Wakati Bunge la Kenya likipinga Mzigo wa Kodi kwa Wananchi, Bunge letu wanapitisha kwa kishindo

Huku Bunge la Tanzania likitishiwa na Ndugai kwamba wasipo pitisha Bajeti Rais atavunja Bunge, Kwa upande wa Majirani zetu kwao ni tofauti kabisa.

Tanzania Bunge lilihitimisha Mjadala wa bajeti kwa kupitisha kwa kishindo bila hata mabadiliko.

Pamoja na utata wa kodi kama ya majengo kulipwa kwa kutumia LUKU na pia kodi ya simu ila Bunge wamepitisha tena kwa kishindo.

Kenya kwa upande wao Wabunge kwa umoja wao wamepinga bajeti na hivyo kubidi ifanyiwe mabadiliko, hii sio mara ya kwanza kwa wao kupinha Bajeti, ni swala la kawaida kwao.

Bunge la Tanzania ukifuatilia kuaniza Spika yuko pale kuitetea Serikali kwa nguvu zote, Wabunge ukifuatilia wako pale kuitetea Serikali na si kusimamia.

Bunge limejaa wanafikia waganga njaa, wakina Msukuma, watapinga kinafiki siku ya kupitisha Bajeti wanapitisha kwa asilimia zote.

Haingii akilini kwamba Kodi ya nyumba itamuhusu Mwenye nyumba ilihali inajulikana fika kabisa mifumo ya upangaji kwa Tanzania kwamba swala la umeme halimuhusu mwenye nyumba kamwe.

Kwa hio hata Serikali ikoja na Bajeti ya Hovyo kiasi gani itapita tu kwa sababu wabunge wanaogopa Bunge kuvunjwa?

Neno Wanjiku kenya linatumika kama huku neno Wanyonge, wakayi huku tunatumia Wanyonge Kenya huwa wanatumia neno Wanjiku.

View attachment 1827188View attachment 1827189
Bunge la AWAMU YA 5 Tanzania ni la HOVYO KUPATA KUTOKEA
 
Na cha kusikitisha ni kama hatujali kabisa, yaani ni kama hakuna kinacho tuhusu, utaona tunalalamika tukiwa tu kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye Daladala na kadhalika.
Kujali tunajali mkuu lakini sasa tutafanyaje? Waliopo bungeni sio tuliowachagua...!!! Katiba mpya ndo itamaliza huu ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani sasa wabunge watetee vipi tena kupinga bajeti, baada ya Spika kuwaonya wasipopitisha, Rais atalivunja bunge.... wakaona makubwa haya tena, isiwe tabu... hahahahaaaa.... kazi kwelikweli.
Cha ajabu na Spika anasimama anatete kwa nguvu zote Serikali, yaani nilivyo soma somo la CIVICS, ni tofauti na ninacho kiona bungeni.

Bunge limegeuka kuwa taasisi ya kuilinda na kuisifia Serikali.
 
Ungetegemea nini pale kwenye bunge ambalo ni sawa na kamati kuu ya ccm hata kam ingeletwa sheria inatutaka wananchi tulale SAA 1 ungesikia kina msukuma wanaunga mkono hoja tuna chakujifunza hapa
 
Msisahau wabunge wa Kenya wanachaguliwa kwa katiba ya wananchi. Wa kwetu ni tofauti kabisa. Kwa katiba iliyopo tusitarajie bunge litetee wananchi. Katiba yetu siyo ya wananchi. Wananchi wameikataa lakini watawala wanalazimisha ibaki.

Kenya walipokuwa na mchakato wa katiba mpya kuna mahali chama tawala kilikataa vipengele muhimu kwa demokrasia. Kilichotokea ni wanafunzi wa vyuo vikuu kuwasha moto hadi matakwa ya wananchi yakapitishwa. Kwetu wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wa ajabu siku hizi. Hawajali hatima ya taifa, na ni waoga sana. Miaka yangu UDSM tulipinga kwa nguvu wabunge kujipandishia mshahara. Walifukuzwa wanafunzi wote waliokamatwa Manzese (tukielekea mjini). Rais akatangaza tumegomea mpango wa kupeleka wataalamu vijijini.

Kifupi ni hivi: bila katiba inayoruhusu watu kuchagua wabunge wanaowataka na isiyoruhusu serikali kuweka wabunge mfukoni, hakuna maana kuwa na hilo bunge. Ni mirija tu ya unyonyaji isiyo na tija kwa taifa.

Uchu wa madaraka na moyo usioogopa kutumia mabavu kutawala hautaruhusu viongozi wa CCM wakubali katiba ya demokrasia ya kweli, yenye tume huru ya uchaguzi na vyombo huru vya ulinzi na usalama, bila kulazimishwa. Wanaoweza kuwalazimisha ni muungano wa wafanyakazi na wanafunzi. Wakiendelea hawa kufyata mkia basi tutaendelea kunyonywa na kudharauliwa na chama tawala kwa muda mrefu kiasi watakachoweza.

Viongozi wa CCM wanajua sio haki kutokuwa na tume huru ya uchaguzi. Mkapa ameandika hivyo kwenye kitabu chake. Tatizo ni kwamba sio rahisi kuachia madaraka. The spirit is willing but the body is weak.

Newton's First Law of Motion states that bodies tend to stay in their state of rest or of uniform motion in a straight line until they are acted upon by external forces. Tusitegemee watawala wa CCM wabadilike bila external pressure.

There are no free lunches. If we want democracy then we must sweat for it.
 
Kujali tunajali mkuu lakini sasa tutafanyaje? Waliopo bungeni sio tuliowachagua...!!! Katiba mpya ndo itamaliza huu ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanaenda na matukio bila kujua chanzo cha matatizo watanzania tunafeli sana uwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo

ccm inapswa kuondolewa kwanguvu za umma tunapaswa kuwaondoa kwakuwatimua na mawe kila kona kila mtu kilasehemu ya nchi ndani ya masaa machache tunaondoa shinda ni uelewa wa watanzania

Utamshawishi vipi MTU kulipa Kodi Wakati ripoti za CAG zikipelekwa Bungeni zinakuta ubadhirifu wa Mali za mlipa Kodi na hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa kulingana na makosa

ccm wanaendelea kutualibia nchi yetu makusudi wanatuchukulia kama ndondocha lakini tukiamka nao kila mtu akabemba kisado cha mawe saa nne asubuhi mbali sana
 
Msisahau wabunge wa Kenya wanachaguliwa kwa katiba ya wananchi. Wa kwetu ni tofauti kabisa. Kwa katiba iliyopo tusitarajie bunge litetee wananchi. Katiba yetu siyo ya wananchi. Wananchi wameikataa lakini watawala wanalazimisha ibaki.

Kenya walipokuwa na mchakato wa katiba mpya kuna mahali chama tawala kilikataa vipengele muhimu kwa demokrasia. Kilichotokea ni wanafunzi wa vyuo vikuu kuwasha moto hadi matakwa ya wananchi yakapitishwa. Kwetu wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wa ajabu siku hizi. Hawajali hatima ya taifa, na ni waoga sana. Miaka yangu UDSM tulipinga kwa nguvu wabunge kujipandishia mshahara. Walifukuzwa wanafunzi wote waliokamatwa Manzese (tukielekea mjini). Rais akatangaza tumegomea mpango wa kupeleka wataalamu vijijini.

Kifupi ni hivi: bila katiba inayoruhusu watu kuchagua wabunge wanaowataka na isiyoruhusu serikali kuweka wabunge mfukoni, hakuna maana kuwa na hilo bunge. Ni mirija tu ya unyonyaji isiyo na tija kwa taifa.

Uchu wa madaraka na moyo usioogopa kutumia mabavu kutawala hautaruhusu viongozi wa CCM wakubali katiba ya demokrasia ya kweli, yenye tume huru ya uchaguzi na vyombo huru vya ulinzi na usalama, bila kulazimishwa. Wanaoweza kuwalazimisha ni muungano wa wafanyakazi na wanafunzi. Wakiendelea hawa kufyata mkia basi tutaendelea kunyonywa na kudharauliwa na chama tawala kwa muda mrefu kiasi watakachoweza.

Viongozi wa CCM wanajua sio haki kutokuwa na tume huru ya uchaguzi. Mkapa ameandika hivyo kwenye kitabu chake. Tatizo ni kwamba sio rahisi kuachia madaraka. The spirit is willing but the body is weak.

Newton's First Law of Motion states that bodies tend to stay in their state of rest or of uniform motion in a straight line until they are acted upon by external forces. Tusitegemee watawala wa CCM wabadilike bila external pressure.

There are no free lunches. If we want democracy then we must sweat for it.
Well said mkuu, sasa tunafanyaje make naona kama tunaangamia
 
Kwasababu wanajua wakipitisha watakiona cha moto,!

Unakumbuka raia waliwahi kupeleka nguruwe bungeni,

Sisi hapa tuko busy kusain petition ya kumtoa diamond BET!

Angalia toka juzi hapa jf nyuzi za majungu kwa wateuliwa wa Samia zilikuwa zinamiminika kila baada ya dk 3

Wakati hiyo kodi inatangazwa uzi wake ulikuwa una coments 94 huku ule wa Sabaya ukiwa na coments 1000+
Watu wakishangilia kwamba mama kawapa zawadi.

Nashauri kodi iongozwe mara 10 zaidi ili kuwakomoa mataga.
Chief , ongezeko la kodi haliwaathiri mataga pekee ni Watanzania wote..

Hata hivo nakubaliana nawe hii kodi ni kidogo sana inapaswa iongezwe mara mia....pengine tunaweza kupata akili ya kuwakemea hawa viongozi wetu uchwara
 
Wewe unaejielewa unataka pesa za kugharamia miradi na huduma zitoke wapi?

Kama ni kupunguza matumizi yasiyo na tija hiyo haiondoi kwamba kodi lazima ilipwe
Tatizo ni hivi ccm ni wezi kama wameweza kuiba Kura nchi mzima washindwaje kuiba Kodi nani mjinga akalipekodi kwa serekali iliyojiweka yenyewenye madarakani?
 
Sasa hizo habari zikapambaniwe kwenye uwanja husika ila kodi lazima ulipe ,usipolipa utashughulikiwa.

Binafsi siko tayari kutoa pesa yangu kwa muuzaji asinipe lisiti kwa sababu siwezi mfaidisha mtu jasho langu
 
Binafsi Sijaona kama ni Mzigo wowote kwangu na Kwa mtu yeyote kulipa Tsh 5 katika kila vocha ya 1000 Kama Kodi ili iende kwenye miradi ya maji, barabara,afya n.k

Tunalalamika kupitiliza, tukikuta barabara mbovu malalamiko, changia sh 5 tujenge barabara bado malalamiko eti ni Mzigo.Tulipe Kodi ili tupate haki ya kuilalamikia serikali na kuikosoa.

Sio kwamba tuna umasikini wa hivyo wa kuelemewa na sh 5,10,100 ,ni akili tu za kimaskini.
Kwa wale waliopata kutembelea nchi za huko ulimwengu wa kwanza, watakubaliana na mimi kwamba sisi bado hatulipi Kodi tunafanya mchezo.

Tulipe Kodi Wakuu tuache porojo za kijinga, hii nchi ni yetu itajengwa Kwa jasho letu
 
Receipt hata ukipewa na muuzaji pesa yako itapigwa tu, ccm ni wezi sana wana matumizi ya kijinga sana.

Ngoja wazikusanye wataanza kununua wapinza, kuna wabunge wanalipwa pesa yako hiyo bila hata kuwa na vyama vya siasi

Dhana ya kupoteza pesa kwako nini umeambiwa nikutokuchukua receipt uzalendo wa kuomba receipt unaupata wapi?

Mimi nikinunua bidhaa za 5m namwambia muuzaji andika receipt ya jero sipangiwi na mtu
 
Binafsi Sijaona kama ni Mzigo wowote kwangu na Kwa mtu yeyote kulipa Tsh 5 katika kila vocha ya 1000 Kama Kodi ili iende kwenye miradi ya maji, barabara,afya n.k

Tunalalamika kupitiliza, tukikuta barabara mbovu malalamiko, changia sh 5 tujenge barabara bado malalamiko eti ni Mzigo.Tulipe Kodi ili tupate haki ya kuilalamikia serikali na kuikosoa.

Sio kwamba tuna umasikini wa hivyo wa kuelemewa na sh 5,10,100 ,ni akili tu za kimaskini.
Kwa wale waliopata kutembelea nchi za huko ulimwengu wa kwanza, watakubaliana na mimi kwamba sisi bado hatulipi Kodi tunafanya mchezo.

Tulipe Kodi Wakuu tuache porojo za kijinga, hii nchi ni yetu itajengwa Kwa jasho letu
Tulipe kondi ngapi?
 
Huku Bunge la Tanzania likitishiwa na Ndugai kwamba wasipo pitisha Bajeti Rais atavunja Bunge, Kwa upande wa Majirani zetu kwao ni tofauti kabisa.

Tanzania Bunge lilihitimisha Mjadala wa bajeti kwa kupitisha kwa kishindo bila hata mabadiliko.

Pamoja na utata wa kodi kama ya majengo kulipwa kwa kutumia LUKU na pia kodi ya simu ila Bunge wamepitisha tena kwa kishindo.

Kenya kwa upande wao Wabunge kwa umoja wao wamepinga bajeti na hivyo kubidi ifanyiwe mabadiliko, hii sio mara ya kwanza kwa wao kupinha Bajeti, ni swala la kawaida kwao.

Bunge la Tanzania ukifuatilia kuaniza Spika yuko pale kuitetea Serikali kwa nguvu zote, Wabunge ukifuatilia wako pale kuitetea Serikali na si kusimamia.

Bunge limejaa wanafikia waganga njaa, wakina Msukuma, watapinga kinafiki siku ya kupitisha Bajeti wanapitisha kwa asilimia zote.

Haingii akilini kwamba Kodi ya nyumba itamuhusu Mwenye nyumba ilihali inajulikana fika kabisa mifumo ya upangaji kwa Tanzania kwamba swala la umeme halimuhusu mwenye nyumba kamwe.

Kwa hio hata Serikali ikoja na Bajeti ya Hovyo kiasi gani itapita tu kwa sababu wabunge wanaogopa Bunge kuvunjwa?

Neno Wanjiku kenya linatumika kama huku neno Wanyonge, wakayi huku tunatumia Wanyonge Kenya huwa wanatumia neno Wanjiku.

View attachment 1827188View attachment 1827189
matatizo ya kenya ni tofauti na matatizo ya tz kwahiyo kila nchi inamaamuzi yake haya ndiyo yetu yale ni ya kwao
 
Back
Top Bottom