Wakala wa upigaji kura ana umuhimu gani kwenye ushindi wa wapinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakala wa upigaji kura ana umuhimu gani kwenye ushindi wa wapinzani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Oct 18, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,094
  Trophy Points: 280
  Pamoja na mbinu zote za CCM na Tume ya uchaguzi ya Taifa za kuiba kura, kama wakala wa chama wa upigaji kura ni makini, mhadilifu, mwaminifu, hana tamaa, anaona mbali basi ushindi kwa wapinzani ni dhahiri. Kazi ya huyu wakala ni kuhakikisha uchaguzi ni huru na haki kuanzia upigaji kura mpaka kuhesabu na kutoa matokeo na sahihi yake inahitajika kwenye karatasi halisi ya NEC ya matokeo na anakuwa na nakala yake ambayo itasaidia kupinga matokeo ya ubunge na kumfanya Makame ashindwe kubadilisha matokeo!

  Muda wote kuanzia kufungua kituo mpaka kubandika matokeo anatakiwa kuwepo ingawaje sheria ya uchaguzi kwenye baadhi ya vifungu inasema 'kama wakala wa upigaji kura au mgombea yupo' hii lugha ni kutaka kuwafanya mawakala wasio makini waondoke mara baada ya kupiga kura kumalizika. Sheria inaruhusu kubadilisha wakala wakati wa kupiga kura, yaani kupata wakala mbadala.

  NEC wametangaza kuwa kutakuwa na vituo 52,000 (HabariLeo 15 Oct. 2010). Sasa wapinzani mmekwisha pata mawakala wa upigaji kura 52,000 wa uhakika? Naomba muwe na mawakala 52,000 wenigne wa uhakika kama mawakala mbadala mara yule wa mwanzo kupata dharura au kupewa hongo au kutishwa na kuondoka. Pili mnaweza kubadilisha mawakala karibu wote ili kufanya kama shift ili mawakala wawe makini muda wote, yaani asubuhi mpaka saa tisa wanakuwemo mawakala wa mwanzo 52,000 halafu kuanzia saa tisa mpaka matokeo kubandikwa wanakuwepo mawakala mbadala hii itasaidia mawakala kuwa makini muda wote bila kuchoshwa na njaa, usingizi na mambo mengine. Na naomba mendeshe semina kwa mawakala wenu na kuwaondolea ukungu kwenye macho yao ili waone Tanzania bora chini ya Urais kutoka chama cha upinzani!

  Huu ndio mchango wangu katika kulikomboa taifa letu!!!!!!!! Itaniuma sana kama kura yangu itachezewa.
   
 2. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimependa mawazo yako. Nafikiri kuanzishwe namna hapa Jf ya kusaidia chama kupata mawakala
   
 3. minda

  minda JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nimependa wazo lako lakini hukumtendea haki jaji makame kwa tuhuma yako ya kubadilish matokeo pale uliposema;

   
Loading...