Wakati CCM inafanya siasa, BAWACHA mkoani Manyara wafikishwa Mahakamani kwa kufanya siasa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,095
103,345
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewafikisha Mahakamani Viongozi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara kwa kosa la kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.

Akithibitisha kukamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa Viongozi hao RPC wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga amesema Viongozi hao wamekamatwa mnano tarehe 15/01/2022 katika maeneo ya Katesh Stand, Wilaya ya Hanang, Manyara.

Kuzaga amewataja viongozi hao waliokamatwa kuwa ni Ngigula Rafael 45) Mwenyekiti wa BAWACHA Manyara, Valentina Shayo (37) Mhasibu BAWACHA na Tasira Karama, Mjumbe wa Kamati Tendaji BAWACHA Manyara.

Polisi wamesema Wahumiwa hao wamekamatwa kwa kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali na baada ya kuhojiwa na Polisi walikiri kufanya kosa hilo la kufanya mkutano bila kuwa na kibali na baada ya Polisi kukamilisha upelelezi 17/01/2022 walifikishwa Mahakamani.

Shauri hilo limepangwa kuendelea tena 16/02/2022 kwa hatua ya usikilizaji wa awali, ambapo Polisi Mkoa wa Manyara imetoa wito kwa Wakazi wa Manyara na Vyama vya Siasa kufuata taratibu za ufanyaji wa mikutano kwa kuwa na kibali kutoka mamlaka zinazohusika.
 
Na mkome!

Si mnapumua nyie?

Sasa haya mambo ya kufikishwa mahakamani yanatoka wapi tena?
 
Chama hiki kilishaamua kumuasi Mwenyezi Mungu na kuandamana na "yule mwovu" ndio maana kwao unyanyasaji, ukatili, uonevu, uharibifu na uongo kwao ni utamaduni na sifa yao. Ila siku zaja kila jiwe litageuzwa.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewafikisha Mahakamani Viongozi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara kwa kosa la kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.

Akithibitisha kukamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa Viongozi hao RPC wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga amesema Viongozi hao wamekamatwa mnano tarehe 15/01/2022 katika maeneo ya Katesh Stand, Wilaya ya Hanang, Manyara.

Kuzaga amewataja viongozi hao waliokamatwa kuwa ni Ngigula Rafael 45) Mwenyekiti wa BAWACHA Manyara, Valentina Shayo (37) Mhasibu BAWACHA na Tasira Karama, Mjumbe wa Kamati Tendaji BAWACHA Manyara.

Polisi wamesema Wahumiwa hao wamekamatwa kwa kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali na baada ya kuhojiwa na Polisi walikiri kufanya kosa hilo la kufanya mkutano bila kuwa na kibali na baada ya Polisi kukamilisha upelelezi 17/01/2022 walifikishwa Mahakamani.

Shauri hilo limepangwa kuendelea tena 16/02/2022 kwa hatua ya usikilizaji wa awali, ambapo Polisi Mkoa wa Manyara imetoa wito kwa Wakazi wa Manyara na Vyama vya Siasa kufuata taratibu za ufanyaji wa mikutano kwa kuwa na kibali kutoka mamlaka zinazohusika.
Staili hiyo yazidi kukosa mvuto na nguvu kwenye siasa.
Makaburu walifanya hivyo hivyo, hata hivyo waliyotenda waliishia kuja kuungama wakilia mbele ya tume ya maridhiano. Ninaiona wakati wake u karibu sana. Wa shetani watakuja jisema HADHARANI na huku WANALIA watashindana kutajana. AMEN.
 
Mnavunja sheria kusudi ili muonewe huruma, this time tumesema hatuangushiwi gari bovu.
 
Back
Top Bottom