Wakati CCM inajivua, CHADEMA wanajifunika magamba 'gubigubi'

tatizo la huu upupu ni serikali kukiri hakuna mafisadi baada ya mahakama walioianzisha tena kwaa mbwembwe na vigelegele kukosa kesi na sasa wanadai hakuna ufisadi......................sasa haya magamba yako kichwani mwa watu lakini uhalisia unawasuta.................
Pia unatakiwa kuelewa au kutambua kwamba hii serikali si ya Jakaya, kama kuna ufisadi unafanyika leo unapashwa kulaumu, JPM hakuja kufanya ujinga wa kufukua makaburi, kwanza si wajibu wake kufanya hivyo, na ndo maana wakaririshaji baada ya kutukana sana pale mwembeanga mafisadi na ushahidi walisema wanao, ilikuwa ni wakati wa wao ss kufungua kesi na bahati nzuri ushahidi walikuwepo nao-lakini wameufyata leo analaumiwa JPM je hiyo ni sahihi?
 
Unaweza kutaja watakao jivua ndani ya ccm kwa ufisadi? Na je kama wapo kwa nn hiyo mahakama imekosa kesi ya kusikiliza?
Hayo ya mahakama waachie wanasheria...huku CCM hata ukituhumiwa tu kwa ufisadi kwa sasa unahamishiwa chadema na gamba lako.
 
Hayo ya mahakama waachie wanasheria...huku CCM hata ukituhumiwa tu kwa ufisadi kwa sasa unahamishiwa chadema na gamba lako.
Tokea lini ccm wakajivua gamba? Je joka la makengeza, magufuri wa nyumba za serikali naye atajivua? Kinana wa meno ya tembo je? Pole pole wa mishahara Mara mbili je? Mwiguru wa BOT? Je wale wa escrow na visandarusi vipi? Pia nakuomba uweke mfano wa watakaojivua gamba ccm.....
 
Meanwhile boss wenu huko Lumumba Mzee wa kubanduka ngozi anabwabwaja tu, nakutuaminisha mahakama ya mafisadi imekosa wateja.
 
adef00eb1673c06069d523bb787ea460.jpg
WEwe na mchokozi
 
Thread za hawa watu ni km taarabu za akina Khadija Kopa na Mzee Yusuph.
Poleni. Naona mnajaza server za JF kwa thread ambazo hazina kichwa wala mkia.
THREAD ZA HAWA WATU WAKUDADAVUA, LIZABONI, YODAYA, MAGONJWA MTAMBUKA NA WENGINE
HAZINA MCHANGO WWTE. HUWA NI KERO

KUNA MAMBO MUHIMU YA KUZUNGUMZIA KTK NCHI. MUONE SALARY SLIP AU TECHNICALLY AWAPE DARASA
 
Kama no mafisafi kwann mahakama mliyoianzisha kwa mbwembwe mkitumia kodi za wananchi mmekosa wateja na kwann mlifungua hiyo mahakama wkt mahakama kuu inaweza kushughulikia makosa kama hayo.....?small mind type
 
Miaka kadhaa iliyopita CCM ilihangaika kujivua 'magamba' lugha iliyomaanisha wanachama wasio na maadili. Na sasa wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa sura mpya zinakuja, Ndugu Polepole ambaye ameteuliwa kama Katibu wa Uenezi na Itikadi amezungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya chama mara kadhaa bila kumung'unya maneno amesema 'mafisadi,wezi wa mali za umma na wasiolipa kodi CCM si mahala pao tena' akaendelea kusema CCM itaisimamia serikali kudumisha maadili, hakika ni maneno 'kuntu' yanayoleta matumaini mapya katika taifa hasa ukizingatia nia ya viongozi kurudisha chama kwa wananchi.

Upande wa Pili, washirika wa Ukawa chini ya Lowassa,Kingunge,Sumaye na Masha wao wamewapiga marufuku wafuasi wa vyama vyao kukemea na kupiga vita ufisadi na ukiukwaji wowote wa maadili 'kama una ushahidi nenda mahakamani', waache kila mbuzi ale urefu wa kamba yake.

Kama tujuavyo Lowassa kwa sasa pamoja ndiye mwenye 'Ukawa' pia jukumu lake kuu ni kushughulikia uenezi na mawasiliano kwani yeye ndiye msimamizi wa propaganda zote za 'ukawa' ikiwamo kuhakikisha media na waandishi wanafanya ayatakayo upande wa pili CCM imempa jukumu hili Kijana machachari Humprey Polepole asimamie uenezi na itikadi kwa kutumia maadili na taaluma.

Je kwa chadema kujifunika 'magamba' haya gubigubi watapata tija?

Umenena vyema kabisa.

Kwa kuongezea tu, licha ya kujifunika magamba, huko chadema ukiwa na fedha zako unanunuwa mpaka tiketi ya kugombea Urais.

Nani wa kubisha hilo?
 
Kama no mafisafi kwann mahakama mliyoianzisha kwa mbwembwe mkitumia kodi za wananchi mmekosa wateja na kwann mlifungua hiyo mahakama wkt mahakama kuu inaweza kushughulikia makosa kama hayo.....?small mind type


Mahakama inachukuwa kesi za ufisadi (papa) wa hali ya juu, na kwa hivi sasa chunguzi nyingi zipo jikoni, ngoja ziwive ujionee.
 
Mahakama inachukuwa kesi za ufisadi (papa) wa hali ya juu, na kwa hivi sasa chunguzi nyingi zipo jikoni, ngoja ziwive ujionee.
Kwani mahakama kuu haiwezi kushughulikia kesi za ufisadi.....?na tusidanganyane hukuna uchunguzi wowote unaoendelea mvua tano zitaisha usemi utakuwa ni huu huu
 
Back
Top Bottom