Wakataliwa maombi ya kuhesabu watu (Sensa) kwa kukosa kadi ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakataliwa maombi ya kuhesabu watu (Sensa) kwa kukosa kadi ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JF2050, Aug 1, 2012.

 1. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Akizungumza nami kwa hisia kali, kijana mmoja ambaye hakunitajia jina lake jana tarehe 31 July 2012 mbele ya Uhamiaji House maeneo ya Kurasini, amesema kwamba alihuzunika na kusikitika mno baada ya maombi yao ya kuomba kazi ya kuhesabu watu, yaani sensa, kukataliwa na Afisa Mtendaji wa mtaa mmoja wa mkoa wa Temeke.

  "Tulifika hapo asubuhi na mapema ofisi ikiwa bado haijafunguliwa, baada ya mtendaji kuja alianza kumwambia kila mmoja wetu taratibu kama huna kadi ya CCM anza tu kuondoka", alisema kijana huyo.

  Aliendelea kueleza kwamba alipouliza kwa nini awe na kadi ya uanachama wa CCM, aliambiwa kuwa kwenye fomu ya mwombaji imeandikwa kuwa mwombaji atatakiwa kutii na kufuata maelekezo yote ikiwa ni pamoja na kuwa na kadi ya chama hicho.  Source: Simplicity.
   
 2. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Sina imani na taarifa yako kama ni ya kweli nahisi umejisikia tu kubuni uongo ili tukusome humu JF
   
 3. KML

  KML JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mmmmmh.....
  napita
   
 4. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwani hapo nimeandika alisema hadharani!
   
 5. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  with ccm,ninaamini inawezekana.
   
 7. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wanaendelea kujimaliza,unategemea huyo kijana ataipenda ccm?
   
 8. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sensa, Vitambulisho vya uraia na daftari la wapiga kura vitatumika kimkakati kulazimisha ushindi wa ccm 2015. Wako katika mpango wa kuchakachua daftari la wapiga kura na kutumia takwimu feki za sensa na vitambulisho vinavyogawiwa kimkakati kuhalalisha huo uchakachuaji. Umesikia wapi wakimbizi wanapewa vitambulisho vya uraia? Wageni wengi sana wana vitambulisho vya kupigia kura, ulikuwa huhitaji proof yoyote ya kuwa Mtanzania kupata kitambulisho cha kupigia kura. Sasa kitambulisho hichohicho unaweza kukitumia kupata Kitambulisho cha uraia. Lazima wachakachue kwenye sensa ili wapate uhalali wa idadi ya kura zao za kugushi.
   
 9. b

  baba gaston Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It is difficult to believe that!!!!!!!!!
   
Loading...