Wakala wa kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) ni jipu

kirumonjeta

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
3,966
1,964
KDA wakishirikiana na wajanja wachache wameanza njama za kuwatapeli wananchi maeneo pembezoni mwa barabara baada ya kujifanya kubadili barabara ambayo wahusika wengi wakiwa hewa wameshalipwa na serikali mabilioni ya shilingi na kubadili ramani kukwepa maeneo yaliyolipwa ili wajanja wajimilikishe upya pamoja NA kuwa wamelipwa.

Tayari vigingi vimeshawekwa kwa ushirikiano na viongozi wasiowaaminifu kimyakimya bila taarifa huku wakijigamba hakuna wa kubadili walichokiamua

Magufuli kuna watu wanakubeep huku Kigamboni tena order ya kulipa maeneo hayo uliitoa mwaka jana kabla hujateuliwa kuwa mgombea wa CCM NA kushinda urais na kuamuru wananchi wasiguswe bali barabara ipite eneo lililopo wazi ambapo waliopo walilipwa mwaka jana na sasa wanataka kurudi kwa gia nyingine kupitia mgongo wa KDA lengo likiwa ni kujimilikisha maeneo hayo kifisadi.
e4a8Kigamboni-satellite-city.jpg


Habari zaidi...

SERIKALI ilitangaza kuanzishwa wakala wa kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA), ambayo itakuwa na kazi ya ujenzi wa mji huo. Hatua ya Serikali, ilikuja huku kukiwa na malalamiko ya wananchi wa Kigamboni, wakiongozwa na Mbunge wao, Dk. Faustine Ndugulile (CCM), kupinga mradi huo kwa madai kuwa umeanzishwa kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam Januari 24, 2013, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema kuanzishwa kwa wakala huo kutaisaidia kusimamia vizuri kupanga mji wa Kigamboni kama inavyotakiwa.

Alisema kuanzishwa kwa KDA, kutaifanya Kigamboni kuwa na mamlaka yake kamili, ikiwemo kuwa na baraza la madiwani ambalo litakuwa na jukumu la kupanga mipango yao kama ilivyo kwa mamlaka ya Ustawishaji wa Mji Dodoma (CDA) na taasisi nyingine za Serikali.

Alisema muundo wa mamlaka hiyo, utaongozwa na mkurugenzi mtendaji na wakurugenzi sita, ambao watakuwa wakuu wa idara ambao kwa pamoja, watasimamiwa na bodi ya ushauri na Baraza la Ushauri la Kigamboni.

Alisema baraza hilo, litakuwa na wajumbe wanaowakilisha wadau wote, wakiwemo wabunge, madiwani na wananchi wa kawaida.

Alisema kutokana na kuundwa kwa mamlaka hiyo, Manispaa ya Temeke haitahusika na suala lolote katika mji huo, kwani wakala huo utakuwa na vyombo vyake vya usimamizi kisheria.

“Kuzaliwa Kigamboni Development Agency (KDA), ni safari ya kuelekea katika kutimiza ahadi ya Serikali ya CCM kwa wananchi wake, hasa katika utekelezaji wa ilani yetu.

“Kwa hali hii, nafasi ya mkurugenzi mtendaji itatangazwa na kushindaniwa na Watanzania wenye uwezo waliopo ndani na nje ya nchi, kwa kuwa anahitajika mtu atakayekuwa na uzoefu katika masuala ya mipango miji.

“Wakati nikiwa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat), mengi tumejifunza na hili linalofanyika Kigamboni sasa ni kutaka kuufanya mji huu kuwa wa kisasa zaidi na wa kimataifa kama ilivyo kwa mji wa Dubai, ambao umepangiliwa vizuri.

“Utekelezaji wa mpango wa kuendeleza mji huo, utakuwa na matokeo mazuri, ikiwemo kuwa na mji uliopangwa kwa kiwango cha kimataifa, kupunguza ujenzi holela, kuongeza mapato ya Serikali yanayotokana na shughuli za viwanda.

“Kwa hali hii, sasa milango imefunguliwa ambapo Kigamboni mpya itakuwa na majengo ya kisasa, zikiwemo hoteli zenye hadhi ya nyota tano, hali itakayokuza biashara ya utalii wa ndani.

“Pia mji huu, utazingatia ujenzi wa vituo vya kibiashara vyenye hadhi ya kimataifa pamoja na vyuo vya elimu ya juu na vituo vya michezo,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alisema kwa kuanza, KDA kutakuwa ni mwanzo wa kuanza malipo kwa wakazi 80,000 ambapo watafidiwa nyumba zao kutokana na soko la sasa la nyumba na ardhi.

“Gharama ya mradi mzima hadi kukamilika ni Sh trilioni 11, huku awamu hii tutatumia Sh bilioni 60.

“Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), litajenga nyumba 500, kampuni kutoka Dubai itajenga nyumba 250 na wadau wengine nao watajenga majengo ya uhakika.

“Katika hili, tunapenda kuyakaribisha makampuni ya uwekezaji ya nyumba kama wafanyabiashara kama kina Fida Hussein na wengineo, ambao wana uwezo wa kujenga majengo ya kisasa katika mji huu wa kisasa.

“Kutokana na malipo ya fidia, wananchi hawatahamishwa bila kupewa nyumba ambazo zinajengwa katika eneo hili, ninapenda kuwatoa hofu hakuna ambaye atadhulumiwa haki yake, ikiwemo ya kuhakikisha wanapewa fedha zao na nyumba ya kuishi.

“Lengo letu, ni kuona hakuna hata mwananchi mmoja anaondoka na manung’uniko wakati wa utekelezaji wa mradi huo, kwani kutakuwepo na ujenzi wa nyumba za bei tofauti.

Alisema kutokana na hali hiyo, wananchi ambao wana viwanja katika eneo la Kigamboni, wanatakiwa kupewa vibali vya ujenzi na KDA ambapo wataelekezwa hata namna ya ujenzi na upakaji wa rangi za kisasa.

Uendelezaji wa mji wa Kigamboni, unatarajiwa kujengwa nyumba 400,000 na awamu ya kwanza, inatarajiwa kukamilika mwaka 2022 na mradi mzima utakamilika mwaka 2032.

Eneo linalotarajiwa kujengwa ni lenye ukubwa wa hekta 50,934 na litahusisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila, Kisarawe II, Kimbiji na Pemba Mnazi.

====

UPDATES:

Hatimaye Rais Magufuli ameivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni (KDA). Habari zaidi soma=>Lukuvi: Rais Magufuli ameivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni (KDA)
 
Back
Top Bottom