Wakamatwa na bunduki iliyofungwa shanga

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAKAZI watatu wa Kijiji cha Mwamlela wilayani Uyui mkoani Tabora, wamekamatwa wakiwa na bunduki iliyofungwa shanga inayosadikiwa ilikuwa ikitumika katika uhalifu wenye kuhusisha ushirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow amesema, watu hao ni sehemu ya watu 16 waliokamatwa katika matukio tofauti katika msako maalumu wa wahalifu uliofanyika.

Amewataja waliokamatwa kutokana na tuhuma hizo ni Lucas Charles (28), Mihambo Mishinyari (34) na Waziri Sukwa (37) ambao ni wakazi wa Kijiji cha Mwamlela, Kata ya Tura wilayani Uyui .

Amesema, watu hao pia walikutwa na ngozi za wanyama aina ya tandala na swala pala wakizimiliki kinyume cha sheria.

Amesema, ngozi hizo zilionesha kwamba wanyama hao walishambuliwa kwa risasi.

Wengine wawili waliokamatwa katika msako huo ni wakazi wa wilayani Nzega, ambao walikutwa wakiwa na silaha aina ya Shot gun iliyokatwa kitako na kubakia na mtambo wa kupakia na kulipua risasi.

Watuhumiwa hao ni Nyanzobe Mbege (28) na Shaaban Salum (37) walikutwa pia na risasi saba za bunduki hiyo yenye mitutu miwili.
 
Zipo nygi hizi huko mipaka ya tz na congo wanabadlishanaga na bidhaa,usishangae sana
 
Back
Top Bottom