Wakati Afrika inajikwamua kiuchumi, Marekani “inavunja ngazi” na China “inajenga ngazi”

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
641.png

Hivi karibuni, hotuba iliyotolewa kwa njia ya video na mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo Endelevu cha Chuo Kikuu cha Columbia, Marekani Jeffrey Sachs ilifuatiliwa na kuitikiwa sana na watu wa Afrika. Kwenye mkutano huu wa Umoja wa Mataifa, profesa huyu alitoa mfano wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo DRC akisema watu wengi wanazikosoa nchi maskini “Lipi limewatokea? Mbona hamwezi kujisimamia vizuri”, lakini hawafikirii ni kwa nini nchi hizo zinashindwa kuondokana na umaskini.

Mchumi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza Ha-Joon Chang amesema kwenye kitabu cha “Mtego wa Nchi Tajiri: Kwa Nini Nchi Zilizoendelea Zinavunja Ngazi?” kuwa Marekani na nchi nyingine tajiri zimemaliza malimbikizo ya awali kupitia uporaji wa kikoloni na kuchimba madini ovyo, na sasa zinavunja “ngazi” iliyowafikisha kileleni na kutumia umwamba wao kiuchumi kuzilazimisha nchi zinazoendelea zikiwemo za Afrika kutekeleza “sera nzuri” kama vile kufungua soko na ushindani wa haki, lakini uhalisia ni “mtego wa kuvunja ngazi” unaokwamisha maendeleo ya nchi hizo.

Tofauti na nchi zilizoendelea kuvunja kwa makusudi “ngazi ya maendeleo” ya nchi za Afrika, China siku zote inazichukulia nchi zinazoendelea kama wenzi muhimu wa ushirikiano. Katika mwaka mmoja uliopita, China inaunga mkono juhudi za nchi za Afrika kupambana na ugonjwa wa COVID-19 na kufufua uchumi ili kulinda haki ya maisha, afya na maendeleo ya watu wa Afrika.

Janga la COVID-19 ni kama mtihani. Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC huko Dakar, Senegal, nchi kadhaa za kusini mwa Afrika ziliripoti maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Corona- Omicron. Hata hivyo China iliamua kufuata ahadi yake kuhusu mkutano huo na kutangaza mpango wa kutoa msaada wa chanjo dhidi ya virusi hivyo ambao ni mkubwa zaidi kuahidiwa na nchi moja tangu kutokea kwa janga hilo. Wakati China ilipotangaza “kutoa chanjo nyingine bilioni 1 kwa nchi za Afrika zikiwemo milioni 600 kama msaada”, kelele za kushangilia zilisikika ukumbini. Kwani kwa Afrika iliyo nyuma duniani kwa asilimia tano tu ya utoaji chanjo, ahadi hiyo ni kama “mvua iliyokuja kwa wakati”.

Kwa upande wa Marekani, mapema mwezi Disemba Wizara ya Mambo ya Nje ilitangaza kuwa “ilikuwa imetoa dozi milioni 94 za chanjo kwa Afrika”. Inaonekana ni ukarimu, lakini hali halisi ni kuwa chanjo iliyohodhiwa na serikali ya Marekani inawatosheleza watu milioni 750, lakini Marekani ina watu milioni 330 tu. Chanjo hiyo ni kitu adimu barani Afrika, lakini inasubiri kupita muda wake katika maghala ya Marekani. Hata gazeti la The New York Times lilitoa makala likisema, “Marekani na nchi nyingine tajiri zinakabiliwa na changamoto kubwa ya kimaadili.”

Kwenye mkutano huo wa FOCAC wa Dakar, China pia ilitangaza kuwa ukiwa mpango wa kwanza wa miaka mitatu wa “Dira ya Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2035”, China na Afrika zitatekeleza kwa pamoja “miradi tisa”. Kutoka “mipango 10 ya ushirikiano”, “hatua 8 za utekelezaji” hadi “miradi tisa”, mkutano wa FOCAC unaofanyika kila baada ya miaka mitatu huwa unatangaza waraka wa ushirikiano wenye vipimo. Katika miaka mitatu iliyopita, miradi mbalimbali ya ushirikiano imezaa matunda na kwamba warsha 11 za Luban (vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi) zimezinduliwa, awamu mbili za maonesho ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yalifanyika, hospitali ya mama na watoto ya Senegal na jengo la magonjwa ya kuambukiza la hospitali ya taifa ya Mauritius lililojengwa kwa msaada wa China lilikabidhiwa, na mradi wa kuzalisha umeme kwa maji wa Souapiti, Guinea na reli kati ya Lagos na Ibadan nchini Nigeria umekamilika.

Lakini kutoka pendekezo la “Power Africa” la Barack Obama, pendekezo la “Kustawisha Afrika” la Donald Trump hadi pendekezo la “Kujenga Dunia Bora” au B3W, mapendekezo yaliyotolewa na Marekani hayakosekani, lakini tatizo ni kutotekelezwa. Kwa mfano wa pendekezo la “Power Africa” lililotolewa na rais wa zamani Barack Obama alipofanya ziara barani Afrika mwaka 2013, mpango huo uliahidi kusaidia kuzalisha umeme wa megawati elfu 20 hadi mwaka 2020 na kufikisha umeme kwenye familia milioni 50. Lakini hadi mwishoni mwa mwaka 2020, umeme uliozalishwa kupitia mpango huo ni megawati 4194 tu, kiasi ambacho hakikufikia hata robo ya ahadi.

Wachina husema kura ya China kwenye Umoja wa Mataifa daima inapigwa kwa ajili ya nchi zinazoendelea. Lakini Marekani huwa inazinyooshea kidole nchi za Afrika. Hivi karibuni, mgogoro wa kisiasa umetokea Ethiopia, na serikali ya Marekani ilisema “itaandika dawa” ya kushughulikia msukosuko wa kidemokrasia, jambo ambalo limeikasirisha kabisa Afrika. Wanamitandao wengi wamezindua kampeni kubwa ya “NoMore” chini na juu ya mtandao wa internet, wakiitaka Marekani “isiingilie tena” mambo ya ndani ya Afrika, “isifanye tena” ukoloni mambo leo na “isifanye njama tena” barani Afrika.

Watu wanauliza, China na Afrika ziko mbali sana na zina tamaduni tofauti, lakini kwa nini zimekuwa marafiki wakubwa? Sababu ni rahisi: kwani uhusiano kati ya China na Afrika ni kuungana mikono kati ya nchi zinazoendelea, ni kusaidiana kati ya ndugu. Lakini Marekani nayo moyoni mwake kuna sumu iliyobakia ya ubeberu, ukoloni na ubaguzi wa rangi, na kutoka kichwani hadi mguuni, nchi hiyo imeonesha tabia za “kujigamba, na kuogopa wenye nguvu na kudhalilisha wanyonge”. Mwenzi kama huyu si wa kutegemeka na pia unahitaji kuwa macho ili asije akakushambulia kutoka nyuma.
 
Umasikini ndiyo unazidi kuongezeka, tumetoka kwenye milo miwili kwa siku sasa tuko kwenye mlo mmoja kwa siku kama utapatikana!
 
Back
Top Bottom