Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Miaka kadhaa iliyopita CCM ilihangaika kujivua 'magamba' lugha iliyomaanisha wanachama wasio na maadili. Na sasa wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa sura mpya zinakuja, Ndugu Polepole ambaye ameteuliwa kama Katibu wa Uenezi na Itikadi amezungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya chama mara kadhaa bila kumung'unya maneno amesema 'mafisadi,wezi wa mali za umma na wasiolipa kodi CCM si mahala pao tena' akaendelea kusema CCM itaisimamia serikali kudumisha maadili, hakika ni maneno 'kuntu' yanayoleta matumaini mapya katika taifa hasa ukizingatia nia ya viongozi kurudisha chama kwa wananchi.
Upande wa Pili, washirika wa Ukawa chini ya Lowassa,Kingunge,Sumaye na Masha wao wamewapiga marufuku wafuasi wa vyama vyao kukemea na kupiga vita ufisadi na ukiukwaji wowote wa maadili 'kama una ushahidi nenda mahakamani', waache kila mbuzi ale urefu wa kamba yake.
Kama tujuavyo Lowassa kwa sasa pamoja ndiye mwenye 'Ukawa' pia jukumu lake kuu ni kushughulikia uenezi na mawasiliano kwani yeye ndiye msimamizi wa propaganda zote za 'ukawa' ikiwamo kuhakikisha media na waandishi wanafanya ayatakayo upande wa pili CCM imempa jukumu hili Kijana machachari Humprey Polepole asimamie uenezi na itikadi kwa kutumia maadili na taaluma.
Je kwa chadema kujifunika 'magamba' haya gubigubi watapata tija?