Wakamatwa kwa vurugu za kidini Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakamatwa kwa vurugu za kidini Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Oct 17, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Maandamano ya kidini Tanzania

  Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 126 baada ya mashambulizi ya wiki jana dhidi ya makanisa mjini Dar es Salaam kwa mujibu wa kamanda wa polisi. Waisilamu waliokuwa wameghadhabishwa walivunja na kuharibu makanisa matano baada ya kijana mmoja kuripotiwa kuikojolea Quran

  Taarifa zinazohusiana Tanzania Rais Jakaya Kikwete , alisema kuwa ghasia hizo hazikubaliki hata kama kitendo kama hicho kimefanyika na kuwaghadhabisha waisilamu. Historia ndefu ya watu kuvumiliana kidini haipaswi kupuuzwa, alisema Rais Kikwete.

  Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau mjini Dar es Salaam anasema kuwa ubishi ulitokea kati ya kijana mwenye umri wa miaka 14 mkristo na rafiki yake musilamu, hali iliyosababisha matukio ya vurugu siku ya Ijumaa.

  'Haki itendeke'

  Ubishi ulitokea baada ya kijana huyo mkristo kuambiwa na mwenzake muisilamu kuwa angebadilika na kuwa nyoka ikiwa angeikojolea Quran. Na kijana huyo akaitisha kitabu hicho na kisha kukikjolea ili kuona kama kweli madai ya mwenzake yangetokea. Kamanda mkuu wa polisi mjini Dar es Salama, Suleiman Kova, aliambia BBC kuwa watu 126 wamekamawa kuhusiana na tukio hilo.

  Mhubiri wa kiisilamu Sheikh Alhadi Musa, ambaye ni mwenyekiti wa kamati moja ya kidini, alilaani mashambulizi hayo dhidi ya makanisa
  Alisema kuwa kuwa Quran imekejeliwa na mtu mmoja kwa hivyo sio sawa kuchukulia hatua hiyo kama msimamo wa wakristo wote.
  Mipango inafanyika ya mikakati ya amani kufanyika kati ya waumini wa dini hizo mbili.

  Rais Kikwete aliyetembelea makanisa yaliyoshambuliwa siku ya Jumamosi alitoa wito wa amani na kusema kuwa wakristo hawapaswi kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwani hatua hiyo itachochea vurugu.

  Source: bbc
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Safi sana Mwema,kova na msangi! kamata hao mburula.wachapieni nao.watajuta kuufahamu mfumo kristo.
   
 3. Haliali

  Haliali JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Atajeuka nyoka, panya au atakuwa kichaa?. mbona kila siku linawekwa kitu kipwa. mwisho watasema angejeuka ---------
   
 4. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watavuna walichopanda
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yaani hawa wanasitahili adhabu akali sana ili iwe fundisho kwa wengine wanaodandia imani
   
Loading...