Wakala wa Barabara nchini (TARURA) sasa wameingia kwenye Biashara hatarishi ya Parking System

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Na
Alloyce Nyanda Mtozi

Wakala wa Barabara nchini (TARURA) sasa wameingia kwenye Biashara hatarishi ya Parking System ,leo ukiwa na gari lako ukaingia mjini ukapaki kuna watu wanakupiga picha plate namba yako wanatuma kwenye System yao .

Na bei halali ya Parking ni 1500 tu ,ikitokea umesema utalipa kesho hiyo hela basi unatakiwa kulipa elfu 40 pamoja na e 1500 ,Au ukiwa wakati huo huna hela unasema basi nitalipa kesho kwa M pesa hutatakiwa kulipa 1500 bali utalipa Elfu 40 jumlisha elf 1500 ,ukikaa siku mbili utalipa Elfu 80 ,Na wanapiga cheni na kubeba Magari kuyapeleka Maeneo yao

Serikali itajikuta inapata fedha za Uonevu kwa watu Masikini! Hivi ni kweli ubunifu wa kukusanya mapato umeshindikana mpaka tuviziane? mpaka tupigane Faini za kukomoana kiasi hiki?

Elfu 1500 Faini yake ni 40? Rais alisema msifanye watanzania ni wajinga Kiasi hicho! Tutapaki Magari na kupanda daladala kwani kuna hasara gani?

Wasi wasi wao ni upi? Kama wamechukua namba ya gari, wameweka kwenye Kumbukukumbu zao hivi hawezi hata kusema siku mbili zikipita utapigwa faini mbona Trafiki barabarani ukipigwa Faini kuna muda wa siku 7 na unalipa 30 sio 40

Mi nadhani wao waendelee kuchoma tu ,Itanuka tu na harufu itawafikia popote walipo

Angalia jamaa yangu ameshaliwa tayari! Hapo chini

FB_IMG_1557825437921.jpeg
 
HIVI TOFAUTI YA TARURA NA TANROADS NI IPI?
TARULA ni wakala wa barabara mijini na vijijini, yaani kwa nyongeza ni kuwa zile barabara zote ambazo hapo awali zilikuwa chini ya Halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji sasa zinashughulikiwa na TARULA.
TANROADS inabaki na barabara zenye hadhi ya kitaifa zinazounganisha tarafa, wilaya, na mikoa.
 
MBONA KAMA NAONA MAJUKUMU YA TARURA NA TANROADS HAYATOFAUTIANI SAANA?
 
Ni kweli, wanachotofautiana ni maeneo ya kazi tu.
Hapo awali kabla TARULA haijaundwa fedha za barabara zilikuwa zinaingizwa kwenye account za halmashauri, moja ya Changamoto zilizokuwepo ni ubadilishaji wa matumizi ya fedha hizo, ndo wakaona suruhu ni kuwa na agency itakayohusika na hizi barabara ndogondogo za mjini na vijijinii

GOOD, HAPO NIMEKUSOMA MKUU
 
MBONA KAMA NAONA MAJUKUMU YA TARURA NA TANROADS HAYATOFAUTIANI SAANA?
1. TANROADS ipo chini ya wizara ya miundo mbinu na mawasiliano lakini TARURA ipo chini ya TAMISEMI
2. TANROADS ni barabara zinaunganisha taifa na mataifa mengine pia barabara zinaunganisha mkoa kwa mkoa lakini TARURA inahusika na barabara zinaunganisha wilaya hadi wilaya, tarafa hadi tarafa, kata hadi kata Kijiji hadi Kijiji bila kujali mjini au kijijini.
 
UFAFANUZI MZURI MKUU
 
jamaa hawa wa tarura wabaya sana wapo wawili mmoja anasema yeye ni muhaya na mmoja mzaliwa igoma mwanza hutembea kwenye bajaji wawili tu kukamata watu hula ruushwa sana mimi nilikuwa nimepark mnazi mmoja kwenye vitenge namgoja mwanangu nilimwambia ataremke kwenye daladala mimi nilikuwa kwenye gari na gari sijazima nimewasha hazard wakaniona wakaingia kwenye gari wakanilazimisha nilipe faini elfu 50000 nikawaambia nimepark pembeni nimewasha hazard wakasema hatujui lipa faini mwisho ilinitoka elfu 20 wakaniachia baada ya siku mbili nilienda jiji kwenye offisi yao nyuma ya jmall nikamweleza boss wao akasema kama uliwasha hazard sina makosa ila akaniuliza ulipiga picha nikamwambia sikupiga nikawa sina ushahidi ila huwa nawaona hao jamaa mjini ndani ya bajaji kwenye mawindo nitaleta picha zao humu siku zinazokuja
 
1. TANROADS ipo chini ya wizara ya miundo mbinu na mawasiliano lakini TARURA ipo chini ya TAMISEMI
2. TANROADS ni barabara zinaunganisha taifa na mataifa mengine pia barabara zinaunganisha mkoa kwa mkoa lakini TARURA inahusika na barabara zinaunganisha wilaya hadi wilaya, tarafa hadi tarafa, kata hadi kata Kijiji hadi Kijiji bila kujali mjini au kijijini.

Wakati (TANROADS) wakiunganisha barabara za taifa na mataifa mengine, mkoa na mkoa wanakuwa wanaruka wilaya ama tarafa au vijiji?
 
Tatizo kubwa ni nchi kuanza kupiga hajua,kuirudisha serikali na taasisi zake kwenye biashara badala ya kuachia sekta binafsi zifanye biashara
 
Back
Top Bottom