MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,172
- 23,975
Kushinda Uchaguzi wa siasa na kushika dola unahitaji udhamini wa makundi muhimu katika jamii. Haijalishi unashinda kwa kuiba kura au kutoiba kura lakini la muhimu sana kama hujapata udhamini wa makundi muhimu katika jamii huwezi kushinda kura na kuchukua dola.
Kila nchi inatofautiana kuhusu aina ya makundi muhimu ya wadhamini yanayopelekea kushinda uchaguzi mkuu na kushika dola. Kwa mfano katika nchi ya Uingereza, makundi muhimu ya wadhamini ambayo huwezi kuyadharau ni mashoga na wayahudi. Ukidharau hata kundi moja katika haya mawili basi usahau pia kushinda uchaguzi na kushika dola.
Kwa Tanzania ukikumbatia kundi la Ushoga kuna uwezekano mkubwa huwezi kushinda Uchaguzi Mkuu na kushika dola. Hata hivyo Tanzania hatuna kundi kubwa la Wayahudi na kwa mantiki hii sio kigezo katika mustakabali wa uchaguzi mkuu.
Makundi ya udhamini kwa Tanzania ambayo ni muhimu sana kukumbatia wakati wa Uchaguzi Mkuu ili ushinde na kushika dola ni kundi la madhehebu ya dini na pia wananchi wanaoishi vijijini na mjini ambao wana kipato cha chini.
CCM kwa kutambua umuhimu huu ndio maana wameanza kujiimarisha kwenye haya makundi wakati wapinzani wakianza kuyadharau na kuyatukana.
Hii imeonekana baada ya Rais Magufuli kukutana na makundi ya madhehebu ya dini na wachimbaji wadogo wa madini na wafanya biashara ndogo ndogo.
Viongozi wa Upinzani ambao wengine ni wajumbe wa Kamati Kuu za vyama vyao wamejitokeza na kuanza kuyashambulia makundi haya mpaka wengine wanayatukana.
Tumewasikia kina Godbless Lema, Peter Msigwa, Halima Mdee, John Heche na Boniface Jacob ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wakiwatukana viongozi wa madhehebu ya dini baada ya kukutana na Rais Magufuli.
Mashambulizi haya hayawasaidii wapinzani bali yanaisaidia sana CCM kuzidi kujiimarisha zaidi kadri Uchaguzi Mkuu unavyokaribia. Kwa mwendo huu 2020 itakuwa hali mbaya sana kwa wapinzani.
GONGA LINK>>>Askofu Kakobe: Viongozi wa CHADEMA watubu hadharani kwa kuwatukana viongozi wa dini
Kwa mfano, nchi masikini kama Tanzania huwezi kupata wanaojitoa mhanga kuandamana kwa kutegemea pekee kundi/tabaka aali (elite). Hili ni tabaka ambalo lilichonacho ni kikubwa zaidi ya kitacholifanya liandamane. Hili ni kundi linaongea sana lakini matendo ni zero. Kwa mfano Godbless Lema wa sasa sio yule wa kabla hajapata ubunge. Lema wa sasa ameingia kwenye kundi la aali (elite) na kwa sababu hii huwezi kumuona eti anahamasisha maandamano ‘’haramu’’. Alichonacho kwa sasa ni zaidi ya kile atakipata kwenye maandamano ‘’haramu’’.
Aliyekuwa Rais wa DRC, Joseph Kabila amlipigwa kwa nguvu kuongeza muhula mwingine wa utawala na makundi hayo muhimu niliyoyataja na sio kundi la aali (elite). Makundi ya madhehebu ya dini na wananchi masikini walijitokeza kwenye maandamano bila kujali athari zao kimaisha kwa sababu hakuna walichokuwa wanapoteza katika maandamano mpaka Rais Kabila akaondoa nia hiyo.
Niliwahi kusema kwenye Thread hii,
GONGA LINK>>>Nape na Bashe wamewapa CHADEMA somo la siasa za CCM
Tumeona kwenye chaguzi ndogo ambapo wale wanachama wa CCM ambao walidhaniwa kuwa ni ‘’waasi ndani ya CCM’’ walijitokeza na kuongoza kampeni za CCM katika chaguzi hizo wakati wapinzani wakishindwa hata kuungana na kusimamia mgombea mmoja.
Wakati wa Uchaguzi Mkuu wapinzani hufarakana wakati CCM huungana na hujiimarisha kwa sababu wanajua umuhimu wake. Hii imeanza kujitokeza.
Siasa sio jazba bali ni sayansi ambayo ina misingi yake kutokana na mazingira. Huwezi kufanikiwa kisiasa kama unadharau misingi yake.
CCM pamoja na mapungufu yao lakini wanajua maana ya sayansi ya siasa katika mazingira ya Tanzania.