Wakala nauliza :Airtel money mnakwama wap? Igeni Tigopesa au Mpesa

Uzalendo Installer

JF-Expert Member
Nov 8, 2014
5,365
8,836
Airtel Money tunaomba muweke mfumo wa kuangalia commission zetu mawakala kama ilivyo kwa vodacom au tigopesa... Tuwe tunaweza kuangalia commission muda wowote ili tuweke hesabu zetu sawa na sio kututumia sms asubuhi za commission kila siku.
Hii inatukatisha tamaa sana maana, kwanza commission yenu ni ndogo sana alafu hujui utapata kiasi gani au umefikisha kiasi gani.
Vodacom na tigo unaweza kuangalia commission muda wowote na ukapangilia hesabu zako.
Kwa mfumo uliopo airtel sasa hiv.. Unatoa mwanya mkubwa wa kutolipwa kamisheni yako mwisho wa mwezi.. Mimi binafsi sikulipwa miezi miwili, nilifatlia kwa wakala mkuu nae akapeleka makao lakin mpaka leo hakuna kitu na tulikuwa wengi.. Labda niwape sababu kwanini tunafunga uwakala wa airtel money
1: kamisheni yenu ndogo sana
2: asilimia za kutolipwa hiyo kamisheni yenu ni kubwa sana yaani mawakala tunakaa na maswali kichwani sijui mwezi huu nitalipwa au la
3: customer care yenu mbovu sana.. Ukiwapigia simu huwa wanajibu majibu mabaya sana
Rekebisheni mambo hayo ili tufanye biashara vizuri.. Pia ongezeni time out ya system yenu inawahi kukata wakati wa kutuma pesa.
Nawasilisha.
 
Kwenye swala commission inategemea na eneo ulipo lipo center na kuna mzunguko wa biashara?...cha pili uwezi linganisha wakala wa aitel money manyara na DSM au tanga kwenye commission coz manyara watumiaji wa airtel n weng ukilinganisha DSM na Tanga..kingine chukua pen na daftari kila asubuhi note commission ikifika tar 25 utapata jibu..nb airtel money mwezi wanafunga kila tar 25 ya mwezi.
 
Kwenye swala commission inategemea na eneo ulipo lipo center na kuna mzunguko wa biashara?...cha pili uwezi linganisha wakala wa aitel money manyara na DSM au tanga kwenye commission coz manyara watumiaji wa airtel n weng ukilinganisha DSM na Tanga..kingine chukua pen na daftari kila asubuhi note commission ikifika tar 25 utapata jibu..nb airtel money mwezi wanafunga kila tar 25 ya mwezi.
Boss dunia hii ya leo kila siku unaandika kamisheni asubuhi.. Kama una ofisi zaidi ya moja unafanyaje?.. Kwanini nao wasiwe kama wenzao...tengeneza 'user friendly syatem' engineers wanaelewa sana hii kitu...
Pili kamisheni ya airtel money ni ndogo hata uwe wap.. Kwa maana utazungusha pesa nyingi alafu unapata kiwango kidogo...
Tatu, sijawah kulipwa tarehe 25, nadhan kama wao wanafunga mwezi huo Sisi wanatulipa mwisho wa mwezi tena mwezi ukianza..
 
Airtel nilifikiri kwa wateja tu kumbe mpaka mawakala??

Wanachosha kwenye kastama kea, wameamua kuwa washindi wa kastama kero.

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Aitel kamishen zao ni ndogo sana.
. Yaan unaweza hudumia wateja wengi lkn malipo yao had unashangaa
 
Hapa ndio mawakala tunapigwa na kitu kizito na ndio eneo ambalo Airtel hutuibia mawakala
 
Back
Top Bottom