Wakala M-Pesa, tiGo-Pesa, Airtel Money na Halo-Pesa

Daktari wa Manchester

JF-Expert Member
Jun 1, 2020
350
401
Habari zenu

Jamani Mimi ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu, nilikua naomba kujua ni process gani zinahitajika kusajili laini za uwakala wa halopesa na mitandao mingine na bei yake mana nilikua nataka niwe nafanya hiii Kaz kama side hustle nikiwa Chuoni

Naombeni mrejesho wenu
 
Nenda TRA omba TIN utafika halmashauli watakupa lesen ukipata hivyo vitu peleka ofisi za mitandao husika watakusaidia

TRA utawambia tu unataka kwaajili ya huduma za kifedha

Na halmashauli utawambia hivyo hivyo
 
TRA ni jinsi utakavyojieleza Ila Kodi minimum ni laki moja , lessen halmashaur ni 86000
 
Ujitahidi pia kuwa na kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA. Maana ni moja ya viambatanisho kwenye huo mchakato.
 
TRA ni jinsi utakavyojieleza Ila Kodi minimum ni laki moja , lessen halmashaur ni 86000
Sorry, na garama ya laini zenyewe ni TSH ngapi ?na hio kodi na ada uliyotaja ni per kila laini au kwa laini
zote ?? Msaad tafadhal
 
Upande wa Tigo pesa unapiga documents zako copy ya Rangi Tin number, Leseni ya Biashara na kitambulisho cha Nida na Tsh 25000
Upande wa Airtel Money uwe na documents na Tsh 21000

Upande wa M pesa unapiga documents zako copy ya Rangi na 21000

Hizo ndio laini za kuanzia nazo
 
Habari zenu

Jamani Mimi ni mwanafunzi wa Chuo kikuu, nilikua naomba kujua ni process Gani zinahitajika kusajili laini za uwakala wa halopesa na mitandao mingine na bei yake mana nilikua nataka niwe nafanya hiii Kaz kama side hustle nikiwa Chuoni

Naombeni mrejesho wenu
Njoo nikuuzie za kwangu
 
TRA ni jinsi utakavyojieleza Ila Kodi minimum ni laki moja , lessen halmashaur ni 86000
Hivi hio kodi inalipwa hata kabla hujaanza biashara na hiyo kodi itakaaa muda gani ili ulipe tena au ukilipa hiyo laki ndio hulipi tena naomba nifahamishe tafadhali
 
Hiyo kodi ni kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Itakulazimu ulipe kabla hujaanza biashara kwa sababu ni moja ya kiambatanisho katika fomu zako za maombi ya uwakala.

NB:
Zamani, gharama za uwakala ni bure kabisa ila walitaka uwe na uwezo wa kukuwekea walau float ya Tsh 1,000,000.

Itakuchukua miezi mitatu mpaka upate uwakala. Lakini ukitaka kwa haraka, jiandae kutoboka.

Lakini;
Unaweza kununua kw watu wanaouza. Gharama huwa kati ya 150,000 mpaka 250,000.

Changamoto ya line za kununua ni kwamba, ikipotea lazima aliyekuuzia ndiyo afanye mchakato kuirejesha.

Hutoweza kuhudumiwa pale utakapohitaji cash kutoka benki, kwa kuwa ni lazima uonyeshe kitambulisho chako kibachoendana na usajili wa till husika.

Kuwa makini utakapoamua kuzinunua, zingine zina mikopo ya SONGESHA na mikopo nyinginezo. Ukitia tu mpunga, wanondoka nao.
 
Nimekupata hapa shukrani

Itakulazimu ulipe kabla hujaanza biashara kwa sababu ni moja ya kiambatanisho katika fomu zako za maombi ya uwakala.

NB:
Zamani, gharama za uwakala ni bure kabisa ila walitaka uwe na uwezo wa kukuwekea walau float ya Tsh 1,000,000.

Itakuchukua miezi mitatu mpaka upate uwakala. Lakini ukitaka kwa haraka, jiandae kutoboka.

Lakini;
Unaweza kununua kw watu wanaouza. Gharama huwa kati ya 150,000 mpaka 250,000.

Changamoto ya line za kununua ni kwamba, ikipotea lazima aliyekuuzia ndiyo afanye mchakato kuirejesha.

Hutoweza kuhudumiwa pale utakapohitaji cash kutoka benki, kwa kuwa ni lazima uonyeshe kitambulisho chako kibachoendana na usajili wa till husika.

Kuwa makini utakapoamua kuzinunua, zingine zina mikopo ya SONGESHA na mikopo nyinginezo. Ukitia tu mpunga, wanondoka nao.
 
Habari zenu

Jamani Mimi ni mwanafunzi wa Chuo kikuu, nilikua naomba kujua ni process Gani zinahitajika kusajili laini za uwakala wa halopesa na mitandao mingine na bei yake mana nilikua nataka niwe nafanya hiii Kaz kama side hustle nikiwa Chuoni

Naombeni mrejesho wenu
Nasikia mpesa wamesitisha kutoa lain za uwakala wa mpesa.
 
Habari zenu

Jamani Mimi ni mwanafunzi wa Chuo kikuu, nilikua naomba kujua ni process Gani zinahitajika kusajili laini za uwakala wa halopesa na mitandao mingine na bei yake mana nilikua nataka niwe nafanya hiii Kaz kama side hustle nikiwa Chuoni

Naombeni mrejesho wenu

Hongera kwa kujiongeza.
Ukafanikishe hadi na crdb na nmb wakala
 
Nifollow pm, nikupe mchongo wa namna ya kupata line ya halopesa within 2 days, kwa gharama nafuu sana.

Hizo line zingine eg. Voda, Tigo na Mpesa, hadi nifatilie ili nikupe details.
 
Back
Top Bottom