Wakati Bunge la Kenya likipinga Mzigo wa Kodi kwa Wananchi, Bunge letu wanapitisha kwa kishindo

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
2,788
2,000
Binafsi Sijaona kama ni Mzigo wowote kwangu na Kwa mtu yeyote kulipa Tsh 5 katika kila vocha ya 1000 Kama Kodi ili iende kwenye miradi ya maji, barabara,afya n.k

Tunalalamika kupitiliza, tukikuta barabara mbovu malalamiko, changia sh 5 tujenge barabara bado malalamiko eti ni Mzigo.Tulipe Kodi ili tupate haki ya kuilalamikia serikali na kuikosoa.

Sio kwamba tuna umasikini wa hivyo wa kuelemewa na sh 5,10,100 ,ni akili tu za kimaskini.
Kwa wale waliopata kutembelea nchi za huko ulimwengu wa kwanza, watakubaliana na mimi kwamba sisi bado hatulipi Kodi tunafanya mchezo.

Tulipe Kodi Wakuu tuache porojo za kijinga, hii nchi ni yetu itajengwa Kwa jasho letu
Wewe unaona matumizi ya Seriklu ni sawa? The way pesa zinatumika?
 

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,539
2,000
Well said mkuu, sasa tunafanyaje make naona kama tunaangamia
Itabidi vyama vya wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo vikuu, maaskofu, mashehe na asasi za kijamii kupaaza sauti kuhusu hili. Kama sauti zao zitadharauliwa basi itabidi waandae maandamano. Ya nchi nzima na sio Dar peke yake. Watawala wakiona kuna hali hiyo basi watakuwa na busara ya ku"manage the change".

There comes a time when those in power, if wise, realize that it is better for them to manage an outcry from the people, than to allow that outcry to gather steam and sweep them away.
 

Tuamoyo

New Member
Jun 17, 2021
2
20
kwenye huu uzi bado malalamiko ni mengi kuliko ushauri wa nini tufanye au tunachoweza kufanya. Inabidi tuhame kifikra kutoka kwenye malalamiko na manung'uniko twende kwenye kuzungumza na kujadili njia au mbinu zinazoweza kututoa kwenye hali hii. Kama hoja/maoni ya malalamiko na manung'uniko zitakua chache basi hapo naamini mabadiliko ya kweli yatakua magumu.

Hata huko Bungeni kwa mfano kwenye hizo kodi za majengo wabunge karibu wote wamelalamika tu tena nahisi ni kinafki ili raia huku nje tuwaone wanajali lakini sijasikia mbunge aliyekuja na wazo mbadala wa njia nzuri, bora na rahisi ya kukusanya hiyo kodi. Matokeo yake mambo yamepita kama yalivyowasilishwa.

Vuguvugu la kutaka katiba mpya ambalo kadiri siku zinavyosogea linazidi kupata nguvu binafsi naamini naamini ni jambo muhimu sana na la kuungwa mkono na wengi ni kweli katiba mpya pekee haitakuwa mwarobaini wa matatizo yote lakini itakua ni hatua kubwa sana kuelekea mabadiliko ya kweli. Natamani kuona wabunge wawe wa chama tawala au upinzani wanapokua bungeni wakiwa na uhuru kwa asilimia 100% kama walivyo wabunge wa mataifa mengine na sio hii sasa mbunge anakosoa jambo ktk hoja halafu akimaliza anasema anaunga mkono hoja sasa hayo ni maigizo ya aina gani.
 

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,503
2,000
Neno Wanjiku nchini Kenya huwa linatumiwa kumaanisha 'mkenya wa kawaida' almaarufu kama 'common mwananchi', sio mnyonge wala wanyonge. Wanjiku ni mkenya ambaye anaelewa haki zake.

Jina Wanjiku liliibuka wakati wa vuguvugu la kuitisha na kupigania katiba mpya. Ambapo Dikteta Moi aliwabeza wakenya, kwa kusema kwamba mkenya wa kawaida(akimuita Wanjiku kwa dharau) haelewi chochote kuhusu sheria na kwamba hayo masuala yangeachiwa wanasheria. Ila wakenya wakapinga sana wazo hilo, wakijibu kwamba wanaelewa haki zao na mkenya wa kawaida lazima ahusishwe kwenye shughuli ya kuandaa rasimu ya katiba mpya.

Hapo ndipo Wanjiku alipopata ushindi wake wa kwanza. Ambapo ilibidi wajumbe wateuliwe kutoka maeneo yote nchini Kenya na vikundi vyote pia, vya kidini, kibiashara n.k, n.k. Ili Wanjiku aweze kutoa maoni yake na kuhusishwa kwenye shughuli yote ya kuandika katiba mpya, chini ya muongozo wa wataalamu wa sheria.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom