Je ni sahihi kwa watu kumzonga na kumzomea mwanamke kwa mavazi yake

Watanzania tunashangaza sana. Yaani udhalilishwaji na unyanyaswaji wa wazi kabisa na ulio dhahiri lakini eti wengine ama hawauoni au wanamlaumu mhanga?

Huyo dada wala hajavaa vibaya kihivyo. Na hata kama angekuwa amevaa vibaya HAKUNA HATA sababu kidoggo inayohalalisha yeye kuzongwa namna hiyo. Hata kama alikuwa kakiuka sijui mila na nini (kisingizio ambacho mimi nakikataa) bado alikuwa hastahili kufanyiwa alivyofanyiwa.

Kuna kitu nimeanza kukiona miongoni mwa Watanzania. Unaweza ukawaibia na wao wakaona ni kawaida tu. Unaweza ukawanyanyasa na wasione ubaya wowote na hata kumtetea mnyanyasaji. Ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu umetapakaa na watu wamekaa kimya tu kama mapopo.

Mdada wa watu kanyanyaswa na kudhalilishwa lakini hata baadhi ya wanawake kama vile wanaona alijisababishia. Poor her. A victim getting blamed. We have a loooooong long way to go.

At last mkuu nimekubali ile statement yako lakini this one should be very specific "Mitanzania ndivyo..." Yaani huwezi amini kuna hata hao wazee around usikute hawakufanya chochote kumsaidia huyo dada. Na labda walikuwa wanajisemea kimoyomoyo akome.

Unapoona jamii inasupport udhalilishaji, lynching, unyanyapaaji tena so selectively ujue kuna tatizo si kidogo!!!!!
 
Uhuru gani huo usio na mipaka, basi watu waruhusiwe tu, watembee uchi, na pia mtete pia biashara ya Ushoga na ukahaba...! Na uvutaji wa Bangi.
 
Unapoona jamii inasupport udhalilishaji, lynching, unyanyapaaji tena so selectively ujue kuna tatizo si kidogo!!!!!

Eeewaa! Mbaya zaidi ni pale ambapo baadhi ya watu wanaanza kumlaumu mhanga eti yeye ndo alijisababishia (wenyewe wanaita ku-provoke) hiyo kadhia kwa namna alivyovaa.

Bado tuna safari ndefu sana Nyambala.
 
Uhuru gani huo usio na mipaka, basi watu waruhusiwe tu, watembee uchi, na pia mtete pia biashara ya Ushoga na ukahaba...! Na uvutaji wa Bangi.

Kwanza kaongee na Wamasai wanaokataga mbuga huku mali zao zikining'inia kama tunguli za mganga! Lakini sitashangaa ukisema wao huo ndo utamaduni wao.

Huyo dada wala hakuvaa vibaya hivyo. Ni ushenzi, ufedhuli, na mfumo dume tu ndio uliopelekea yeye kupatwa na hiyo kadhia.
 
Wamasai wanavaa Lubega sikatai lakini nyuchi zao hazionekani kaka...! |Si kweli maneno yako.
 
Huyu ni MZUDHUNGU au MBOFONGO? Naamini 100% wewe mwenyewe huwezi kvaa hivyo. Mzungu hana matamanio.

Kama mawazo yenu bado finyu bora msidai tu hyo haki sawa kwa wote.

:A S thumbs_up:
 
Mimi nashangaa mtu anajihesabu mchamungu kisha anashabikia udhalilishaji kama huo.

Dini gani isiyoheshimu sheria?
 
Na ndio maana wakazomea.

Wewe na wenzako mnaomlaumu huyo dada mnashangaza. Ila hamna neno. Nyie kuweni kama mnavyotaka kuwa. Teteeni huo upuuzi nyuma ya pazia la tamaduni. Upakeni rangi ya mila huo ufedhuli wa hao wahuni. Na endeleeni kutetea maovu na kulaumu wahanga. Mimi nimemaliza kumpigia mbuzi gitaa. Adios.
 
Sawa mkuu, nahisi wewe unatetea haki za binadamu zilizo pitiliza ubinadamu...!

Anyway hatuna ugomvi zaidi kila mtu anatetea kile anacho kiamini.

Waweka mali zako nje zikiibiwa, unalalamika ooh! Nimeibiwa... Ajabu kweli kweli.
 
jamani,kwa hio wanawake hatuna freedom ya kuvaa kile tupendacho???
mie nailaumu serikali,kwa kuruhusu hii hali....
hapo ingetokea hao wazomeaji wakapata kash kash kidogo next time wasingezomea.....

eti tunajivunia Tanzania peaceful country....my as*
be blessed
peacefull country kwa wanaume tu yaani sisi hatuna haki ya kuvaa tutakavyo. aaah hapa si uarabuni watuache
 
nimacho yangu sijui...au nishazoea,minaona mbonaa kawaida tu...kweli tuache kuzalilisha dada zetu,chukuliaa kama MAMAA AKO,DADAA AKO,MDOGO WAKO AU MPENZI WAKO....ndo anafanyiwa hivyo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom