal exchange lakini tunaelekea kubaya zaidi ambako hawatawaza tena hizi malighafi watatu neglect kwa maana hiyo utazalisha pamba ambayo hujui utaipeleka wapi au utachimba dhahabu ambayo utabaki nayo.

Wakati huo huo tunaendelea kufundisha kinjekitile kuanzia la tano hadi chuo kikuu, watu hawalali wanawaza tutashindaje pale Singida mashariki kwa Lisu ni mbinu na mikakati usiku na mchana inapangwa. Vijana wetu wapo busy kwenye kubeti na kucheza madongolo ya mchina ya kutumbukiza mia mbili mia mbili nk.

#Tunawaza mambo marahisi mno..... Sitaki kuongea sana..... Tuendelee kuyaweka haya kwenye maandishi yanaweza kutumika kama sio Leo ni kesho

Ngoja nirudi Jalalani, Leo nipo kwenye jalala la Lumumba huku hakuna kuwaza ni kuimba litania za masifu na mapambio angalau MTU aambulie chochote.

Ole Mushi.
0712702602
 
Ole Mushi nimekuelewa lakn kinacho sababisha yote haya ni ELIMU. Viongozi wetu wawekeze kwanza kwenye ELIMU ndio litakuwa suluhisho.
 
Ole Mushi nimekuelewa lakn kinacho sababisha yote haya ni ELIMU. Viongozi wetu wawekeze kwanza kwenye ELIMU ndio litakuwa suluhisho.
ukielimisha kizazi chako itakuwa ngumu kukitawala utakavyo...ni sawa na kuoa mke msomi hutamburuza utakavyo - ndiyo maana unakuta Prof mzima kaokota msichana darasa la saba....maana hata ukirudi asubuhi hauulizwi ulikotoka cha msingi ameshiba basi....

Watanzania wanaolewa mambo ni kati ya 10 - 15 % tuliobakia sisi ni kufuata upepo unakovuma....na huu ni mtaji wa watawala.....
 
Mohamed al Makhtoum ni ruler of Dubai(sio PM) ila pia ni Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa UAE(Muunganiko wa Emirati)....

Hayo mengine umegongelea msumari penyewe kabisa. Tuna safari ndefu mno
 
ukielimisha kizazi chako itakuwa ngumu kukitawala utakavyo...ni sawa na kuoa mke msomi hutamburuza utakavyo - ndiyo maana unakuta Prof mzima kaokota msichana darasa la saba....maana hata ukirudi asubuhi hauulizwi ulikotoka cha msingi ameshiba basi....

Watanzania wanaolewa mambo ni kati ya 10 - 15 % tuliobakia sisi ni kufuata upepo unakovuma....na huu ni mtaji wa watawala.....
Ushauri wako ni upi sasa
 
Ole Mushi nimekuelewa lakn kinacho sababisha yote haya ni ELIMU. Viongozi wetu wawekeze kwanza kwenye ELIMU ndio litakuwa suluhisho.
Elimu NI kila kitu sijui kwanini watu hawaelewi aliyesema tusichimbe madini mpaka tuelimike aliona mbali.Mfano kijijini familia za Kwanza kujenga nyumba Bora nakuachana na nyasi ni familia ya waliosoma,wazee wa Kwanza kutoka vijijini na kuja kupumzika au kutibiwa mijini kama Dar ni wazee walio somesha.Familia Bora zinazo ongoza zenye exposure NI za walio soma.
 
Back
Top Bottom