Uchaguzi 2020 Wakati CCM ikinadi sera yao kuu ni kudumisha Amani na Utulivu, wao wenyewe ndiyo mabingwa wa kuivunja Amani hiyo

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,342
2,000
Katika maandiko ya Biblia takatifu katika kitabu cha Mithali 14:34 kinasema hivi "Haki huinua Taifa, Bali dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.

Kutokana na maandiko hayo na sera hiyo kuu ya CCM, wao wanafanya "vice versa" ya sera hiyo.

Kwa kuwa haiwezekani kwa chama kinachodai kuwa sera yao kuu ni kudumisha amani na utulivu nchini, wakati huo huo Tume ya uchaguzi ya Taifa, imewaengua "kihuni" wagombea wa uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu, wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani, zaidi ya 500 nchini kote, wakati hakuna mgombea hata mmoja kutoka chama cha CCM aliyeenguliwa!

Hivi sasa ni zaidi ya wiki tatu wagombea hao wamepiga kambi mjini Dodoma, wakisikilizia rufani zao walizokata kwa Tume hiyo ya uchaguzi, huku Tume hiyo "ikisuasua" kusikiliza rufaa hizo.

Kibaya zaidi hao wasimamizi wa uchaguzi, maDED's, ambao ni wateule wa Rais, wamewakata bila sababu za msingi, wagombea hao wa upinzani katika yale maeneo ambayo wao CCM wanajua wazi kuwa "piga ua" hawana ubavu wa kushinda.

Hao Tume wamewaengia wabunge 15 kati ya wabunge 18 wa ACT Wazalendo wanaogombea katika visiwa vya Pemba, wakati wanajua wazi kuwa hivyo visiwa ni kambi isiyoyumba kwa Maalim Seif

Vile vile wameenguliwa "kimizengwe" wagombea uidiwani 16 wa Chadema, kati ya idadi yote ya madiwani 36 wa jijini Mbeya ambako ni ngome imara ya Chama cha Chadema.

Licha ya hao wagombea wengine mania kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Nawauliza CCM hivi kitu gani kinachowatia hofu sana katika uchaguzi ujao, wakati mnajua kuwa vyombo vyote vya habari vya Umma na vya binafsi, kwa masaa yote 24, vinaimba mapambio ya "kusifu na kuabudu" juhudi za utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 katika kujenga miundi mbinu ya barabara za lami nchi nzima, ujengaji wa "mafly oves" kwenye majiji makubwa, kununua ndege kubwa za aina ya Bombardiers, kujenga reli ya kisiasa ya SGR, kutengeneza bwawa la Stieglers Gorge huko mto Rufiji?

Hivi chama kilichowafanyia mambo makubwa sana wananchi, huku kikiwapiga "pini" kufanya siasa vyama vya upinzani, ndicho cha kuogopa kiasi hiki vyama vya upinzani?

Nimeamini kuwa hivi sasa CCM ipo "Intensive Care Unit" ikipumulia mashine, huku chama hicho kikitegemea kubebwa na vyombo vya dola, kama vile Jeshi letu la Polisi, TRA na watendaji wengi wa serikali hii ya serikali ya awamu ya 5 wakijiona kama vile bado wapo kwenye mfumo wa Chama kimoja!

Kama nilivyoeleza mwanzo wa mada yangu nikinukuu maandiko kwenye Biblia kuwa HAKI HULIINUA TAIFA na DHAMBI HULIANGAMIZA TAIFA

Kwa hiyo ningewasihi sana watawala wetu waone umuhimu wa kujenga Taifa lenye kuheshimu Haki, kwani ndiyo njia pekee ya kuliepusha Taifa hili lisiingie kwenye machafuko makubwa ya umwagaji damu
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,130
2,000
..zamani ccm ilikuwa chama cha ukombozi.

..sasa hivi kimekuwa chama cha kidhalimu.

..angalia video kuanzia dakika ya 10:45

 
  • Love
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom