Wakati CUF wakijiandaa kuandamana: Mbunge Magdalena Sakaya na wenzie waachiwa huko Tabora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati CUF wakijiandaa kuandamana: Mbunge Magdalena Sakaya na wenzie waachiwa huko Tabora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WISDOM SEEDS, Jun 7, 2011.

 1. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Lipumba alitangaza
  leo kuwa wanajiandaa kufanya maandamano makubwa kufuatia viongozi wao
  kunyimwa dhamana, na wakati huu taarifa inatolewa kuwa mbunge wao,
  Magdalena sakaya na viongozi wengine wameachiwa.

  Hii maana yake nini, polisi hawataki kuwaachia viongozi wa upinzani hadi
  watakaposikia kuna mipango ya kufanya maandamano!
   
 2. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Inamaana bila ubabe kutangazwa nchi hii haiendi. Dawa ya moto ni moto na wala sio maji
   
 3. M'bongo

  M'bongo Senior Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mh, hii sasa kali. Yaani kama hakuna mpango wa maandamano basi huwezi
  kupata haki yako? Wapi tunakwenda?
   
 4. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hivi hii nchi ni ya askari wa Jk tu! Mbona naona kama kuna ka unyanyasaji fulani hivi
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  kama vipi tuandamane labda JK ataondoka
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kumbe jaribu uone shughuli yake utafikili libya...
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani hawa jamaa wamekaa kama fundi umeme bila tester hafanyi kazi, inasikitisha sana kuona mahakama zikifanya shere kwa viongozi wa upinzani! Labda bado hawaamini kuwa ipo siku nchi inaweza kuongozwa na upinzani.
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nadhani mtu akishapelekwa mahakamani swala la kutoa dhamana linakuwa chini ya mahakama na sio polisi. Polisi wanatoa dhamana pale tu mtuhumiwa akiwa chini ya himaya yao.
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  kutesa kwa zamu. Kuna siku askari mdogo atapanda cheo na kuwa mkubwa na hapo ndo patakuwa patamu.
   
 10. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Ha!!!yaani mtoto bila viboko haendi!!!?.Jk kwa namna hii ya kuendesha nchi kihuni tutafika kweli!!!?Hii ni Kali ya mwaka
   
 11. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hebu jaribu hii! Hawa wanasiasa huwa wanapima upepo wa mahakama na kutoa vitisho vya kibazazi. Hao CUF walikuwa wapi hata viongozi wao wakakaa siku 15 jela. Kwa uzushi uleule Lipumba alikwenda kutaka kumtowa Mbowe huku akiachia viongozi wake wakinyia ndooni na wala hatukuwahi kusikia mipango ya maandamano. Ni jana tu wakati tukipata tetesi kuwa huenda wakaachiliwa ndio CUF wanakurupuka na kudai watafanya maandamano.
  Kwa upande wa CHADEMA vile vile hata kipofu gani alijuwa kuwa Mbowe akienda mahakamani atarejeshewa dhamana yake halafu wanatokea na kutowa saa 48 kama sharti ya kuachiwa Mbowe.
  Tatizo letu Watanzania njaa inatufanya tusiwe na uwezo wa kufikiri na viongozi wa kisiasa wanachukulia advantage kukata tamaa kwetu. Wanasiasa wao ndio walioko bungeni na wana uwezo na sauti ya kulazimisha watendaji wa Serikali kutuondolea matatizo badala yake wanatufanya tuache kazi za kujitafutia riziki kuungana nao kwenye maandamano ambayo hayaleti maisha bora isipokuwa fujo. Wao wanasiasa siasa ni kazi yao hivyo wanakula kwa hayo maandamano lakini mwananchi anaambulia mabomu ya machozi na vifo na wanapotiwa ndani wanateseka huku waliowachombeza haweana habari wakiendelea na mradi wao kwa kutumia wananchi.
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakubaliana na wewe. Wakati mbunge wake ananyea ndoo huko Tabora, Lipumba alikuwa central Dar kwa Mbowe. Sijui hata kama alimwona. Halafu aliingia pale kwa gia eti yeye ni kiongozi sijui wa NGOs fulani. Ya nini yote hayo wakati tunamjua yeye ni mwanasiasa kama wengine? Uzushi mtupu. Tena heri mbunge wa CUF Bi. Magdalena Sakaya alikamatwa sio kwa kiuka amri ya mahakama kama Mh Mbowe bali alikwenda Urambo kwa ajili ya kufuatilia mauaji na vurugu zinazoendelea jimboni humo. Sijui nazo sio shughuli za kibunge? Maana siku hizi imekuwa kama fasheni vile. Ukiwa mbunge kila unachofanya unakingwa na wananchi wanaelekea kulikubali hilo.
   
 13. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Kwani huko Tabora kulikuwa na coverage ya media? Lipumba alikwenda central police
  kwa kuwa aliamini atapata coverage nzuri kwa kuwa vyombo vyote vya habari vilikuwa
  vinafuatilia suala hilo. Kwa kuwa alishajua kuwa nyota yake imeanza kufifia hivyo
  aliamua kufanya juhudi ya kuisafisha ili ing'ae tena.
   
Loading...