Wakaka naomba kujifunza haya kutoka kwenu..

cocochanel

Platinum Member
Oct 6, 2007
26,701
73,281
Salamu kwako, Jamani mawasiliano, mawasiliano, mawasiliano why #matatizo huwa hayaishi?

Mimi nimekuwa nashindwa kuelewa juu ya mawasiliano kati ya wanaume na wanawake hadi leo sababu yana mengi, ila naamini wewe utaweza kuandika yako ikasaidia kuelewa.

Kwa kweli nikiongea na marafiki zangu tukitoka tunakaa chini, hata sehemu za pembezoni mwa ziwa huku napoishi na upepo mzuri bado malalamiko ya kila aina hayaishi. Ukweli ni kama mpo 10 basikila mtu na malalamiko yake, lazima kuna kitu lazima...sababu gani mnafanya haya kuumiza wanawake?

Hii ni kwa walio single, walio married, walio separate n.k.

1. Mnapenda mawasiliano ya aina gani na wenza wenu mke/mchumba/girlfriend?

2. Ni nini kinakusumbua kichwa ukiona katika mawasiliano mwanamke anafanya sana na haupendi? unamweleza au unaacha hivyo lililo na liwe? au unamkimbia?

3. Kama mwanaume wewe hupendi mawasiliano na mwenza wako akajitahidi kufanya hivyo, je kumkalia kimya au kuandika vineno viwili vitatu na kutokumjibu mengine ni sawa?

4. Mume unatoka ndani unachelewa, wala haufikirii kumpa taarifa mwenzako, hata ka message hapana, hata basi simu ya sekunde 25 hupigi kwa nini?

5. Mwanaume umekaa unadai unampenda girlfriend wako, ila mawasiliano mabaya upo kama haupo. unalalamikiwa anasema inamuumiza wewe hujali eti upo busy. Hii imekaaje kwenu? sababu ni nini?

6. Ukiwa haupendi kutumiana message na haujaribu njia ingine, only kusubiri uandikiwe ndio hujibu hiyo imekaaje na reasons zako ni nini?

7. Mwingine unakaa unamwambia mwenzako kuwa hupendi kuwasiliana, ila ukianza kuchat hata na wanawake marafiki unakuwa unajua kuandika kama cherehani. hii inakuwaje unamuumiza mwenza hivi? hapo anajua au anasikia au anaona. Hata ndugu zake unafanya hivyo bila shida, ila ikija kwake unadai unampenda mapenzi mengi bali mawasiliano sifuri kama vile unasukumwa, ni nini kinachojiri kwako

8. Wanaume mnapenda kusumbua wanawake wawapende, mkiwapata tu mnaanza habari nyingi kama upo busy sana hata kusema kwa wiki mbili tatu utakuwa busy. Ukipata mkakubaliana mahusiano unabadilika, unakuwa sio yule msumbufu hata salamu hutoi asubuhi hapo mnaishi nyumba tofauti. Inakuwaje hivyo umfanyie mwenza hayo na hausemi sabau bali kuishi kuumiza roho ya mtu

9. Mwanaume anasema kwa mwenza nitakupigia, inapita mawiki hata siku moja hajawahi kupiga hata missed call kutokea ika ukasema alikukumbuka, ni nini hupendi kama uko hivi sababu nini?

10. Mwingine yake ni huko kwenye viber sijui imo, anatuma message kwa mpenzi anajibiwa. akiandika tena hata kuaga au kuuliza kitu, basi hajibiwi tena na hapo anaona mtu yupo online. Na baadae anaweza kuona mtu yupo online lakini wapi anauchuna..je ni hataki aandikiwe tena au anaona anasumbuliwa? je ni nini kama sio kuonyesha dharau, kweli unapata notification then unaiacha hata not read for over thre days hata wiki. mwanaume ni nini kinajiri?

11. kwa wewe unayependa kutoa sababu mia, mia mbili, kwanini yote hayo?
...

nimejaribu kuandika ila napenda sana kujua ni nini kinawaudhi katika mawasiliano zaidi ya hayo nimejaribu kuweka juu niliyosikia kutoka kwa wenzangu.

Nitafurahi sana mkinielewesha kwanini mawasiliano mnakuwa na mengi,
kama hamtaki mnajisikiaje kitu umesema hupendi mwanamke bado anafanya?
Kwanini usimwambie hutaki tena mawasiliano?
je unakuwa unakaa sababu kuna kitu unatakakutoka kwake?
Je haufurahii kuwa yeye kakuwaza anataka kujua unaendeleaje na ndio maana anakutafuta kwa simu kuongea nawe au kutuma message?

mnisamehe kwa mengi, ila nimeishi na haya nasikia naona na naomba mnijuze nijue naamini wengi pia wanataka kujua mengi juu ya mawasiliano, kiini kikubwa cha uhusiano wa mapenzi.

ni miezi imenichukua kuja kuandika haya, hata mwenzangu husema hana majibu kila mtu ana yake...hayo yako ni yapi... Natanguliza shukurani
 
Mamii siri ya mtungi aijuae ni kata,wewe haya mambo ya mapenzi inaonekana wazi huyajui au vipi?,ukiona mtu na mpenzi wake hawaelewani na kuna sintofahamu basi ujue kuna siri inafichwa tena siri mbaya ya kuuwa mtu,hebu jiulize wewe Carrie nakutamani na nakufukizia miaka,mwisho unanikubali halafu tunaanza mapenzi motomoto,muda mfupi sana tena sana yaani 3 months nakuchoka na sikupendi tena na wala sikutamani kabisaaaa,je nini kimetokea?,ni kwamba una bonge la kasoro tena kubwa sana ambalo wakati nakutamani sikulijuwa,sasa nakuja kugundua au vipi?,na moyo wangu unaingia nyongo nakuchukia kuliko sumu,hasa nikikumbuka ulivyokua unadengua na kutaka kunitoa roho,kumbe kila kitu made in China(fake),unategemea mimi niwe fala wa kuishi na mwanamke wa maigizo mimi?,potelea mbali coz roho yangu imeshaona wewe sio yule niliokufikiria kabisa,so nenda ukatongozwe na watu wa aina yako,.,.,.periooood.
 
Wanawake mnasumbua sana.. Huo ujinga wa kuchatt muda wote nani anautaka? Mimi wadada wengi tumeshindana kwa hiyo tabia ya kutaka kuandikiana sms muda wote, hivi huwa mnadhani hela tunatafuta saa ngapi??
Kuchatt muda wote mnataka na pesa mnazitaka pia, chagueni moja basi!!
 
Mamii siri ya mtungi aijuae ni kata,wewe haya mambo ya mapenzi inaonekana wazi huyajui au vipi?,ukiona mtu na mpenzi wake hawaelewani na kuna sintofahamu basi ujue kuna siri inafichwa tena siri mbaya ya kuuwa mtu,hebu jiulize wewe Carrie nakutamani na nakufukizia miaka,mwisho unanikubali halafu tunaanza mapenzi motomoto,muda mfupi sana tena sana yaani 3 months nakuchoka na sikupendi tena na wala sikutamani kabisaaaa,je nini kimetokea?,ni kwamba una bonge la kasoro tena kubwa sana ambalo wakati nakutamani sikulijuwa,sasa nakuja kugundua au vipi?,na moyo wangu unaingia nyongo nakuchukia kuliko sumu,hasa nikikumbuka ulivyokua unadengua na kutaka kunitoa roho,kumbe kila kitu made in China(fake),unategemea mimi niwe fala wa kuishi na mwanamke wa maigizo mimi?,potelea mbali coz roho yangu imeshaona wewe sio yule niliokufikiria kabisa,so nenda ukatongozwe na watu wa aina yako,.,.,.periooood.
Brazaaaa umeua
 
hehe kaka congratulations hapo umegonga ndipo kwelikweli
 
Wanawake nyie ndo hamtabiriki.
mfano kuna mwanadada anapenda kuchat. Ila chatting yake inaboa kidogo tu anakutumia text ukimjibu yeye anaanza kujibu kifupi..sasa mtu kama huyu naweza nisijibu tena text zake siku nzima.
 
Kuna kitu kinaitwa obsession
Especially kwa kinadada ambao hawako busy na kaZi zao.....Kama upo busy na kazi zako,biashara zako au mishe zingine hayo yanatoka wapi
Maana asubuhi mnaagana kazi njema sawa
Mchana ikifika unamuambia mwenzio lunch time Kama upo karibu na free tukakule wote baada ya hapo mnakutana jioni
Hiyo mambo ya charting sijui kwenye fesibuku Au wasapu kila saaa sio mimi mwenyewe sipendi
Lakini kama ni mgeni amenitaka neno kwa msg itajibiwa tuuu....
 
Wanawake nyie ndo hamtabiriki.
mfano kuna mwanadada anapenda kuchat. Ila chatting yake inaboa kidogo tu anakutumia text ukimjibu yeye anaanza kujibu kifupi..sasa mtu kama huyu naweza nisijibu tena text zake siku nzima.
kaka nakuelewa....dada katuma text kasema hi.....alafu baada ya dakika kumi hivi kasma how r u......inaboa kwelikweli
 
Wanawake wengi hufikiria sura na shepu nzuri walizonazo ndo pekee wanaume wanachohitaji!!¡ wengine wachafu balaa! Unamfukuzia miezi, ukimpata siku moja humtamani tena, haya madawa ya nywele mnayotumia mara nyingi yanapunguza pafomance ya mwanaume' kuna 1 nilimwambia akaoge, alivorudi kutoka bafuni eti hajaosha kichwa! Sikumwambia chochote ila sitamani tena kuwa nae, ile harufu ya dawa aliotumia hata nikiifikiria tu kichwa kinauma" muwe mnajisafisha vzr sio sura tu na uzungu mwingi+uchina" haiingii akilini mtu akupende halafu ukimpa mara moja tu, kama alikupenda kwa 89% inashuka ghafla hadi 11% mjirekebishe"
 
Ntakujibu kwa namna hiii

1. Mnapenda mawasiliano ya aina gani na wenza wenu mke/mchumba/girlfriend?

Hapa kila mmoja ana namna yake ya kuwasiliana... Na hii inaweza ikawa inachangiwa na malezi mtu aliyopitia... Ila kwa ujumla, tunahitaji mwananmke muelewa.. Ukimwambia nimebanwa ndiyo maana sijawasiliana na wewe ka wakati uliouhitaji muwe mnaelewa

2. Ni nini kinakusumbua kichwa ukiona katika mawasiliano mwanamke anafanya sana na haupendi? unamweleza au unaacha hivyo lililo na liwe? au unamkimbia?

Hakuna mawasilianao yanayosumbua na yasiyosumbua... Kimsingi mawasilianao yoyote yatakayoharibu mahusiano ndo hayo hayatakiwi... Kwa mfano unajijuwa kabisa mume, mchumba au mpenzi wako anarudi saa flani toka sehemu flani, na muda huo akiwa amerudi wewe ndo upo bize na kuchart, kuongea na simu etc ilimradi unawasiliana na walio nje yetu... My friend, hapo doesnt matter kama unayewasiliana naye ni mama, baba, kaka au rafiki au ndugu mwingine yeyto... Ninapohitaji attension yako na wewe huileti hapo lazima pawe na shida....

3. Kama mwanaume wewe hupendi mawasiliano na mwenza wako akajitahidi kufanya hivyo, je kumkalia kimya au kuandika vineno viwili vitatu na kutokumjibu mengine ni sawa?

Kuna njia nyingi za kumkataza mwenza asifanye kitu fulani au asiwasiliane na wewe kwa wakati fulani kwa vile tu kuna kitu kinahitajika kifanyike kwa wakati huo. Sasa mwanzo huwa watu mnaambiwa lakini huwaga hamuelewi. Mwisho mtu anaamua aendelee na kile anachokifanya na atawasiliana na wewe pindi akimaliza. Kimsingi jitahidini kuwa waelewa, nini kifanyike na kwa wakati gani... Kuna muda mtu unamwambia nipo mkutanoni au nipo sehemu ambayo siwezi kuongea andi sms lakini bado misimu kibao..... UKIONA MTU HAKUJIBU, JUA KUWA AMESHAFIKIA MWISHO WA KUKUELEZA KWA NAMNA YA KAWAIDA KAONA SASA AKAE KIMYA PENGINE UTAELEWA

4. Mume unatoka ndani unachelewa, wala haufikirii kumpa taarifa mwenzako, hata ka message hapana, hata basi simu ya sekunde 25 hupigi kwa nini?

Hapa napo kuna shida moja toka kwa wanawake walio wengi... Siku ya kwanza mtu anakuaga, ntachelewa lakini matokeo yake mineno mnayotoaga ni kama vile hakuaga... YAANI AKIAGA NA ASIPOAGA KWENU NI YALE YALE, KWAMBA KACHELEWA... Nikutolee mfano kwa uzoefu wangu... Unaaga ntachelewa, tena wakati mwingine kikazi kabisaa na unaaga kwa landline ya kazini, lakini wapii... UNAONEKANA ULIKWENDA KUCHEPUKA... DO YOU EXPECT NTAAGA TENA? If you can make a difference kati ya kuaga na kutoaga kwenye maneno yako, yes, ntaaga kila nionapo ntachelewa...

5. Mwanaume umekaa unadai unampenda girlfriend wako, ila mawasiliano mabaya upo kama haupo. unalalamikiwa anasema inamuumiza wewe hujali eti upo busy. Hii imekaaje kwenu? sababu ni nini?

Tatizo kuna wanawake wanapenda mapenzi ua ISIDINGO... kila wakati bebi umekula, bebi umemaliza kazi, bebi umafanya hiki... kama mpo kazini mjue kile kitendo cha simu kuita pekee kinaharibu mtiririko wa ulichokuwa unakifanya, halafu mbaya unapokea simu iliyokuharibia mtiririko ndo unakutana na makorokocho ya kiisidingo... WHAT DO YOU EXPECT?

6. Ukiwa haupendi kutumiana message na haujaribu njia ingine, only kusubiri uandikiwe ndio hujibu hiyo imekaaje na reasons zako ni nini?

Hapa hakuna sababu moja kwa wote, zipo nyingi, na nikwambie mtu haanzi tu kutojibu sms kwa muda uutakao.. MSOME MTU WAKO KIPI HAPENDI NA ANAWEZA KUKISEMA NA KIPI HAPENDI LAKINI HAJASEMA... Siyo kwa sabau hajasema then you take for granted kwamba kila kisichosemwa basi KINAPENDWA... msome mtu wako.

SI ila wakati mtu ashike simu... kuna mamo mengine ya kufanya vile vile... AND YOU HAVE TO UNDERSTAND

7. Mwingine unakaa unamwambia mwenzako kuwa hupendi kuwasiliana, ila ukianza kuchat hata na wanawake marafiki unakuwa unajua kuandika kama cherehani. hii inakuwaje unamuumiza mwenza hivi? hapo anajua au anasikia au anaona. Hata ndugu zake unafanya hivyo bila shida, ila ikija kwake unadai unampenda mapenzi mengi bali mawasiliano sifuri kama vile unasukumwa, ni nini kinachojiri kwako.

Hapa ndo wanawake wengi wanakoseaga.... ntakujibu kwa kifupi.... KAMA UNACHOONGEA WEWE KILA SAA NI MALALAMIKO UNATEGEMEA NINI TOKWA KWA UNAYEMLALAMIKIA? Wengine mna GUBU hatari............. BY THE WAY, GUPU NI KITENDO CHA KUWASILISHA JAMBO KWA KUONGEA NA MWINGINE KWA NJIA YA MALALAMIKO TU.... yaani wewe hata kumuuliza mtu UMEKULA? unaiweka hivi... HIVI KINACHOKUFANYA UWE HUJALA MPAKA SASA NI NINI? Unategemea nini hapo?

8. Wanaume mnapenda kusumbua wanawake wawapende, mkiwapata tu mnaanza habari nyingi kama upo busy sana hata kusema kwa wiki mbili tatu utakuwa busy. Ukipata mkakubaliana mahusiano unabadilika, unakuwa sio yule msumbufu hata salamu hutoi asubuhi hapo mnaishi nyumba tofauti. Inakuwaje hivyo umfanyie mwenza hayo na hausemi sabau bali kuishi kuumiza roho ya mtu

Tatizo kubwa la binadamu ni kwamba, kwa kila kinachomtokea, ANAONA KWA 100% KIMESABABISHWA NA MTU MWINGINE... Kila mara jitahidi kujitazama... Hakuna kitu kama eti mnakorofishana na mwenza then 100% amekosea yeye... Kwenye kila kutoelewana kila mmoja ana percentage yake kwenye kusababisha kukorofishana huko kutokee... Sasa tatizo ni kwamba hamtazami michango yenu ni ipi.

Mwanaume anapomfuata mwanamke kunapercentage fulani ya factors anazozitaka kwa mwanamke ameziona kwake... Sasa kuna yale mamo ambayo huwezi jua mpaka uingie uonee ..... Kuna wengine wanakutana na vitu anaona bora ale kona

9. Mwanaume anasema kwa mwenza nitakupigia, inapita mawiki hata siku moja hajawahi kupiga hata missed call kutokea ika ukasema alikukumbuka, ni nini hupendi kama uko hivi sababu nini?

Wa hivi tayari usham-bore... We nenda zako... Na wakati uanenda zako jaribu kutafuta nini kimesababisha hali hiyo. Tatizo la wanawake walio wengi huwa mna-deal sana na outcome kuliko source... We badala ya kutafuta kwa nini hali ipo hivi, unahangaika na hali yenyewe... USIPOWEZA KUTAFUTA CHANZO, UNAWEZA UKAJIKUTA UNABADILISHA WANAUME KILA KUKICHA...

Acheni kuvikimia vivuli vyenu wakati uwezo wa ku-control jua lisiwake hamnao.....

10. Mwingine yake ni huko kwenye viber sijui imo, anatuma message kwa mpenzi anajibiwa. akiandika tena hata kuaga au kuuliza kitu, basi hajibiwi tena na hapo anaona mtu yupo online. Na baadae anaweza kuona mtu yupo online lakini wapi anauchuna..je ni hataki aandikiwe tena au anaona anasumbuliwa? je ni nini kama sio kuonyesha dharau, kweli unapata notification then unaiacha hata not read for over thre days hata wiki. mwanaume ni nini kinajiri?

Mwanaume kuwa na mpenzi wewe.. HAIMAANISHI KWAMBA AACHE MAWASILIANO NA WENGINE. HILI NI TATIZO KUBWA SANA KWA WANAWAKE WENGI... Yaani mnataka in the name ya mimi kuwa mpenzi wako, basi kuwa ONLINE ni wakati nawasiliana na wewe tu... Yaani ni kama nimeachana na marafiki, ndugu, jamaa, mates.... Wewe umenikuta nimesoma primary, secondary, vyuo mbalimbali na huko kwote nna watu ninaofahamiana nao... NAACHAJE KUWASILIANA NA HAO WOTE KIASA TU WAPENZI??

11. kwa wewe unayependa kutoa sababu mia, mia mbili, kwanini yote hayo?

Jichunguzeni.....
Hakuna atoae sababu bila sababu... Na muwe mnaambilika basi... Unajuwa kwa kawaida mwanamke anaongea sana kuliko mwanaume... Hiyo inawagharimu sana

YOTE TISA... KUMI SASA..
ILE TABIA YA KILA NIKICHELEWA NILIKUWA NACHEPUKA, KILA NISIPOPIGA SIMU NILIKUWA NACHEPUKA, KILA NISIPOJIBU SMS NILIKUWA NACHEPUKA, KILA NINAPOKUWA NA MARAFIKI, BASI WANANIUNGANISHIA MICHEPU....... hii ndo sababu kubwa sana ha yote hapo juu

tabia zenu za kuwakoromea wanaume kama watoto mliowazaa tena bado wadogo inawagharimu sana.... HUWEZI KUNIKOROMEA KAMA MTOTO AND ALL OF THE SUDDEN UHITAJI KITU TOKA KWANGU NA UKIPATE AS IF HUJANIKOROMEA....

WENGINE MNAISHIAGA KUPIGWA ILA MLIO WENGI MNAKALIWAGA KIMYA
 
Unajua kuna maswali matatu yaulizwayo na wanawake yaani yana kera
UKO WAPI? UNAFANYA NINI? NA NANI? yaani kama mkiweza hili bassi tena

alafu kitu kingine muache basi kuringa maana wanaume tuna hisia za muda na wanawake mna hisia za muda mrefu sasa inapotokea figisufigisu wanaume huwaga tunakimbia tu (mwanaume yoyote ni mzaifu wa mapenzi ila ana maamuzi akiamua kuachana na wewe basi ata umshaurije hawezi kukurudia)
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom