Wakala mnaosajili ni wahuni, nimekuta namba nisiyoifahamu kwenye uhakiki

Bin Shaib

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
1,315
1,186
Habari tena wana jukwaa, nimekuja kasi sana usiku huu baada ya kukutana ma swala ambalo limenikera sana tena sana,
Ni baada ya 1-8-2020 Vodacom walinitumia ujumbe kuwa nihakiki namba zangu zilizosajiliwa kwa namba yangu ya NIDA.

Wakati huo sikuwa nayo hiyo namba yangu ya NIDA, nilitaka nihakiki kuna nini?

Ndio muda huu nimeingia kulala nahakiki nakuta namba ambayo siifahamu,, nimeenda kwa upande wa m-pesa jina limesoma la kwangu,, walah nimejiuliza sana.

Kumbe hawa mawakala wameanza uhuni hapa mjini.

Nipo natunga sheria na kabla sijachukua maamuzi nahitaji ushauri toka kwenu.

a) Je, nikamripoti polisi mwenye hii namba kwa kosa la kudukua namba yangu ya NIDA pasipo taarifa?. Na iwe funzo.

b) Au niende tu Vodashop ikafutwe?

c) Wakala aliye kamilisha hii namba anaweza kupatikana kwa kuangalia mashine yake ya usajili?.

Asanteni kwa usomaji mwema
Nimeumia sana hawa mawakala msiwaamini japo sio wote,,

Ushauri" ingefanywa system ukimaliza kusajili history zinafutwa kwenye mashine zao za usajili ingekuwa vyema.

©Bin Shaib Classic 2020
 
Mkuu naona umekuja fasta sana alafu unaonekana unajazba kama wewe ni mgeni na vitu hivi.....haya mambo ni kawaida sana wala si vyakushangaza chamsingi katika iyo menu ya kuangalia usajili pia inakuruhusu kufuta hivyo ni swala ambalo halihitaji kuumiza kichwa.
 
Kwa nilivyoelewa ni kwamba kuna namba usiyoifahamu imesajiliwa kwa kutumia kitambulisho chako, na ukicheck mpesa jina ni la kwako.
Ukienda kushtaki polisi utakuwa unamshtaki nani?
 
demi nakupenda ila umeniangusha kwakwel, kwahiyo hujamuelewa?
 
Mkuu naona umekuja fasta sana alafu unaonekana unajazba kama wewe ni mgeni na vitu hivi.....haya mambo ni kawaida sana wala si vyakushangaza chamsingi katika iyo menu ya kuangalia usajili pia inakuruhusu kufuta hivyo ni swala ambalo halihitaji kuumiza kichwa.
Asante mkuu kwa kunielewesha.
 
Kwa nilivyoelewa ni kwamba kuna namba usiyoifahamu imesajiliwa kwa kutumia kitambulisho chako, na ukicheck mpesa jina ni la kwako.
Ukienda kushtaki polisi utakuwa unamshtaki nani?
Naishitaki hiyo namba.
 
Kwa nilivyoelewa ni kwamba kuna namba usiyoifahamu imesajiliwa kwa kutumia kitambulisho chako, na ukicheck mpesa jina ni la kwako.
Ukienda kushtaki polisi utakuwa unamshtaki nani?

Asiyejulikana
 
Umeoooa???
Maana.kama.uko.KWENYE ndoaa using estupotezea .MDA hapaa
Unatulizaa wakati HAO wamekwambia kama.HUJUI namba ufwate procedure
Ina maana huwaamini mpaka.uje Jf
YESU WANGU.
 
Mkuu naona umekuja fasta sana alafu unaonekana unajazba kama wewe ni mgeni na vitu hivi.....haya mambo ni kawaida sana wala si vyakushangaza chamsingi katika iyo menu ya kuangalia usajili pia inakuruhusu kufuta hivyo ni swala ambalo halihitaji kuumiza kichwa.
kufuta mpaka uende kwenye shop zao,sio kwa simu tu.
 
nida haiwezi kudukuliwa kwa Ivo...eti mtu adukue no za nida afu akamilishe usajili juu kwa juu bila wewe kuhusika...!??hiyo ni non sense

2.unaeza futa iyo namba tu vodashop....

3:aliesajili iyo namba kimagumashi anapatikana tu easy....ila ukitaka usipoteze muda we kafute tu iyo namba Kama huitambui
 
Kwa nilivyoelewa ni kwamba kuna namba usiyoifahamu imesajiliwa kwa kutumia kitambulisho chako, na ukicheck mpesa jina ni la kwako.
Ukienda kushtaki polisi utakuwa unamshtaki nani?
Mbona uonekani Twtter sikuhizi.
 
Back
Top Bottom