Wakati Dkt. Kigwangalla anagawa baiskeli kama karanga, wafanyakazi wa Tanapa hawajalipwa mshahara miezi miwili sasa!

Akichangia hotuba ya sheria ya bajeti mbunge Magdalena Sakaya amemtaka Waziri wa Utalii na maliasili Dkt. Kigwangalla kushughulikia suala la mishahara ya watumishi wa Tanapa kwa dharura.

Sakaya amesema wafanyakazi wa Tanapa hawajalipwa mishahara kwa miezi miwili hivyo ni vema waziri Dkt. Kigwangalla akaacha legacy kwa kutatua suala hilo kabla hajastaafu hivi karibuni.

Maendeleo hayana vyama!
Anasema ameuza mpunga magunia ya kutosha
 
Jamaa huko twitter kasema ameuza mpunga gunia 1500 kwa TZS 65,000 kila gunia.

Navyomjua Kigwa, angepiga hata pichq za hayo mashamba na kutonesha hatua zote hadi akimalizia kuvuna achilia mbali mauzo aliyofanya.

Sijui kamuuzia nani huo mzigo.

Sijui kama hata kodi na ushuru amelipa.
 
Hii tabia ya Channel ten kukatisha matangazo pale ambapo wabunge wa upinzani wanapoanza kuchangia au kutajwa na Spika haijakaa sawa. Kwa mfano leo wamekatisha wakati Msemaji wa Kambi rasmi ya upinzani alipotajwa kuwasilisha maoni, wakarudi wakati wa kuchangia, aliposimama Zitto Kabwe kuchangia hata hajamaliza wakakata tena.

Inakera
wanateseka sana
 
Akichangia hotuba ya sheria ya bajeti mbunge Magdalena Sakaya amemtaka Waziri wa Utalii na maliasili Dkt. Kigwangalla kushughulikia suala la mishahara ya watumishi wa Tanapa kwa dharura.

Sakaya amesema wafanyakazi wa Tanapa hawajalipwa mishahara kwa miezi miwili hivyo ni vema waziri Dkt. Kigwangalla akaacha legacy kwa kutatua suala hilo kabla hajastaafu hivi karibuni.

Maendeleo hayana vyama!

Mbona hakuna Logical Connection kati ya Headline yako na Content hii ya Uzi? Nilitegemea hapa sasa ndiyo ungetuhabarisha zaidi kile unachokijua.
 
Back
Top Bottom