Wakati bunge la bajeti lilielekea ukingoni, hakuna wizara iliyoleta bajeti ya kimabadiliko,yaleyale

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Tuliahidiwa makubwa wakati wa kampeni,lakini ili yatekelezwe lazima pesa ziwepo na zinatengwa na wizara kupitia bunge,mpaka sasa hakuna wizara iliyowasilisha bajeti ya kimapinduzi itayoonyesha tofauti ya utawala mmoja na mwingine

Wizara ya viwanda haina hata moja la kushikika la kuifanya Tanzania iwe ya viwanda....porojo nyingi tu

Wizara ya Kilimo haina ajenda hata moja iliyoitoa kumkomboa mkulima au kuweka link ya Kilimo na viwanda, Tanzania ya viwanda itabaki ndotoni

Wizara ya vijana pia yaleyale,ukimuuuliza kijana kuhusu hotuba ya waziri nape, hakuna hata kijana mmoja anayejua...hakuna ajenda ya ajira kwa vijana wala kuwakomboa na umasikini

Hili pia liko wizara ya afya

Kwa ujumla mambo ni yaleyale kama enzi zile za kale,kutuimbia maneno meeengi kwenye bajeti lakini hayana ubunifu wa kuisogeza nchi mbele,nawahakikishia Tanzania kupiga hatua itakuwa ndoto na inawezekana mpaka 2020 Yukawa tumerudi nyuma zaidi
 
Back
Top Bottom