Wakala wa VH.SHAH wauza sukari kwa bei "chee" mikoa ya kanda ya ziwa

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Wakala wa VH.SHAH wauza sukari kwa bei "chee" kanda ya ziwa

WAKALA na msambazaji mkubwa wa sukari katika mikoa ya kanda ya ziwa VH. Shah, ameendelea kuuza sukari katika mikoa hiyo kwa bei elekezi inayotakiwa na Serikali.

Hivi karibuni, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, aliwaonya baadhi ya mawakala "wapigaji" wa sukari nchini kuacha kupandisha bei kwa madai ya kwamba bidhaa hiyo imeadimika nchini huku akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa atakaebainika.

Msimamo huo wa SHAH ni njia moja wapo ya utekelezaji wa agizo la Serikali la kuwataka wasambazaji (mawakala) wa sukari nchini kuuza sukari kwa mjibu wa taratibu.

Akizungumza Aprili 18 mwaka huu, amesema sukari yote iliyopo katika magahara yake, itauzwa kwa watu wote bila kubagua mtu au mfanyabiashara yeyote yule.

Pia amesema, bei ya sukari inayouzwa (na wao) ni bei ya chini ya bei elekezi iliyoelekezwa na Serikali huku akisisitiza kuwa hakuna sababu ya wao kupandisha bei.

"Sisi tunauza sukari mpaka chini ya bei elekezi, lakini unaweza kushangaa leo tumeuza sukari ya kilo 50 kwa Tsh.130,000 lakini kesho ukakuta tumeuza chini au zaidi ya hapo.

"V.H.Shah hatujawahi kupandisha bei na tunafanya kazi kwa mjibu wa sheria hatuwezi kufanya kosa la kupandisha bei ya sukari, tunafahamu tukipandisha bei ni kosa na tunaweza kufutiwa hata leseni na tunafanya kazi hii kwa kusasaidia wananchi wetu " amesema Shah.

Amesema kazi ya kusambaza sukari kanda ya ziwa wanaifanya kwa kufuata sheria na kanuni za biashara za nchi pamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. John Magufuli, anaepambana kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati.

"Rais wetu Magufuli anafanya kazi ya kuhakikisha nchi hii inakuwa na uchumi kupitia viwanda, sasa sisi tunafanya kazi hii ili kusaidiana nae, lakini unakuta kuna watu wanaongea mambo ya kwamba sisi tumepandisha bei kitu ambacho sio kweli," amesema.

Pia amewaondoa wasi wasi wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahakikisha kuwa sukari ipo ya kutosha na hakuna bei iliyopandishwa ya uuzwaji wa sukari.

Mkoa wa Mwanza, sukari ya KG 50 inauzwa kwa Tsh. 130,000 huku mfuko wa KG 25 ukicheza kwa Tsh. 60,000, ambapo bei hiyo ni kwa jumla.

Na Charles Charles
 
Hawa ndo wazalendo wa kweli kama vipi serikali iwapatie uwakala wa tz nzima tuachane na haya majizi wanaopenda pata faida nyingi kupitia mgongo wa matatizo katika taifa mfano kipindi ichi cha Covid
 
Hapo lazima kuna udanganyifu unafanyika. Haiwezekani mfuko wa kilo 50 unauzwa kwa ah 130,000/= ila wa kilo 25 unauzwa kwa sh 60,000/=. 25*2 = 50. Kibiashara anayenunua vingi anapata punguzo. Sasa hapa anayenununua vingi anabamizwa.
 
Iko haja ya distribution companies kuorodheshwa ktk stock exchange market na kupanua uwigo wa uwazi katika hiyo biashara na kuwashirikisha watu wengine
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom