Wakandarasi wababaishaji sitaki -Kikwete

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Inaelekea mkuu wa nchi haelewi njia za kukuza viwango vya makandarasi wetu.
Kama miradi karibu yote wanapewa wageni kwa asilimia 100, je hawa wa kwetu watajifunza vipi? Hakuna technology transfer na hilo ndilo tatizo mojawapo kubwa kwa TZ. Matokeo yake miaka 100 ijayo bado tutaendelea kutegemea wageni kwenye miradi yetu mbalimbali.

Wakandarasi wababaishaji sitaki -Kikwete

2008-05-04 10:45:16
Na Lucy Lyatuu, Singida

Rais Jakaya Kikwete `ameicharukia` Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini TANROADS kutowapa kazi wakandarasi wababaishaji, pia kutowalipa wanaojenga barabara chini ya viwango.

``Wakandarasi wababaishaji wasipewe kazi, wanatufikisha pabaya,`` alisema.

Aidha, aliwataka wizara ya ujenzi wanapotoa tenda wamchague yule aliyetoa hesabu kubwa na sio kuangalia mwenye hesabu ndogo kwani wao pia ukubwa wa kazi wanaijua.

``Hakuna sababu wizara, TANROADS kumchagua mtu mwenye hesabu ndogo, mnapotangaza tenda lazima kuangalia kama kazi ataiweza, ingawa wale watakaokosa watasema mnajali mafisadi,... hayo msiyajali?,`` alishauri.

Aidha, amesema yapo makampuni kadhaa hapa nchini ambayo kazi yao ni kudanganya pindi wanapokuwa wamepewa tenda za kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati akizindua barabara ya Isuna hadi Manyoni yenye urefu wa kilomita 55 baada ya mkandarasi aliyepewa kazi ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kushindwa kazi kwa visingizio.

Rais Kikwete yuko mkoani humu kwa ziara ya siku sita kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka 2005.

Rais Kikwete alisema awali barabara hiyo ya Isuna-Manyoni, ilikuwa ikijengwa na mkandarasi kutoka China ambaye alishindwa kukamilisha kazi kama ilivyotakiwa.

Alisema kilichotokea hapo iwe ni fundisho na kwamba tatizo la namna hiyo lisijitokeze tena.

Aidha Rais Kikwete alibainisha kuwa kupewa tenda kwa mkandarasi mwenye hesabu ndogo ndiko kunakosababisha matatizo ikiwa ni pamoja na miradi kutokamilika kwa wakati uliotakiwa.

Alisema wakiendelea na utaratibu huo wa kuangalia hesabu ndogo watakwama wakati nchi bado ni maskini.

``Ninaomba sana, bure ni ghali sana, kwani angalia sasa tunaingia gharama nyingine tena kubwa zaidi kuliko zile za awali,`` alisema.

Aliongeza kuwa mzabuni atakayekiuka utaratibu unaotakiwa wanapaswa kumuita na kumuuliza ili wasimamie katika ukweli na haki na sio kuwachanganya.

Kuhusu makampuni yanayodanganya alisema hapa nchini yapo kadhaa na kazi yao ndio hiyo halafu badaye huhitaji majadiliano.

``Simamieni wataalamu mlio nao, makampuni yawe yanasema ukweli kuepusha hasara katika nchi,`` alisema.

``Nchi hii ni maskini, ujenzi huu unagharamiwa na fedha za wananchi, epukeni kuingia gharama mara mbili, kwani wanaofanya hivyo wanakuwa wanyonya damu,`` alisema.

Pia aliwataka kukasirika na kuwachukulia hatua makampuni yanayokiuka utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwaambia kwa herini (byebye) wakatafute tenda nyingine nje ya nchi.

Rais aliongeza kuwa mhandisi mshauri naye hatakiwi kulipwa malipo yake endapo ujenzi hautakuwa umekamilika kwa kiwango kinachotakiwa kwani wasipofanya hivyo Tanzania itakuwa shamba la wajinga.

Lazima Watanzania waone uchungu na kutekeleza miradi ya wananchi katika kiwango kinachotakiwa, alisisitiza.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Bw. Omar Chambo alisema barabara hiyo itagharimu kiasi cha Sh. bilioni 30.43 na ujenzi wake ulisainiwa Desemba 11, mwaka 2007.

Alisema barabara hiyo ilisainiwa kati ya TANROADS na Kampuni ya China Geo Engineering kutoka nchini China na kwamba sehemu ya barabara hiyo inatarajiwa kukamilia ifikapo mwaka 2010.

Alisema mradi huo unasimamiwa na mhandisi mshauri Black &Veatch kutoka Afrika Kusini akishirikiana na Kampuni ya Mak Consult ya Tanzania kwa gharama ya Sh. milioni 857.23
 
JK hutaki unafanya nini sasa? Siasa kwenye kazi hatutaki. Tunataka maendelo na kama hutaki sema kwa vitendo, si uliambiwa Richmond ilipatikana vipi? akina EL siwamewajibika. Mwanyik, Mrindiko na yule jamaa wa PCCB umewafanya nini mpaka kwenye uhandisi tuamini hutaki? Hujui kama kusema sio kutenda? hujui kutenda sio kuamini? Hujui kama ukiamini itadumu milele?
 
Si JK alisema wameichukua Richmond kwa sababu ya urahisi wa bei? anataka kusema nini?
 
mkuu katoa maagizo sasa watendaji wamepewa meno wakishindwa kutafuna hiyari yao.

ukipigao ndio ukufunzao
 
JK bwana . Anaongea weeeeeeeeeee mbona hafani matendo ? Anzia nyuma mkuu wa kaya JK .Haya ya sasa unatuzuga tu mkuu tunakujua .
 
Aidha Rais Kikwete alibainisha kuwa kupewa tenda kwa mkandarasi mwenye hesabu ndogo ndiko kunakosababisha matatizo ikiwa ni pamoja na miradi kutokamilika kwa wakati uliotakiwa.

Alisema wakiendelea na utaratibu huo wa kuangalia hesabu ndogo watakwama wakati nchi bado ni maskini.

``Ninaomba sana, bure ni ghali sana, kwani angalia sasa tunaingia gharama nyingine tena kubwa zaidi kuliko zile za awali,`` alisema.

Aliongeza kuwa mzabuni atakayekiuka utaratibu unaotakiwa wanapaswa kumuita na kumuuliza ili wasimamie katika ukweli na haki na sio kuwachanganya.

Hapa JK ameongea jambo la msingi sana,serikali isipokuwa makini katika shughuli nzima ya kandarasi italeta hasara, kwa hivyo tuiunge mkono kauli/agizo lake huku tukimtaka alitekeleze kwa vitendo,
agizo zuri nalo ni muhimu jamani
 
``Wakandarasi wababaishaji wasipewe kazi, wanatufikisha pabaya,`` alisema.

Aaahahh! Muungwana bwana saa ingine sijui anakuwaje, sasa hawa Ujenzi tabia ya ubabaishaji wameiiga kutoka wapi kama sio kwenye utawala wake?

Yaaani kweli talking about ubabaishaji Tanzania , unaanzia Ujenzi au CCM na serikali kwa ujumla?
 
Kila mara mimi huwa nasema ES ukiwa na point sitasita kukuunga mkono kama vile ambavyo sitasita kuiunga serikali ya JK mkono kaa itafanya jambo la maana .Maneno yako yanatosha FMES.
 
Kusema sio kazi, kazi iko kwenye utendaji.

Maisha Bora kwa kila Mtanzania yanawezekana kama Ufisadi ukitokomezwa!
 
Wakuu hapo naomba nipingane na sababu zilizotolewa kwamba eti ni bei inasababisha yote haya.... Jamani kwa wale tunaofahamu mambo ya procurement of these jobs ni kwamba kabala hujajua jamaa ni cheap au expensive lazima uwe ushampitisha kuwa yeye ni mzuri... Sasa hili la bei rahisi na kazi mbovu ina maana:
1. Wanafungua tender documents kiholela - Kimsingi/kiutaratibu ni kwamba kwanza unafungua "Technical Proposal" then unafungua "Financial Proposals" only from qualified only those technically qualified firms!! Sasa kama mmeangalia mkaona jamaa ni mbangaizaji who open his financial??

2. Our Technical requirements set forth in our bids are very poor kiasi kwamba hata mimi Maasai nisiyekuwa na ujuzi wala pesa for that case ninaweza kuwa qualified.....

3. Hawa wakuu wanajua kipengele kinaitwa "Liquidated Damages" amabcho kinaendana sambamba na "Out put/stage based payment based on certificate/inspection" ambapo kuna minimum na mazimum payments za kumlipa kandarasi kwa kuzingatia muda, production and bila kusahau kuwa kuna "Performance Bond"??

Sasa wakuu ili niweze kuwakubalia hao jamaa kuwa kuchagua rahisi ndio expensive lazima wanihakikishie kuwa hayo mawili hapo juu sio ndio wachawi wetu kwenye sekta hii... Wao lazima wakubali kuwa wao wenyewe ndio tatizo sio hata yule kandarasi aliyeshindwa kazi sababu walipmitisha kuwa technically - Manpower, equipments, materials source, technical capacity, time schedule etc were all complient to technical requirement!!!!!

Jamani tutaendelea kuwasikiliza hawa jamaa na vijisababu vyao uchwara mpaka lini?? Mbaya zaidi ni pale amabapo wameshamdanganya hata Rais kuwa eti ni kutaka cheap ndipo kumetuponza wakati we all know kuwa kama sio 10% then ni kutokujua kabisa??

Naomba kuwakilisha!!!
 
Rais Jakaya Kikwete `ameicharukia` Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini TANROADS kutowapa kazi wakandarasi wababaishaji, pia kutowalipa wanaojenga barabara chini ya viwango.
Charity begins at home wazungu wanasema, watu wanaojulikana kuwa wababaishaji muheshimiwa ndio anawapa uwaziri, na ingekuwa vyema basi ,if he really mean what he is saying, hata mawaziri wenye poor performance wasilipwe! Mikwala kama hii isiishie barabarani tu.
 
Well maneno mazuri toka kwa Mkuu............i.e. support

1. Ni kweli Mkandarasi anaposhindwa na kuachishwa.....posibility ya mkandarasi anayekuja atawapiga bei DUBLE!!

2.......wapi PERFORMANCE BOND?

3. Mpendekezo ya Evaluation team inabidi kuchunguzwa.

4. Wakandarasi kama hawa walioshindwa inabidi wawe blacklisted.

......Wakuu....hivi ile barabara iliyokuwa ikijengwa na Konoike toka Dodoma mpaka Manyoni ilishaisha successfully?
 
Halafu haya mambo ya Rais kusema Tanzania ni nchi maskini sikubaliani nayo kabisa. Rais aseme Tanzania ni nchi tajiri kwa rehema ya mungu, lakini inaibiwa na kufisadiwa mpaka inabaki bila hela zozote za kuendeleza nchi.

Halafu Rais kuongea mambo bila kufikiri ndio mwanzo wa matatizo. Sidhani kama kusema bei kubwa ndio zipewe itasaidia, kwani hapa itaongeza ufisadi. Yaani kwa maoni yangu angesema Zabuni zipewe kwa watu wenye tender zilizokuwa sahii na zenye kukidhi mahitaji, halafu ndio mambo ya gharama yazungumziwe.

Sasa hapa Tanroards, wakijua gharama 1 billion, si kiasi cha kumwambia mtoa tender oya, rais kasema gharama sio issue wewe weka bilion 5 tutakulipa.
 
Well maneno mazuri toka kwa Mkuu............i.e. support

1. Ni kweli Mkandarasi anaposhindwa na kuachishwa.....posibility ya mkandarasi anayekuja atawapiga bei DUBLE!!

2.......wapi PERFORMANCE BOND?

3. Mpendekezo ya Evaluation team inabidi kuchunguzwa.

4. Wakandarasi kama hawa walioshindwa inabidi wawe blacklisted.

......Wakuu....hivi ile barabara iliyokuwa ikijengwa na Konoike toka Dodoma mpaka Manyoni ilishaisha successfully?

Mkuu Ogah, Tupo pamoja mkuu lakini blacklisting does not exits in our vocabulary.... Pia mambo ya technical advises hayafuatwi kabisaaaaa..... To sum up and support my points hapa ni mfano wa tender moja ambayo ndio imechunguzwa kikamilifu RICHMOND....... Ile uchunguzi ilifanywa kwa Richmond ikifanyika kwa roads nk basi Mkuu sidhani kama kuna watu wataweza kuangaliwa machoni manake ni uchafu mtupu.....
 
Hapa JK ameongea jambo la msingi sana,serikali isipokuwa makini katika shughuli nzima ya kandarasi italeta hasara, kwa hivyo tuiunge mkono kauli/agizo lake huku tukimtaka alitekeleze kwa vitendo,
agizo zuri nalo ni muhimu jamani

Gamba la Nyoka,

Alichoongea JK ni sahihi ila tu kwa kiongozi wa nchi lazima aangalie pia kwanini hao wakandarasi wanakuwa wababaishaji?

Tatizo letu lilianza nyuma kabisa, tulipoamua kwamba MECCO hawawezi kazi na kuanza kuwapatia KAJIMA na wengine.

Hilo lilikuwa sawa lakini sambamba na hilo ilitakiwa kuwe na kipengere kinachoyalazimisha makampuni kama KAJIMA ili kufanya ubia na makampuni ya Kitanzania kwa lengo la Watanzania kujifunza (technology transfer).

Bahati mbaya hatukufanya hivyo, makampuni ya Tanzania kwa muda mrefu yamekuwa yakihusika na projects njiwa na wenyewe kulazimika kufanya kazi kiubabaishaji.

Nchi haiwezi kuendelea kwa kutegemea wageni kwa kila kitu. Ndio maana hata juice tunaagiziwa toka nje ya nchi.

Mimi naamini quality ni muhimu mno kwenye projects zote lakini pia lazima kuwe na jitihada ya wazi kuwasaidia Wakandarasi wadogo wadogo ili wapate uwezo na baadaye waweze kujitegemea.

Kadri nchi itakavyokuwa na Wakandarasi wengi wenye uwezo basi hata ushindani utakuwa mkubwa, ubora utaongezeka na bei kupungua.

Ni rahisi kuwasema baadhi ya Wakandarasi wetu wababaishaji, lakini pia serikali ina wajibu wa kuwa na sera za kuwasaidia Wakandarasi na makundi mengine ya Wazawa ili waweze kupata capacity (hasa technology) ya kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Vinginevyo Watanzania tutaishia kuwa vibarua tu wa makampuni ya nje.
 
Aaahahh! Muungwana bwana saa ingine sijui anakuwaje, sasa hawa Ujenzi tabia ya ubabaishaji wameiiga kutoka wapi kama sio kwenye utawala wake?

Yaaani kweli talking about ubabaishaji Tanzania , unaanzia Ujenzi au CCM na serikali kwa ujumla?

Hata wale walioifisadi Tanzania walialikwa kwenye kikao kule Butiama na wengine bado wanapeta kama wabunge na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM au kamati kuu. Maneno mengiiiii, utekelezaji ZERO! Yeye mwenyewe mbabaishaji lakini halioni hilo, acha usanii JK!
 
Mh Rais bana!Kwani hao makandarasi wanapewa tenda na kina nani?
Tunataka sasa tuone heading kama hii;
Re:Viongozi Mafisadi sitaki-Kikwete
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom