Wakala ‘akomba’ mabilioni NHC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakala ‘akomba’ mabilioni NHC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Mar 29, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira imebaini kuwapo kwa mtu aliyekuwa akihodhi nyumba 30 za Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) huku akizitumia kujipatia takribani Sh milioni 525 kwa mwezi kutoka kwa watu aliopangisha.

  Taarifa juu ya wakala huyo ambaye hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati, James Lembeli, na
  uongozi wa NHC hawakuweka jina lake hadharani mbele ya waandishi wa habari, ilitolewa wakati wa kuelezea changamoto zinazolikabili shirika hilo.

  Akikariri taarifa kutoka kwa uongozi wa shirika, Lembeli alisema mtu huyo alikuwa akihodhi nyumba hizo eneo la Masaki, Dar es Salaam na mkataba wake ulisitishwa Januari.

  Kamati na uongozi wa shirika, pia hawakuweka bayana undani wa mkataba huo; muda na maudhui yake.

  Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa NHC, Lembeli alisema wakati mtu huyo alikuwa akiwasilisha dola 15,000 (Sh milioni 225) za Marekani kwa NHC kila mwezi, binafsi alikuwa akibakiwa na dola 50,000 (Sh milioni 750) kila mwezi.

  Katika kile ambacho Mwenyekiti huyo wa Kamati alisema ni matokeo ya mikataba mibovu kati ya NHC na wapangaji wake, alisema kwa mwaka, wakala huyo alijipatia dola 600,000 (Sh milioni 900) dhidi ya dola 180,000 (Sh milioni 270) alizowasilisha NHC.

  “Naomba muwe wakali. Serikali isiwatetee. Tatizo wengi wa wapangaji wa Shirika la Nyumba ni wastaafu, wafanyabiashara wakubwa na watumishi wenye nyadhifa,” alisisitiza Lembeli.

  Mwenyekiti huyo alisisitiza, “kama kuna wengine wa aina hii, zichukuliwe hatua. Naamini wapo wengine wanaohodhi nyumba na kukodisha kwa wengine.

  Kwa nini haya yatokee kwenye taasisi za Serikali?” Alihoji. Kamati hiyo ililitaka Shirika kuhakikisha linaingia mikataba yenye tija na uwezo wa kuwabana wapangaji, kuhakikisha haitoi mianya ya kulifikisha mahakamani.

  Kwa mujibu wa Lembeli, zipo kesi zaidi ya 200 kati ya NHC na wapangaji ambazo ni matokeo ya mikataba mibovu.

  Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, alisema mkataba wa wakala huyo ulisitishwa na nyumba kurudishwa kwa Shirika tangu Januari.

  Mchechu ambaye alishika wadhifa huo Aprili mwaka jana, hata hivyo alipongezwa na kamati hiyo kwa kilichoelezwa kwamba tangu aongoze shirika, baada ya miezi minne, yapo mabadiliko makubwa chanya yaliyojitokeza.

  Miongoni mwa mambo yaliyopongezwa kufanywa na uongozi huo mpya, ni pamoja na ongezeko la makusanyo ya madeni ambayo kulingana na taarifa iliyotolewa, hadi Novemba mwaka jana, Shirika lilikuwa na Sh bilioni 1.5 benki lakini sasa zipo Sh bilioni nane.

  “Wabunge wamekubali, watendaji ni wazuri, wana uwezo na nia ya kufanya kazi… sana sana ni
  vijana,” alisema Lembeli na kuitaka Serikali isiliingilie Shirika kwa kutumia wanasiasa ambao kwa mujibu wake, wamesababisha mashirika mengi kufa.

  Wakati huo huo, Mchechu alisema leo wanaanza operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu walioshindwa kulipa malimbikizo ya kodi.

  Deni linalodaiwa kutoka kwa wapangaji ni Sh bilioni 4.8. Kamati ya Bunge ilishauri majina ya wadaiwa wakubwa na kiasi cha fedha wanazodaiwa viwekwe hadharani.

  Katika hatua nyingine, Kamati iliishauri Serikali kufanya mabadiliko ya Sheria iliyounda NHC ili kuiwezesha kukopa benki bila kulazimika kupata kibali cha Hazina, ili iongeze kasi ya ujenzi wa nyumba za kuuza.

  Kwa mujibu wa Kamati, ombi hilo linazingatia kwamba mkakati wa ujenzi wa nyumba 15,000 ndani ya miaka mitano, unahitaji kasi, jambo ambalo upo wasiwasi kwamba hatua ya kusubiri kibali cha Wizara, inaweza kulikwamisha.

  Ilitaka mabadiliko hayo ya Sheria namba 2 ya mwaka 1990 iliyounda NHC pia yaiondolee Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati wa kuuza nyumba hizo, ili kukidhi malengo ya kuziuza kwa bei nafuu.
  HABARI LEO,CHANZO
   
 2. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #2
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lazima atakuwa mhindi, maana nyumba hizo ni mali yao
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hiyo kamati iangalia pia kwa makini huu mpango wa kujenga nyumba kwa ubia
   
 4. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  wahariri muwe mnahakiki taarifa zenu na kama hamuwezi muulkize kwa wataalamu husika. Dola 15,000 sawa na Tshs 225 million?!,dola 50,000 sawa na Tshs 750 million? halafu dola nyingi, 180,000 sawa na Tshs 270,000?!! hii nini hii?!
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Well done and noted.....
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama mtoa mada amefanya COPY and PASTE - basi kutakuwa kuna tatizo kubwa sana la KIMAHESABU na aidha Mwandishi wa Habari au Kamati ya Bunge...

  Halafu pia, inakuwaje Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge "anawaomba" NHC wafanye kazi yao?
   
 7. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hizi nyumba zilikua meant kwa ajili ya wahindi tu au? Maana kwa Arusha, Nyumba na maduka karibia yote yanamilikiwa na hawa jamaa. Hili likamati linatakikana lihoji process ya kupata hizi nyumba na iwekwe open.
   
 8. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  alafu NHC wakitaka kupandisha bei wahindi wanalalamika

  If they are so f***en poor kwa nini wasiende kuishi Mbagala!!
   
 9. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huwa sielewi kwa nini JIZI linaiba pesa za serikali halafu jina halitajwi
   
 10. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Habari inakosa mvuto pale inazungumzia mabilioni lakini huko ndani unakuta $15,000 kwa Tzs 225,000m au $50,000 kwa Tzs750,000m; tunashindwa kujua takwimu ipi iko sahihi.
  Source yenyewe ni Habari Leo, gazeti la mipasho!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Hilo la management kuongeza makusanyo kutoka 1.5 bilioni mpaka 8 bilioni linastahili kupongezwa hasa kwa kujua kwamba wengi wa wakurugenzi/mameneja pale ni vijana.
   
 11. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwanza tukubaliane kuwa nyumba hizi serikali iliwadhulumu waliokuwa wanazimiliki,pia ijulikane kuwa wakati serikali inadhulumu nyumba hizo waliokuwa wamiliki i e wahindi ndio walokuwa wanaishi katika nyumba hizo,kwa hiyo obviously wengi wao bado wanaishi humo, lakini pia naomba tukubaliane kuwa wapo baadhi ya waafrika waliopangishwa katika nyumba hizo na baadae wao wenyewe kwa tamaa ya fedha wakaamua kupisha wahindi kwa malipo, mimi ninalo duka mitaa ya Kariakoo, mwafrika alokuwa anapanga katika duka kaniambia anataka USD 25000 ili anipishe , nikampa na leo mimi ndio mpangaji wa NHC, kosa langu nini? Au unataka wahindi wote tufunge pesa zetu kwenye zipu? au ungependa sote tufanye ''ubia'' na TBL, ?? Mimi napenda kukushauri angalia ulipojikwaa sio ulipoangukia,
  ?
   
Loading...